DC aagiza walimu wazinzi wakamatwe

DC aagiza walimu wazinzi wakamatwe

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,578
[h=2]MKUU wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi, ameagiza kukamatwa kwa walimu wawili na wengine wanne wa Shule ya Msingi Msoga, kutokana na kukiuka maadili ya utumishi. Kipozi alitoa agizo hilo jana, wakati akizungumza katika kikao cha pamoja baina yake na wazee wa Bagamoyo, viongozi wa dini na watendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo.[/h]
Mkuu huyo wa wilaya aliagiza kukamatwa kwa walimu hao, Samuel Mjema na Joel Mjema na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Kipozi alisema kuwa walimu hao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakikiuka maadili na kanuni za utumishi kwa kufanya ngono na wanafunzi wao, kitu ambacho ni kinyume cha kanuni na taratibu za utumishi.

“Kwa ujumla hatuwezi kuvumilia uchafu huu wa mtu anayepaswa kuheshimiwa kama mwalimu kuamua kuanza kuwashawishi na kufanya ngono na wanafunzi wake.

“Mbaya zaidi ni kuwakatishia masomo watoto hao, hivyo naagiza mara moja kukamatwa kwa walimu hao na kufikishwa katika mikono ya sheria,” alisema Kipozi.

Akizungumzia tuhuma za walimu hao, Kipozi alisema Mwalimu Joel Mjema anatuhumiwa kumbebesha mimba aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la sita wa shule hiyo.

Kwa mujibu wa Kipozi, mwalimu huyo alimpa mimba mwanafunzi Tatu Shaabani, hali iliyomfanya mwanafunzi huyo kushindwa kuendelea na masomo yake ya kuhitimu elimu ya msingi.

“Kama vile haitoshi, mwalimu huyo huyo alimjaza mimba na kupelekea kumkatisha masomo mwanafunzi mwingine wa kidato cha tatu wa Shule ya Sekondari Lugoba, Latifa Shaaban na kuamua kuishi naye kinyumba,” alisema.

Kuhusu Mwalimu Samuel Mjema, Kipozi alisema mwalimu huyo anatuhumiwa kutembea na mwanafunzi aliyemtaja kwa jina la Maimuna Hamis, ambapo alifumaniwa na wazazi wa mwanafunzi huyo.

“Jambo la kushangaza suala hilo lilimalizwa kimya kimya baina ya mwalimu huyo na wazazi na binti, vitendo hivi havikubaliki, wazazi ambao wamekuwa wakifikia makubaliano ya kuvunja sheria nao wachukuliwe hatua,” alisema.

Katika tukio jingine, mkuu huyo wa wilaya ameagiza kusakwa kwa wafugaji watatu wa jamii ya Kimasai ambao majina yao yamehifadhiwa kwa madai ya kuwavizia na kutaka kuwabaka wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ubena.

Kipozi alisema Wamasai hao wamejenga mtandao wao ambapo wamekuwa na tabia ya kuwavizia wanafunzi wasichana katika vichaka vilivyo katika njia ya kuelekea shuleni.
 
[h=2]mkuu wa wilaya ya bagamoyo, ahmed kipozi, ameagiza kukamatwa kwa walimu wawili na wengine wanne wa shule ya msingi msoga, kutokana na kukiuka maadili ya utumishi. Kipozi alitoa agizo hilo jana, wakati akizungumza katika kikao cha pamoja baina yake na wazee wa bagamoyo, viongozi wa dini na watendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo.[/h]mkuu huyo wa wilaya aliagiza kukamatwa kwa walimu hao, samuel mjema na joel mjema na kufikishwa katika vyombo vya sheria. Kipozi alisema kuwa walimu hao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakikiuka maadili na kanuni za utumishi kwa kufanya ngono na wanafunzi wao, kitu ambacho ni kinyume cha kanuni na taratibu za utumishi. “kwa ujumla hatuwezi kuvumilia uchafu huu wa mtu anayepaswa kuheshimiwa kama mwalimu kuamua kuanza kuwashawishi na kufanya ngono na wanafunzi wake.“mbaya zaidi ni kuwakatishia masomo watoto hao, hivyo naagiza mara moja kukamatwa kwa walimu hao na kufikishwa katika mikono ya sheria,” alisema kipozi. Akizungumzia tuhuma za walimu hao, kipozi alisema mwalimu joel mjema anatuhumiwa kumbebesha mimba aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la sita wa shule hiyo.kwa mujibu wa kipozi, mwalimu huyo alimpa mimba mwanafunzi tatu shaabani, hali iliyomfanya mwanafunzi huyo kushindwa kuendelea na masomo yake ya kuhitimu elimu ya msingi. “kama vile haitoshi, mwalimu huyo huyo alimjaza mimba na kupelekea kumkatisha masomo mwanafunzi mwingine wa kidato cha tatu wa shule ya sekondari lugoba, latifa shaaban na kuamua kuishi naye kinyumba,” alisema.kuhusu mwalimu samuel mjema, kipozi alisema mwalimu huyo anatuhumiwa kutembea na mwanafunzi aliyemtaja kwa jina la maimuna hamis, ambapo alifumaniwa na wazazi wa mwanafunzi huyo.“jambo la kushangaza suala hilo lilimalizwa kimya kimya baina ya mwalimu huyo na wazazi na binti, vitendo hivi havikubaliki, wazazi ambao wamekuwa wakifikia makubaliano ya kuvunja sheria nao wachukuliwe hatua,” alisema.katika tukio jingine, mkuu huyo wa wilaya ameagiza kusakwa kwa wafugaji watatu wa jamii ya kimasai ambao majina yao yamehifadhiwa kwa madai ya kuwavizia na kutaka kuwabaka wanafunzi wa shule ya sekondari ubena.kipozi alisema wamasai hao wamejenga mtandao wao ambapo wamekuwa na tabia ya kuwavizia wanafunzi wasichana katika vichaka vilivyo katika njia ya kuelekea shuleni.
hawa ni sawa na simba au chui wanaovizia ng'ombe na mbuzi badala ya swala na tandala wakamatwe na kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria miaka 30 na viboko 15 wakati wa kuingia na 15 watakapoachiwa ili wakawaoneshe wake zao ambao watakuwa vikongwe wakti huo
 
  • Thanks
Reactions: Ctr
Nchi hii haishi vituko hivi viongozi wa serikal hii wakisema wakamatwe wazinzi kuna mtu atabaki nje?ukianzia na juu kuleee.
 
Hawa wakuu wa Wilaya wa JK wa ajabu sana. Mkuu wa Wilaya anatoa order ya kijinga namna hii? Hapa hawa walimu wanaweza kushtaki kwa defamation. Kubaka ndio kosa la jinai na ni kazi ya polisi kushughulika na upelelezi si DC?
 
Unategemea nini pale mzazi wa mtoto "anapoyamaliza" na offender kifamilia? Una kesi tena hapo? Shahidi yako awe nani? Kwanza ukanda huo wote kumtia mimba mtoto wa mtu is not an issue! Cha msingi kajisalimishe kwa wazazi na uwape "mahari" yao. Vivyo hivyo hata kukamatwa ugoni (uzinzi) mitaa hiyo wanaita sunna! Huo ndio utamaduni wao, halafu wewe unakuja na matamko yanayokinzana na utamaduni wa watu, hakika huwezi fanikiwa. Enyi maDC, jitahidini sana kutambua tamaduni za jamii mnazoishi ili kazi zenu ziwe rahisi. Vinginevyo mnajitia aibu tu. Watu watakamatwa sawa na wataachiwa kama sio polisi basi Mahakamani kwa kukosa ushahidi!
 
Walimu pekee ndio wanaonekana kuwatia watoto washule mimba.Nani asiyeifahamu Bagamoyo?Mh.Dc aje na statistics za wanafunzi waliotiwa mimba mashuleni na watuhumiwa wote wafikishwe mahakamani na si mwalimu mmoja au wawili ndo wajadiliwe na kikako wakati wazinzi wengine wakiendelea kuharibu wanafunzi na wakijificha nyuma ya migongo ya walimu.
Kuna mwaka mwl.moja alitiwa hatiani kwa mwanafunzi kutiwa mimba.kesi ilikuwa hivi:
Mwanafunzi alitaja wanaume aliongonoka nao na kufikia idadi ya wanaume 30.
Kati ya hao kulikuwepo na jina moja la mwalimu.wakaamua ku mkomalia mwalimu bila kuangalia uhusika wake.
Mwl. alipo ulizwa alikiri kutembea na mwanafunzi mara moja,miaka miwili iliyopita.
Hivyo mwalimu akaachiwa huru kwa kuto husika kwenye kesi ya msingi ya kutia mimba.
My take:
DC asikurupuke,utafiti ufanyike kwa shule chache kuangalia ukubwa wa tatizo ili hatua za dhati zichukuliwe kutatua tatizo kwa ujumla wake na siyo kuwafanya walimu hao kondoo wa kafara wakati Bagamoyo ngono ni sehemu ya tamaduni zao
 
  • Thanks
Reactions: Ctr
Ingawa si mtu wa bagamoyo kikazi ama kwa kuzaliwa lakini si dhani kama tendo la uzinzi ni miongoni mwa tamaduni za kabila lolote lile,hivyo ni kosa kusema kuwa bagamoyo tendo la ngono ni utamaduni kwao,tusichanganye tabia,mihemko na utamaduni.
 
Huko si kule nyumbani kwa mkuu wa nchi? Fisi wameanza kula kwa mwenye nyumba kumwambia kuwa hana nguvu ya kuiongoza nchi kama hata primary yenyewe imemshinda pale nyumbani kwake. Yaani wamasai wanajifika vichakani kuwabaka wanafunzi? Tanzania tunaenda wapi na huyu kiongozi ambae hata kijijini kwake hakuna kitu?
 
Nchi hii haishi vituko hivi viongozi wa serikal hii wakisema wakamatwe wazinzi kuna mtu atabaki nje?ukianzia na juu kuleee.

Nilipoona eti walimu wazinzi wakamatwe nilishtuka sana. Lakini baada ya kusoma nikagundua ni walimu wanaofanya uasherati na wanafunzi. nilishtuka kwa sababu suala la uzinzi hawaweze kukamatwa walimu tu. lakini kama wamethibitishwa kufanya uasherati na wanafunzi wao wanastahili adhabu kali. Hili ndilo tatizo la kutokuwaona wanafunzi kama dada au watoto na kuwaona ni watu wazima. Sasa ukishamvulia nguo hiuyu binti atakuwa anakusikiliza wakati unamfundisha? Na je, pindi atakapofanya kosa unaweza kumwadhibu? Hiki nacho ni chanzo kingine cha wanafunzi kufeli mtihani. Ebu jaribu kuwaza mtoto ametoka nyumbani kwao hajanywa chai halafu anakutana na mpuzi fulani ambaye yuko tayari kumrubuni kwa kumpa shilingi 5,000. Unadhani atazikataa? Imeniudhi sana. Mbona kuna makahaba kibao kama hawajaoa? Hao walimu waadhibiwe sawasawa na sheria za nchi na kanuni za utumishi wa umma.
 
hawa ni sawa na simba au chui wanaovizia ng'ombe na mbuzi badala ya swala na tandala wakamatwe na kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria miaka 30 na viboko 15 wakati wa kuingia na 15 watakapoachiwa ili wakawaoneshe wake zao ambao watakuwa vikongwe wakti huo
mkuu hiyo ni vema kabisa,nikitazama kwa jicho la 3 naona ni kama mtu anae kamatwa na ngozi ndiye aliye kula nyama.Nasema hivyo kwa sababu kwa ujumla maadili kwa sasa hakuna c kwa waalimu wala wanafunzi na mbaya zaidi hali mbaya ya maisha na utandawazi kwa ujumla wake.watoto wadogo wanajua mambo makubwa mpaka unashangaa kaona au kusikia wapi.Sasa basi mianya kama hiyo na awali ya mtu,haijalishi awe mwalimu au mtu mwingine yeyote yule kama ndiyo mwenendo wake ni mpaka yamkute au ashikwe na ngozi.Mkuu kuna wengine ni wakali sana katika mambo hayo utackia tetesi tu na wala wataalamu ki vyao.SASA TUFANYEJE?kama kweli mkuu wa wilaya anataka kukamata waalimu wazinzi,mi nashauri ALAMATE YEYOTE YULE ANAE WALA WANAFUNZI-AENDE SHULE MOJA BAADA YA INGINE-WAPE KARATASI WANAFUNZI WA KIKE WAANDIKE MAJINA YA WATU NA ANUANI ZAO AMBAO AMEWAHI KUWA NAO-ILA WASIANDIKE MAJINA YAO.Anaweza zimia kwa presha kwani si ajabu akakuta mmoja au hakuna ambaye hajawahi kujamiiana.Lakini kukamata sampo tu ya wa wili!c amini kama ndio kupunguza au kumaliza tatizo,MKUU WA WILAYA KAPIGISHE KURA YA SIRI-KUTOKA HAPO UTAJUA CHA KUFANYA.
 
Huko si kule nyumbani kwa mkuu wa nchi? Fisi wameanza kula kwa mwenye nyumba kumwambia kuwa hana nguvu ya kuiongoza nchi kama hata primary yenyewe imemshinda pale nyumbani kwake. Yaani wamasai wanajifika vichakani kuwabaka wanafunzi? Tanzania tunaenda wapi na huyu kiongozi ambae hata kijijini kwake hakuna kitu?

akipeleka bandari kule mnahunya hunya.
 
Nchi hii haishi vituko hivi viongozi wa serikal hii wakisema wakamatwe wazinzi kuna mtu atabaki nje?ukianzia na juu kuleee.
wazinzi kwa wanafunzi? madhara ya taahira kuwa karibu na keyboard.
 
Hawa waalimu ni ndugu? Majina na tuhuma zao zimefanana.
 
sawa... ashughulikiwe ila mimi natoa kazi ya kufikiria idadi ya wazinzi sanasana wasio walimu na waliopo kwenye nyadhifa za juu za utawala wa nchi!
 
Nilipoona eti walimu wazinzi wakamatwe nilishtuka sana. Lakini baada ya kusoma nikagundua ni walimu wanaofanya uasherati na wanafunzi. nilishtuka kwa sababu suala la uzinzi hawaweze kukamatwa walimu tu.

Kwa kweli JF is never boring!!!!!...nimevunjika mbavu baada ya kuisoma hii!!!!
 
DC amekosea kutaja majina ya wabakwaji hadharani, Huyu kipoi ni mwandishi ina maana Viyoyozi vya miaka miwili vimegandisha weledi wake haraka hivi?
 
Wachina wakijenga bandari na kuhamia Bagamoyo,watazalisha wachina wazaramo wengi hadi tukitaka wachina watujengee nyumba na mabarabara tutakuwa nao humu humu nchini.
 
Back
Top Bottom