Dayosisi mpya ya Ruvuma kuzinduliwa Leo.

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
21,369
Reaction score
27,785
Habari wana Jamii Forums.

Leo kutakuwa na shughuli kubwa ya uzinduzi wa Dayosisi mpya ya Ruvuma.

Mkuu wa kanisa la KKKT Dr. Alex Malasusa akiambatana na maaskofu kutoka dayosisi mbalimbali nchini pamoja na wachungaji, wainjilisti na watumishi wengine wanashiriki uzinduzi huu, mchungaji Amon Joel Mwenda anategemewa kusimikwa kuwa Askofu wa dayosisi hii mpya ya Ruvuma.

Mh. Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda anategemewa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huu.
 
Kila la heri Dayosisi mpya ya ELCT, jambo kubwa na la muhimu ni kujiepusha na tamaa za kujitajirisha kupitia zaka hatimaye kuliingiza kanisa kwenye mifarakano isiyokwisha
 
Namshukuru Mungu kwa kuanzishwa kwa Dayosisi hii na kumchagua Mchungaji Mwenda kuwa Askofu wa kwanza wa RUDI (Ruvuma Diocese). Nimepita maeneo hayo na nilichojifunza ni kwamba Dayosisi hii imeanzishwa lakini ni Maskini. Haina kitegauchumi wala kituo chochote cha huduma za jamii. Kwa miaka mingi vituo na vitegauchumi vimewekezwa maeneo mengine ya Dayosisi mama (Dayosisi ya Kusini).

Hata hivyo waumini wa Dayosisi hii mpya sio maskini na ni wapenda maendeleo kwani kwa kipindi kifupi waliweza kujenga nyumba za ibada kama Ruhwiko, Seed farm, Msamala, Mshangano, Tunduru inaendelea n.k. Naamini kwa umoja huo wanaweza kuweka vitegauchumi na huduma za jamii tukashangaa baada ya miaka mitano.

Nawaombea kwa Mungu awazidishie moyo wa kujitoa kwa maombi, hali na mali. Tuheshimu na kutoa ushirikiano kwa uongozi wetu ili dayosisi hii changa ikue na kusonga mbele. Ule Msemo wenu niliousikia pale kanisani Msamala uendelee kwani ujenzi wa Dayosisi ni wa kudumu. HAYA NA TUONDOKE - TUIJENGE DAYOSISI YA RUVUMA.

Mungu baba wa Bwana wetu Yesu Kristo wa Nazareti awajalie na kuwaongezea kwa kipimo cha kujaa na kusukwasukwa. Na mwishoni awafute machozi sawasawa na neno lake kwa taabu mliyoipata hapa Duniani. AMEN
 
Hongereni wanaruvuma, natumai ningekuwepo mahali hapo, nami pia ni mmoja kati ya watu waliokuwepo kipindi vuguvugu la kujenga dayosisi.

Kuhusu kitega uchumi, walikuwa na mpango wa kujenga Ghorofa hapo makao makuu, ila sijajua wameishia wapi.

HAYA NA TUONDOKE, TUKAIJENGE DAYOSISI YA RUVUMA.
 
Back
Top Bottom