DOKEZO Dawati la Jinsia Polisi Chang'ombe lichunguzwe kwa kupiga danadana tukio la mwanafunzi Kibasila kudhalilishwa na mwalimu wa kiume

DOKEZO Dawati la Jinsia Polisi Chang'ombe lichunguzwe kwa kupiga danadana tukio la mwanafunzi Kibasila kudhalilishwa na mwalimu wa kiume

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Babamiye

New Member
Joined
Jul 23, 2025
Posts
2
Reaction score
1
Oktoba 29, 2024, Mwanafunzi wa kike aliyekuwa anasoma Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Kibasila iliyopo Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam aliripoti tukio la kupigwa vibaya na kudhalilishwa na Mwalimu wa Kiume wa shule hiyo

Mama Mzazi wa Binti huyo amejitokeza na kuomba Dawati la Jinsia lililopo Polisi Chang'ombe lichunguzwe kutokana na kushindwa kushughulikia kesi ya mtoto wake na kumpiga danadana kwa muda wa miezi 10 sasa huku tukio hilo likiwa limemuathiri vibaya binti yake kimwili na kiakili.

Akielezea tukio la kushambuliwa Binti yake ambalo lilitokea Oktoba 24, 2024 Mama huyo anasema siku hiyo akiwa nyumbani kwake Mbezi Louis jijini Dar es Salaam majira ya saa tisa mchana binti huyo alirudi nyumbani na kumwangukia miguuni huku akiwa analia kwa uchungu. Anadai alipomwangalia mtoto alimuona akiwa amevimba uso huku sehemu mbalimbali za mwili zikiwa zimevimba na kuvilia damu.

''Kiukweli nilishtuka sana'' anasema Mama huyo kwa uchungu na kuongeza ''nilianza kumtuliza kwanza ili aweze kunisimulia kilichotokea huku nikiwa nimepeleka mawazo yangu kwenye ajali'' alisisitiza

Anaendelea kueleza kuwa baada ya kama nusu saa hivi binti alianza kumsimulia kile kilichotokea. Binti huyo aliyekuwa amebakiza siku 10 tu kuanza mitihani yake ya kuhitimu kidato cha nne, alisema ile ilikuwa sio ajali ya barabarani bali alishambuliwa na mwalimu mmoja wa kiue shuleni aliyemtaja kwa jina moja la Deus kwa fimbo na makofi.

''Nilipomwuliza kilichosababisha mwalimu ampe adhabu kubwa kiasi kile akasema eti kwa alivaa viatu ambavyo sio sare ya shule'' akasema na kuongeza '' viatu vyenyewe tuliagizwa na shule tuwanunulie kwa ajili ya mahafali yao ambayo ilifanyika siku mbili kabla'' alisema.

Anasema, alimpeleka binti hospitali ambao alitakiwa kwenda Polisi kuchukua Fomu ya Polisi Na. 3 (PF3), ambapo alipimwa na kutibiwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani.

Kesho yake Oktoba 25, 2024 aliongozana na Binti pamoja na Baba yake kwenda shuleni kupata taarifa zaidi ya kile kilichotokea na kusababisha binti kuadhibiwa kiasi kile. Baada ya kufika shuleni na kumtafuta Mkuu wa Shule, aliwaelekeza kwenda kwa Msaidizi wake ambaye hata hivyo pamoja na kuona jinsi mtoto livyokuwa ameumizwa alisema tu kuwa atamkanya mwalimu husika.

''Tulikuwa tunataka atukutanishe na Mwalimu Deus pamoja na Kamati ya Nidhamu ili kujua pengine mtoto ana makosa mengine lakini aliztuzungusha hadi Oktoba 29 2024 tulipoamua kwenda kuripoti kwenye Dawati ili mtoto aweze kupata haki yake'' anasema Mama huyo

Walipofika kwenye Dawati la Jinsia la Kituo cha Polisi Chang'ombe, waliandikishwa maelezo na Station Sergeant Focus ambaye aliwataka wachukue RB na kwenda kumkamata mtuhumiwa Mwalimu Deus ambaye baadaye alitoka kwa dhamana.

Tangu siku hiyo amekuwa akifuatilia kesi hiyo kwa Afande Focus ambaye amekuwa akimjibu kuwa bado hajamfanyia mahojiano Daktari aliyemfanyia mtoto uchunguzi jambo ambalo lilichukua miezi minane pamoja na kwamba Daktari huo ni mwajiriwa wa serikali na anapatikana kwenye kituo chake cha kazi na namba yake anayo na inapatokana.

Mama huyo anasema baada ya kuona afande huyo wa Dawati anampiga chenga, ilipofika Juni 12, 2025 alimtafuta Mkuu wa Kituo ambae naye alimwelekeza kwa Mpelelezi (Inspector) Mariamu ambaye alimwagiza Afande Focus amletee na baada ya kuliangalia akaagiza lipelekwe kwa Waendesha Mashtaka.

''Baada ya hapo alinitaka nirudi nyumbani ambapo baada ya wiki moja nilipompigia simu Inspekta alinipa namba ya Waendesha mashitaka na kunitaka niwasiliane nao'' anasema kwa uchungu na kuongeza '' Hadi kufikia tarehe 11 Agosti 2025, Waendesha Mashtaka wananiambia faili limerudi Dawati linahitaji marekebisho.

Mama wa Binti anasisitiza kuwa kesi hiyo ya mwanawe ni miongoni mwa kesi kadhaa alizozikuta kwenye Dawati hilo la Jinsia Chang'ombe ambazo alikutana na watu wanaolalamika kupigwa danadana na mafaili yao kupotezwa, na kushauri uchunguzi ufanyike ili Dawati hilo na Madawati mengine nchini yaweze kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake.
 
Back
Top Bottom