DAWASCO Inakera saaaaana sana, mapato yanapotea. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

DAWASCO Inakera saaaaana sana, mapato yanapotea.

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by ngoshwe, Jan 2, 2012.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kuna mashirika yanapaswa kubadili mfumo wake wa Utendaji kazi. Katika kuwezesha wateja kulipia bili zao kwa wakati DAWASCO wametoa mifumo mbalimbali ya malipo ikiwemo M-Pesa, NMB Mobile nk lakini cha kusikitisha, unapojaribu kulipia bili yako ya maji kupitia mifumo hiyo pengine huduma haipatikani kabiosa, na unaweza kukata tamaaa hasa ukitumia NMB Mobile.Unapoomba maelekezo kutoka kwa watendaji wa Shirika hilo wanakuambia kulipia kupitia njia hizo mbadala kunachelewesha shirika kupokea malipo na haikuwezeshi kupata stakabadhi mpaka uende tena ofisini kwao. Hii ni urasimu usio wa lazima na unaisababishi Serikali kupoteza mapato mengi. Aidha, tofauti na wakusanya Kodi kama TRA ambao wanatewmbea na mashine za kukukatia risiti wanapofuatilia walipa kodi, kwa DAWASCO ni tofauti, msoma mita akija kwako kusoma mita pengine anakuwa hana rekodi kamili ya unachodaiwa (hana kumbuklumbu ya mita yako) na akija atakutaka wewe ndio umpe risiti uliyolipia mara ya mwisho ili ajiridhishe .Msomaji huyo akisoma na kubaini unadaiwa, anataka ukalipie Ofisini kwao ili upate risiti vinginevyo atakukatia maji ili ukilipa ndipo urejeshewe tena..huu ni upuuzi na kushindwa kutimiza wajibu..kwa nini mashirika kama DAWASCO yasiwe na utartibu wa wasoma mita kutumika kukusanya Bili moja kwa moja kwa wateja badala ya kuwasababishia wateja usumbufu usio na msingi wa kwenda kupanga foleni Ofisini??? Ni kiasi gani cha fedha zinazopotea kwa mteja ambae ametumia maji kwa kliwango kikubwa lakini badala yake akaishia kukatiwa maji na kuachwa tu ili arejeshewe baada ya kulipia bili?? DAWASCO hamuoni kuwa wapo wateja ambao wao shida sio kulipa bili bali wanakosa muda wa kufika Ofisini kwenu kulipa au kufuatilia risiti tu za malipo baada ya kulipa ??? Hamuoni unapoteza wateja na Serikali kupoteza mapato??..kwa nini wananchi wasijiunganishie maji kihuni kama ninyi hamna mkakati wa kuwafanya waheshimu sheria bila shuruti wana usumbufu ??
   
 2. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #2
  Jan 2, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Ipo siku watabadili mfumo....mabadiliko yanaendana na muda na wakati kwa wahusika....watakuwa bado wanajipanga tu ila ukweli wanaujua
   
 3. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  na tanesiko waambie basi
  wanakata umeme siku za sikukuu ili waje kutengeneza
  afu mutaoe kiaina
   
 4. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #4
  Jan 2, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  hiyo dudu inaitwa Tanesco acha kabisa ni kama askari wa Trafiki ambae siku ya sikukuu unamkuta barbarani tena amejificha anavizia madereva wafanye makosa ili awachomoe "posho" ya sikukuuu
   
 5. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #5
  Jan 2, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Tanesco ndo noma bora hawa dawasco..si wa mikoani hatuwajui zaidi ya Tanesco
   
 6. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #6
  Jan 3, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mkuu huko hakuna Mamlaka zozote za Maji Safi na Taka ?? au Mnapataje maji??

  Tanesco kufulu kabisa...hao watabadilika tu wakipata mshindani kama ilivyokuwa TTCL zamani wakati wa simu za kuzungusha!!
   
Loading...