DAWASCO huenda imelemewa

DAWASCO huenda imelemewa

tungatagaga

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2024
Posts
672
Reaction score
913
Jiji la dar Lina idadi kubwa ya watu kuliko miji mwingine nchini.Na idadi hiyo inayokadiriwa m.8 inazidi kuongezeka.
Mojawapo ya huduma mhimu katika maisha ya binadamu ni maji safi na salama.Maeneo flani hapa dar kama huku kinyerezi tulikuwa tupata maji mara tatu kwa wiki hivi Sasa tunaweza kupata mara Moja kwa wiki mbili.Hii inaonyesha kulemewa kwa watoa huduma huku afya za wananchi zikiwa hatari
Ningeshauri serkali itafute wawekezaji wa upatikanaji wa huduma ya maji kwa wakazi wa dar na kuipunguzia mzigo Dawasco.
Pili dawasco iweke mpango wa ratiba ya maji kwa Kila eneo kwa siku nzima ili hata waliopembezoni wapate
Fungeni leakage zote.
Hali ni mbaya kama mnavyofikiria
 
Mkuu,nimeshangaa hata mbeya mjini Pana mgawo mkali sana wa maji,maji hutoka mara 1 kwa wiki 2 tena saa tisa usiku🤔!hii nchi ngumu sana
 
Vyanzo vya mito kama Wami na Rufiji
Vitamaliza kabisa tatizo la maji ukanda huu hasa Dar es salaam inayokua kwa kasi
 
Jiji la dar Lina idadi kubwa ya watu kuliko miji mwingine nchini.Na idadi hiyo inayokadiriwa m.8 inazidi kuongezeka.
Mojawapo ya huduma mhimu katika maisha ya binadamu ni maji safi na salama.Maeneo flani hapa dar kama huku kinyerezi tulikuwa tupata maji mara tatu kwa wiki hivi Sasa tunaweza kupata mara Moja kwa wiki mbili.Hii inaonyesha kulemewa kwa watoa huduma huku afya za wananchi zikiwa hatari
Ningeshauri serkali itafute wawekezaji wa upatikanaji wa huduma ya maji kwa wakazi wa dar na kuipunguzia mzigo Dawasco.
Pili dawasco iweke mpango wa ratiba ya maji kwa Kila eneo kwa siku nzima ili hata waliopembezoni wapate
Fungeni leakage zote.
Hali ni mbaya kama mnavyofikiria
Ni jambo la kustaajabisha kweli,kwa teknolojia ilivyokua sana kwa miaka ya hivi karibuni bado tunakabiliana na tatizo la ukosefu wa maji kwenye jiji kubwa nchini,ambapo tuna vyanzo zaidi ya viwili vinavyoweza kutupa maji ya uhakika kwa wakazi wote.
 
Mkuu,nimeshangaa hata mbeya mjini Pana mgawo mkali sana wa maji,maji hutoka mara 1 kwa wiki 2 tena saa tisa usiku🤔!hii nchi ngumu sana
Mwanza Kuna ziwa la pili kwa ukubwa Duniani, maji ni ya mgao inaweza pita hata wiki hakuna maji, na bili zinakuja Tena kubwa tu, Sasa sijui tatizo ni nini. MUNGU anisamehe nahusisha suala hili na mambo ya siasa. Sioni sababu yoyote ya Mwanza kukosa maji wakati huo kahama, shinyanga mpaka tabora wanatumia maji hayo hayo na hawalalamiki. Mtandao uliounganisha mwanza mpaka tabora wakaazi wa mkoa huo wangelitakiwa tatizo la maji walisikie kwenye mikoa isiyokuwa na vyanzo vya maji vya uhakika.
 
Inashangaza sana,mpaka huwa najiuliza sisi ni kipi cha maana tumeweza kifanya 100% bila dosari.
 
Yami ni kero kubwa sisi wa Mbezi Msumi tuna miezi mitatu sasa hatun maji halafu wanakuja kusoma mita. Hii ni maajabu!
 
Back
Top Bottom