TAARIFA KWA WAKAZI WA DAR ES SALAAM NA PWANI
TAARIFA YA UPUNGUFU WA HUDUMA YA MAJI
6.12.2025
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawataarifu wateja na wananchi wanaohudumiwa na mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Chini (Kuanzia maeneo ya Bagamoyo, Tegeta, Boko, Mbezi Beach, Mwenge, Kinondoni, Mwananyamala, Masaki hadi Ilala) kuwa kumekuwa na upungufu wa huduma ya maji katika maeneo mengi kutokana na uzalishaji wa Maji kushuka zaidi ya kiwango cha kawaida kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kushuka kwa kina cha Mto Ruvu iliyosababishwa na kuchelewa kwa Mvua.
Kwa mtambo wa Ruvu Juu katika maeneo ya kuanzia Kibaha, Kibamba, Kimara, Tabata, Kinyerezi, Pugu hadi Kisarawe hali ya uzalishaji maji inaendelea vizuri na huduma inawafikia wananchi.
Jitihada mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa kwa kushirikiana na Wizara ya Maji ikiwemo kusitisha matumizi ya Maji ya Mto Ruvu kwenye shughuli za Kilimo na kuyaelekeza katika matumizi ya Binadamu tu na kuongeza matumizi ya Visima ili kupunguza changamoto ya ki-huduma.
DAWASA itaendelea kutoa taarifa za kila wakati juu ya hali ya upatikanaji Maji kwa Wananchi ili waweze kujiandaa na shughuli muhimu za kiuchumi.
Tunawaomba Wananchi kuendelea kuhifadhi Maji yanayopatikana kwa matumizi muhimu
DAWASA inaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza
Wasiliana nasi Kituo cha huduma kwa wateja 181 (bure) na 0735 202-121 (WhatsApp tu)
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano.
181
Malipo Bila
WhatsApp Pekee 0735 202 121
Tutembelea kwenye tovuti yetu www.dawasa.go.tz
Barua Pepe
Mitandao ya kijamii
info@dawasa.go.tzdawasatz