DAWASA yatoa mkono wa Eid kwa makundi ya Wahitaji Kijitonyama

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) katika hatua ya kujali na kuthamini makundi maalumu katika jamii, imetoa msaada wa mahitaji ya kibinadamu katika kituo cha Makao ya Kulea Watoto Yatima, kilichopo mtaa wa Nzasa, Kata ya Kijitonyama Wilaya ya Ubungo.

Hatua hii ni sehemu ya mpango wa Mamlaka wa kuthamini na kujali nafasi ya makundi maalumu katika jamii.

1742894712488.png
Akizungumza wakati wa utoaji wa msaada wa vitu mbalimbali vilivyowasilishwa ikiwemo vyakula, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Mkama Bwire amesema kuwa upo umuhimu mkubwa wa jamii kuwajali na kuthamini makundi maalumu hususani watoto ambao wanaishi katika mazingira magumu.

1742894830308.png
"Kwa kuwajali watoto hawa kutasaidia kuwatengeneza mazingira mazuri katika ukuaji wao ili waweze kufanikiwa kiuchumi na kuweza kuwa viongozi wa baadae," amesema Mhandisi Bwire.

Amepongeza kazi kubwa inayofanywa na walezi wa kituo hicho ya kuwatunza na kuwaongoza watoto hao katika misingi mizuri, na kuahidi DAWASA kuendelea kushirikiana na kituo hicho katika kusaidia ukuaji mzuri wa watoto hao ikiwemo kuchangia gharama za kuwasomesha shule pamoja na matibabu ya afya.

1742895107811.png
Kwa upande wake Hassan Hamisi, mlezi Mkuu wa kituo hicho ameishukuru DAWASA kwa kuwajali na kuwashika mkono kwa mahitaji ya kibinadamu pamoja na kueleza nia ya Taasisi ya kuwasaidia kimasomo.

"Ni jambo la faraja sana kwetu kupata msaada wa kuendelea kuwalea watoto hao," amesema.

Amesema kituo hicho kwa sasa kina jumla ya watoto 86 ambao wengine wanasoma na wengine bado ni wadogo wanaobaki kulelewa, hivyo misaada hiyo itatusaidia kuongeza ufanisi katika kuwahudumia na kuwakuza watoto hawa.

1742895138614.png
 
Mbona sioni issue yoyote inayohusu kwaresma? Au kwa kuwa Rais muislam? Hata TV channels km TBC na Channel Ten vipindi vya Iddi vingi sana ila sijawahi ona kuhusu
Mfungo wa kwaresma
 
Back
Top Bottom