DAWASA na hujuma ya maji Kibamba Kibwegere

Rufiji dam

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
3,801
8,782
Wakazi wa Kibamba delini, Kibwegere tunalalamikia DAWASA Kimara kwa kushindwa kuturekebishia bili za maji ambazo wametubambika tofauti na bili halisi, tumelalamika zaidi ya miezi 8 sasa hakuna ufumbuzi, matokeo tunashindwa kulipa bili halisi na deni halieleweki, bili tunazotumiwa na mita inavyosoma vitu tofauti.

Tatizo si kwetu tu hadi Kibwegere, Hondogo. Waziri husika na hujuma hizi zifutilie.
 
Nadhani kuna matatizo makubwa kwa wasoma bili wengi wao sio waadilifu, hawafuati maadili ya kazi zao, udanganyifu na pia kuto kuheshimu wateja, lugha mbovu, nadhani tatizo hilo lipo kila kona ya jiji la DSM.

Mhe. Waziri Awesu baadhi ya hawa wasoma bili wanatia doa wizara ya maji.

Wananchi wengi wa DSM wanamalalmiko ya kubambikiziwa bili na jambo hili linafanywa na wasoma mita kwa lengo la kujipatia kitu kidogo kutoka kwa wateja hakika jambo hili limekuwa kero sana.
 
Back
Top Bottom