Mamlaka zinazohusika ziangazie DAWASA kibaha,niliwahi kufuatiliaji maji nikazungushwa
nikaomba kumuona meneja,katibu mhutasi akanidanganya kwamba meneja hayupo
kaenda kwenye kikao.
Mungu si athumani papo hapo wakaingia watu kutoka wizara ya afya
wanakagua mazingira ya utekelezaji wa mapambano dhidi ya korona,yule mama akaona kigugumizi
akiangalia ameishanidanganya kwamba meneja hayupo,na hawa wakubwa wanamtaka meneja
ikabidi aingie ofisini ampashe habari,wale wageni wakaruhusiwa kuingia. Mimi kuona hivyo na muda wangu ukikuwa mdogo
nikaondoka,ila nilisikitika kuona mama wa makamo anasema uongo mchana kweupe,na ni mtumishi wa umma.