Dawa za viagra erecto katika supu ya pweza

Dawa za viagra erecto katika supu ya pweza

FbUser

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2014
Posts
439
Reaction score
644
Tahadhari kwa wale wanywaji wa supu ya Pweza wauzaji wameanza kuichanganya na vidonge vya kuongeza nguvu za kiume aina ya erecto ili wanywaji waione kuwa inawasaidia kuinogesha ligi ya kitandani 'stadium'
Uchunguzi huu umethibitishwa zaidi na baadhi ya watumiaji nikiwemo mwenyewe kuwa unapotumia inakuletea nguvu zisizo za kawaida na tayari niliwaeleza marafiki tunaotumia huku Buguruni tunakugundua hali hiyo na jana jioni tulipomvamia yule kijana wa kipemba kulitaka thermos lake liwe mikononi mwetu aligoma kulitoa hadi mzee mmoja mwenye busara akamwombea samahani huku akimtaka akiri kuwa ni kweli akaomba samahani rafiki yangu akataka pia aseme anatuwekea dawa gani akagoma akasema sio yeye ni tajiri wake anaempa hiyo supu basi sakata likaanza upya
Alipoona tumemnyang'anya thermos na yeye tunamlazimisha twende polisi huku watu wakiwa wamejaa akasema kuwa huwa anasaga vidonge vya erectro vi3 kwa thermos moja ndipo tulipomwaga supu yote kwa mathemos makubwa mawili na tukaachana nae. Hii ni hatari kwani vidonge vya erectro ni viagra kali sana na ina madhara kwa wagonjwa wa moyo na pressure BP na kwa wengine wakiwa adicted hupoteza kabisa nguvu za kiume hadi watumie vidonge hivyo ambavyo viko katika maduka mengi ya dawa. TFDA walione hili lakini Mabwana afya ndio zaidi wawajibike.
 
Nimegonga kitu cha pweza pale mwenge jana then nikazuka home wife aliipata pata!one hour no dwn !
60th mini game over!wife mikono juu!maana hajazoea !
 
Kuna baadhi ya vyakula ni muhim kuandaliwa nyumbani.
Msiooa mnapata tabu saaaana.

Mie supu ya pweza na aina yoyote ya supu hutengenezewa nyumbani na Wife.

Nje ya nyumbani nitakula vyakula vya kawaida,kama wali,nyama,maharage,mchicha nk.

Ila kwenye Pweza huwa sipatikani mitaaani,na ifahamike kwamba kuna namna ya uandaaji wa supu hii.
 
Back
Top Bottom