Dawa za mfadhaiko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dawa za mfadhaiko

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Feb 18, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 18, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Dawa za mfadhaiko


  [​IMG]
  Fluoxetine (Prozac), ni SSRI  [​IMG]
  Venlafaxine, ni SNRI

  Dawa za mfadhaiko ni dawa za ugonjwa wa akili zinazotumika kupunguza mivurugo ya halihisi ya moyo, kama vile mfadhaiko mkubwa na ukataji tamaa na hali ya wasiwasi kama vile woga wa kuingiliana na watu. Dawa kama vile vizuia oksidesi vya monoamini(MAOIs), dawa dhidi ya mfadhaiko aina ya trisaikliki (TCAs), dawa dhidi ya mfadhaiko aina ya

  tetrasaikliki (TeCAs), vizuizi vya uchukuzi wa serotonini kinachochagua (SSRIs), na vizuizi vya uchukuzi wa serotonini-norepinefrini(SNRIs) ndizo zinazohusishwa kwa kawaida na neno hilo. Dawa hizi ni mojawapo kati ya zile ambazo kwa kawaida huagizwa na wataalamu wa magonjwa ya akili na madaktari wengine, na ufanifu pamoja na athari zao ni mada ya

  tafiti nyingi na madai mengi yanayoshindana. Dawa nyingi husababisha athari za dawamfadhaiko, lakini vikwazo kuhusu matumizi yao yameleta utata unaosababishwa na matumizi yao kwa kutibu maradhi mengine mbali na yale yaliyokusudiwa hatari, licha ya madai kuwa yana ufanisi wa kiwango cha juu.

  Ufanifu wa dawamfadhaiko ya kisasa aina ya thaimoleptiki haijawahi kudhihirishwa kikamilifu kuwa ni bora zaidi ya ule wa kipozaungo hai, kulingana na kaguzi mbili za shirika la Cochrane Collaboraton. Ukaguzi wa tafiti zote kuhusu dawamfadhaiko zilizowahi kuwasilishwa kwa FDA, zile zilizochapishwa na zile ambazo hazikuchapishwa, zilizowasilishwa kwa

  FDA katika mwaka wa 2004. Kwa maandishi yaliyochapishwa, tibamifadhaiko ilikuwa na mafanikio ya 94% katika kutibu mfadhaiko. Kwa maandishi ambayo hayakuchapishwa, mafanikio yalikuwa ni chini ya 50%.Kwa ujumla, tafiti zote

  zilionyesha ufanisi wa 51% - pointi mbili tu zaidi kuliko ile ya kipozaungo. Hii iliongeza dhahiri ufanifi wa dawamfadhaiko tofauti kutoka 11% hadi 69% zaidi ya kipozaungo. Dawa ambayo huenda ikawa ni tofauti na ile ya mirtazepine- pinzani ya

  norepinefrini na serotonini, yenye athari zilizo kinyume na zile za SSRI na SNRIS - na venlafaksini, SNRI iliyo na usawa katika mfumo wa kemikali kwa kiwango kikubwa na tramadoli ya afyuni iliyonyumbuliwa.

  Afyuni zilitumika kutibu mfadhaiko wa kiwango cha juuu hadi mwishoni mwa miaka ya 1950. Ampfetamini zilitumika hadi katikati ya miaka ya 1960. Kuagiza afyuni au amfetamini kwa kutibu mfadhaiko ni jambo linaloleta utata kisheria. Utafiti

  kuhusu uwezo wa afyuni ya kunyumbuliwa wa kutibu mfadhaiko umefanywa mara chache tu katika kipindi cha miaka sitini iliyopita, ili hali amfetamini zimepata soko linalostawi kwa hali mbalimbali kama vile maradhi ya upungufu wa makini,

  nakolepsi, na unene wa kupindukia na zinaendelea kuchunguzwa kwa matumizi mengi. Afyuni na amfetamini zote husababisha mwitiko wa haraka sana wa matibabu. Huonyesha matokeo kwa muda usiopita masaa ishirini na manne hadi

  arobaini na manane; uwiano wa matibabu kwa afyuni na amfetamini ni mkubwa kuliko ule wa dawamfadhaiko aina ya trisaikliki. Katika baadhi ya tafiti hizi zenye vikwazo vikuu, buprenofini ya afyuni imeonyesha uwezo mkubwa wa kutibu mfadhaiko mkali ulio sugu kwa matibabu wa dawa yoyote inayojulikana katika utafiti mdogo ambao kwa ujumla ilitambuliwa na kuchapishwa mwaka wa 1995, lakini haijawahi kufwatiliwa kutokana na unyanyapaa wa kijamii unaohusishwa na afyuni

  pamoja na ile inayohusishwa na ugonjwa wa akili nchini Marekani.
  Aina nyingi za dawamfadhaiko zinazofanana na asili huchelewa kuanza utekelezaji kwa (kati ya wiki 2-6) na kwa kawaida hutolewa kwa muda wa wakati wowote kati ya miezi hadi miaka. Licha ya jina hilo, dawamfadhaiko mara nyingi hutumika kwa

  njia ya ubishi, na katika muktadha wa upungufu wa ushahidi unaotegemea majaribio kusaidia dalili zao, matumizi ya dawa kutibu maradhi mengine bali na yale yaliyokusudiwa awali, kama vile hali ya wasiwasi, ugonjwa wa akili ambapo mtu huwa na kiwango cha juu cha tamaa au shauku, matatizo ya kula, maumivu sugu, na baadhi ya hali zinazotatiza urazini wa

  upatanisho wa homoni kama vile hedhi chungu. Zikiwa peke yao au pamoja na kinza msukosuko (kwa mfano Tegretoli au Depakote), dawa hizi zinaweza kutumika kutibu upungufu makini wa kupepesuka (ADHD) na matumizi mabaya ya dawa kwa kushughulikia mfadhaiko msingi. Pia, dawamfadhaiko zimetumika wakati mwingine kutibu kukoroma na vipandauso.

  Dawa zingine ambazo kwa kawaida haziitwi dawamfadhaiko, ikiwa ni pamoja na vizuia magonjwa ya akili vya vipimo vya chini na benzodiazepini, zinaweza kutumika kwa kudhibiti mfadhaiko, ingawa benzodiazepini - pamoja na dawa zote zinazoitwa

  "dawamfadhaiko" - husababisha utegemezi wa mwili. Kuacha matibabu ya benzodiazepini (au SSRI) kwa ghafla kunaweza kusababisha dalili zisizopendeza za kuachishwa. Kizinduo cha mmea wa St John's Wort hutumika kwa kawaida kama dawamfadhaiko, ingawa imealamishwa kama kijalizo cha chakula katika nchi zingine. Neno dawamfadhaiko wakati mwingine

  hutumiwa kwa tiba (kwa mfano, matibabu ya kisaikolojia, tiba ya msukosuko ya umeme, tiba vitobo) au mchakato (kwa mfano kuvuruga usingizi, kuongezeka kwa kiwango cha mwanga, mazoezi ya mara kwa mara) yametambulika kama njia za kudhibiti mfadhaiko wa kimawazo.

  Vipozaungo tepetevu vinaweza kuleta athari kuu za dawamfadhaiko, kwa hivyo, ili kudhibitisha Dutu kama "dawamfadhaiko", katika utafiti wa kiafya wa kliniki ni muhimu kuonyesha ukuu wake ukilinganishwa na kipozaungo.

   
 2. princess ariana

  princess ariana JF-Expert Member

  #2
  Dec 13, 2016
  Joined: Aug 19, 2016
  Messages: 4,433
  Likes Received: 5,965
  Trophy Points: 280
  Jamani haya matatizo ya saikolojia ,wasi wasi & woga yananimaliza
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Dec 17, 2016
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Nitafute nipate kukutibia
   
Loading...