Dawa za magonjwa ya kuku

sumu-ya-panya

JF-Expert Member
Aug 6, 2016
632
572
Habari wana jamii
Mimi ni kijana nilie ajiriwa sekta binafsi na pia nimejiari pia katika ufugaji wa kuku wa kienyeji.
ijapokua sina uelewa na baadhi ya madawa ya kuku na magonjwa yao.

Wapo kuku nilimwona anachechemea,yupo mwenye kinyesi chenye rangi kama damu,naomba msaada na pia nataka kuwapa chanjo ya newcastle, nidawa gani ninunue na bei zake

asante
 
Kuna chanjo inayowapa kwa kudondoshea tone kwenye jicho inaitwa thermostable 1-2
Hiyo kuhara damu unaweza kuwapa cooccidiostat.
 
Hbr ya mwaka mpya.hiyo ya kudondoshea tone mwenye jicho.dozi yke ipo vp?maana niliulizia maduka matatu tofauti nikapewa maelekezo tofauti
 
Ipo mbona karibu maduka mengi ya mifugo ila ni chanjo.

ipo mkuu ila jinsi ya kuitumia,duka LA kwanza waliniambia ninaweka tone moja kwa kila kuku,kila baada ya miezi mitatu,duka la pili walinieleza tone moja kwa kila kuku,nakaa siku 21 narudia tena kuwapa,duka La tatu waliniambia nawapa tone moja,baada ya siku 7 nawapa tena,nikaa tena siku 7 nawapa nimekuwa nimeshamaliza dozi.sasa sielewe kwa maelezo hayo yupi ni sahii.
 
Mi ninavyotumiaga na kwa mujibu wa jarida LA haifer international, baada ya kuwapa chanjo siku ya kwanza nasubiri tena baada siku 21 baada ya hapo kila baada ya miezi mitatu.
 
Nakumbuka bibi yangu alikuwa anazuia magonjwa na vifo vya kuku kwa kuwapa Alovera tu katika maji, sina hakika kama miaka hii itafanya kazi pengine magonjwa mapya ya ndege yamejitokeza.
 
Habari wana jamii
Mimi ni kijana nilie ajiriwa sekta binafsi na pia nimejiari pia katika ufugaji wa kuku wa kienyeji.
ijapokua sina uelewa na baadhi ya madawa ya kuku na magonjwa yao.

Wapo kuku nilimwona anachechemea,yupo mwenye kinyesi chenye rangi kama damu,naomba msaada na pia nataka kuwapa chanjo ya newcastle, nidawa gani ninunue na bei zake

asante
Pole na changamoto mkuu.Magonjwa yanayosumbua kuku ni mengi.Ila magonjwa hatari kabisa ni magonjwa yanayosababishwa na Virusi.namaanisha NEW CASTLE,GUMBORO,,MAFUA MAKALI(mafua makali ni tofauti na na mafua ya kawaida.na ukumbuke kuwa magonjwa yanayosababishwa na virusi mengi HAYATIBIKI.Kwa ufupi magonjwa yanayosumbua Kuku wako yanatibika.Huyo anaeharisha damu mpe otc 20 au otc plus.na hakikisha vyombo unavyotumia na maji unayowapa ni safi mda ote.anaechechemea mchunguze vizuri maranyingi hupata majeraha ndani ya banda kama kuna vidonda kuna dawa fika duka lolote la mifugu utapata maelekezo
 
Nakumbuka bibi yangu alikuwa anazuia magonjwa na vifo vya kuku kwa kuwapa Alovera tu katika maji, sina hakika kama miaka hii itafanya kazi pengine magonjwa mapya ya ndege yamejitokeza.
alovera ni ni nzuri kwa kuku kwani inawafanya kuku wachangamke sana na pia wanakua haraka haraka
 
Wewe ndo umeuliza muda huu habari za Ufugaji hata ratiba ya chanjo huna hakika, Mara ushajua alovela wanasaidia Kuku kukua haraka? Au ndo mambo ya kusikia kwenye TV?
 
Pole na changamoto mkuu.Magonjwa yanayosumbua kuku ni mengi.Ila magonjwa hatari kabisa ni magonjwa yanayosababishwa na Virusi.namaanisha NEW CASTLE,GUMBORO,,MAFUA MAKALI(mafua makali ni tofauti na na mafua ya kawaida.na ukumbuke kuwa magonjwa yanayosababishwa na virusi mengi HAYATIBIKI.Kwa ufupi magonjwa yanayosumbua Kuku wako yanatibika.Huyo anaeharisha damu mpe otc 20 au otc plus.na hakikisha vyombo unavyotumia na maji unayowapa ni safi mda ote.anaechechemea mchunguze vizuri maranyingi hupata majeraha ndani ya banda kama kuna vidonda kuna dawa fika duka lolote la mifugu utapata maelekezo
Samahani bumblefoot na fungus ni sawa dawa yake nini
 
Boss Ushauri mzuri ila mara nyingi otc 20% inadunda ama kufanya kazi pole pole so ingefaa zaid otc 50% inanguvu kuliko 20.
 
Habari wakuu. Moja kati ya vifaranga wangu anatatizo ambalo sijawahi kulisikia wala kuliona. Anajikunja na kuficha kichwa chake chini ya miguu. Leo ni siku ya pili, hali wala kunywa. Nimempiga picha lakini nimeshindwa kuzituma huku, sina uzoefu sana. Naomba msaada kwa anayelijua tatizo na namna ya kulitatua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
501c6f89d8028b6bda2cda6e2e9a1d49.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom