Dawa za kulevya za mabilioni zakamatwa

Dawa za kulevya za mabilioni zakamatwa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,037
Reaction score
34,742
Zilitokea Dar kwenda Afrika Kusini
headline_bullet.jpg
Wakamatwa wanawake wawili

Christopher%20Shekiondo.jpg

Mwenyekiti wa Tume ya Kuthibiti Dawa za Kulevya, Christopher Shekiondo

Dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8 zimekamatwa nchini Afrika Kusini wakati zikisafirishwa kutoka Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka nchini humo, wanawake wawili walikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Oriver Tambo uliopo eneo la Kempton Park siku ya Ijumaa wiki iliyopita wakitokea Tanzania.

Wanawake hao walikamatwa wakiwa na mabegi sita ambayo yalipokaguliwa yalikutwa na kilo 150 za dawa hizo ambazo pia zinajulikana kama ‘Tik’.

Baada ya kukamatwa na dawa hizo wanawake hao walikabidhiwa polisi.

Mwenyekiti wa Tume ya Kuthibiti Dawa za Kulevya, Christopher Shekiondo, alipotafutwa alisema hajapata taarifa hizo na aliahidi kufuatilia.

"Sijapata taarifa za tukio hilo lakini nitafuatilia kujua kama kweli wanawake walitoka Tanzania," alisema Shekiondo.

Hivi karibuni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, katika taarifa yake ilisomwa kwa niaba yake na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, mjini Dodoma, katika maadhimisho ya kitaifa ya ‘Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani’ alisema tatizo la dawa hizo ni janga la kitaifa hivi sasa nchini.

Alisema kumekuwa na wimbi kubwa la Watanzania wanaojiingiza katika biashara haramu ya dawa za kulevya ndani na nje ya nchi na kwamba, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, watuhumiwa 10,799 walikamatwa kwa kujihusisha na dawa hizo.

Pia alisema katika kipindi hicho, Watanzania 240 walikamatwa katika nchi za Brazil, Pakistan na Afrika Kusini, kuharibu taswira ya nchi na kusababisha Watanzania wasio na hatia kupata usumbufu na masharti magumu wanapotaka kusafiri kwenda nchi mbalimbali duniani.

Alisema mwaka huu pekee kumekuwa na ukamataji mkubwa wa dawa za kulevya katika eneo la kimataifa la Bahari ya Hindi karibu na Tanzania.

Pinda alisema hivi sasa mikate, maandazi na askrimu zinazouzwa kwenye shule za msingi, zinawekwa dawa za kulevya.

Alisema vitendo hivyo vinafanya vijana wengi wa shule za msingi na hata sekondari kuwa na tabia za ajabu, ikiwamo kuingia darasani wakiwa na kiatu kimoja mguuni, mkufu wenye nyembe na kidani chenye nyembe kifuani.

CHANZO: NIPASHE

WANAWAKE WAWILI WAMEKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA KATIKA UWANJA WA NDEGE WA AFRIKA KUSINI WAKITOKEA TANZANI

Ripoti kutoka Afrika Kusini zinasema wanawake wawiliwamekamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa OR Tambo nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania, wakiwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya Rand million 42.6 kiasi ambacho ni kikubwa zaidi kuwahi kukamatwa katika mpaka wowote wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyoripotiwa na shirika la habari la Africa Kusini SABC siku ya Ijumaa (July 5), msemaji wa South African Revenue Services (SARS) Marika Muller amesema, wanawake hao waliowasili na ndege kutoka Tanzania, walikutwa na mabegi 6 makubwa yaliyojaa madawa (crystal meth) yenye thamani ya Rand 42.6 million ambayo ni sawa na zaidi ya billion 6 ya Tanzania.

Muller aliendelea kusema baada ya mizigo yao kuanza kukaguliwa ndipo timu ya maafisa uhamiaji iligundua kilo karibia 150 za madawa katika mizigo yao, kiasi ambacho ndio kikubwa kuwahi kukamatwa kama mzigo mmoja katika mpaka wowote wa Africa Kusini.

“When searching their luggage which was six large bags of black holdall bags, the customs team found just less than 150 kilos of crystal meth that is what we also call Tik in South Africa.

Those drugs are valued at R42.6 million which makes it the single largest seizure by the SARS customs team at any border in South Africa.” Alisema Muller.

Wanawake hao ambao hawakutajwa majina wala uraia wameshikiliwa na polisi nchini Afrika Kusini.

Tazama video yenye habari hiyo

Last edited by a moderator:
Serikali ya Tanzania imelala usingizi wanaowatumia wananchi wao kubeba mizigo ya Madawa ya Kulevya ni wageni watu kutoka Afrika Magharibi wanaoishi hapo nchini Tanzania. Wa-Tanzania amkeni fuatilieni Wageni wote haswa watu weusi ambao sio Raia wa Ki-Tanzania ndio wanaoharibu nchi yetu.
 
Zilitokea Dar kwenda Afrika Kusini
headline_bullet.jpg
Wakamatwa wanawake wawili

Christopher%20Shekiondo.jpg

Mwenyekiti wa Tume ya Kuthibiti Dawa za Kulevya, Christopher Shekiondo

Dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8 zimekamatwa nchini Afrika Kusini wakati zikisafirishwa kutoka Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka nchini humo, wanawake wawili walikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Oriver Tambo uliopo eneo la Kempton Park siku ya Ijumaa wiki iliyopita wakitokea Tanzania.

Wanawake hao walikamatwa wakiwa na mabegi sita ambayo yalipokaguliwa yalikutwa na kilo 150 za dawa hizo ambazo pia zinajulikana kama ‘Tik’.

Baada ya kukamatwa na dawa hizo wanawake hao walikabidhiwa polisi.

Mwenyekiti wa Tume ya Kuthibiti Dawa za Kulevya, Christopher Shekiondo, alipotafutwa alisema hajapata taarifa hizo na aliahidi kufuatilia.

"Sijapata taarifa za tukio hilo lakini nitafuatilia kujua kama kweli wanawake walitoka Tanzania," alisema Shekiondo.

Hivi karibuni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, katika taarifa yake ilisomwa kwa niaba yake na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, mjini Dodoma, katika maadhimisho ya kitaifa ya ‘Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani’ alisema tatizo la dawa hizo ni janga la kitaifa hivi sasa nchini.

Alisema kumekuwa na wimbi kubwa la Watanzania wanaojiingiza katika biashara haramu ya dawa za kulevya ndani na nje ya nchi na kwamba, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, watuhumiwa 10,799 walikamatwa kwa kujihusisha na dawa hizo.

Pia alisema katika kipindi hicho, Watanzania 240 walikamatwa katika nchi za Brazil, Pakistan na Afrika Kusini, kuharibu taswira ya nchi na kusababisha Watanzania wasio na hatia kupata usumbufu na masharti magumu wanapotaka kusafiri kwenda nchi mbalimbali duniani.

Alisema mwaka huu pekee kumekuwa na ukamataji mkubwa wa dawa za kulevya katika eneo la kimataifa la Bahari ya Hindi karibu na Tanzania.

Pinda alisema hivi sasa mikate, maandazi na askrimu zinazouzwa kwenye shule za msingi, zinawekwa dawa za kulevya.

Alisema vitendo hivyo vinafanya vijana wengi wa shule za msingi na hata sekondari kuwa na tabia za ajabu, ikiwamo kuingia darasani wakiwa na kiatu kimoja mguuni, mkufu wenye nyembe na kidani chenye nyembe kifuani.

CHANZO: NIPASHE

Hawa watu wako wengi sana Tanzania. Naweza kusema idadi kubwa ya wanawake wanaojiita mafashionista wote ni wazungu wa unga pamoja na wale wenye ma-boutique. Yaani ni kitu kinachoeleweka na sijuwi kwanini serikali yetu haifuatilii haya mambo.
 
Hicho kilichokamatwa ni TONE katika BWAWA KUBWA tuu!!!!! Sasa kama yameaanza kuchanganywa hadi kwenye RAMBARAMBA aka ice-cream za mashuleni ina maana wanawafanya watoto wetu wawe mateja mapeema!!!!!Eee MUNGU tuokoe na hawa wenye kujali hela ya biashara hii bila kukubali kuangalia madhara yake katika jamii
 
Serikali ya Tanzania imelala usingizi wanaowatumia wananchi wao kubeba mizigo ya Madawa ya Kulevya ni wageni watu kutoka Afrika Magharibi wanaoishi hapo nchini Tanzania. Wa-Tanzania amkeni fuatilieni Wageni wote haswa watu weusi ambao sio Raia wa Ki-Tanzania ndio wanaoharibu nchi yetu.

mkuu wahusika wakuu hata jk anawafahamu, acha kusingizia wageni mkuu!
umesahau orodha aliyopewa JK na Makamba?
 
kama serikali imeshindwa kuwazibiti hawa wana haram inabidi tuwakataze watoto wetu kula mandazi
 
Serikali ya CCM ni Janga la kitaifa.rai wenu alipewa orodha hadi leo hamna alichokifanya.sasa mna shangaa nini?Sioni kama serikali iko serious katika hili.Hawa akina shekiondo ndio wala rushwa ,halafu utegemee wauza unga papa wakamtwe?
 
kama serikali imeshindwa kuwazibiti hawa wana haram inabidi tuwakataze watoto wetu kula mandazi
Wakati Mh. Halima Mdee anachangia bajeti juzi alisema mambo mengi mazuri lakini lililonivutia na la kweli zaidi ni kusema 'kama wameshindwa waondoke'. Kuwazuia watoto kula mandazi ni kuwaonea tu
 
Kweli, hili ni janga la kitaifa, kuna haja ya serikali na jamii ya wabongo kuliangalia hili kwa karibu.
 
Can not understand!
Ule usumbufu tunaoupata kwenye check in imekuwaje mabegi hayo yote yapite un noticed..Officers on duty on that particular day were involved.mkianza nao mtajua nani aliwahonga wafumbe macho
 
Back
Top Bottom