Dawa za bilioni 5/- zaharibika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dawa za bilioni 5/- zaharibika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MpendaCHADEMA, Apr 4, 2012.

 1. M

  MpendaCHADEMA Member

  #1
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WAKATI Watanzania katika maeneo mengi wakilalamikia ukosefu wa dawa, imebainika kuwa dawa zenye
  thamani ya Sh bilioni 4.7 zilizonunuliwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii zimeharibika.

  Wabunge wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) wamehoji dawa hizo za thamani kubwa hivyo kuharibika wakati wananchi wakikosa dawa kwenye zahanati nyingi hasa vijijini.

  Eneo lingine ambalo wabunge wamehoji ni kiasi kikubwa cha fedha zinazochukuliwa na Mamlaka ya Dawa na Chakula (TFDA) wakati inapokagua dawa zilizoagizwa na Serikali.

  Kamati hiyo ilielezwa jana Dar es Salaam, kuwa TFDA inatoza asilimia mbili ya thamani ya dawa zinazonunuliwa na Serikali au zinazotolewa na wahisani hali iliyosababisha Bohari ya Dawa (MSD) kuwa na deni la Sh bilioni 45.

  “Kwa nini TFDA itoze Wizara mama fedha nyingi kiasi hiki, hivi kweli wanastahili kulipwa Sh bilioni 4 kwa kuchunguza dawa zinazoingia nchini, ni kitu gani kinafanywa na Mamlaka hii?” alihoji John Chenyo ambaye ni Mwenyekiti wa PAC na Mbunge wa Bariadi Mashariki.

  Cheyo aliongeza kuwa Sheria inayoipa TFDA kutoza kiasi hicho cha fedha ni mbovu; kwani gharama zinazolipwa na Serikali kwa Mamlaka hiyo, mzigo wake unakwenda kwa wagonjwa. Alisema: ”TFDA ni watoa huduma si wafanyabiasha

  Source: Habari Leo

  My take:
  Habari za tetesi nilizonazo ni kwamba baadhi ya vigogo hununua dawa hizi tayari zikiwa zimeharibika kwa bei chee ( huku wakihadaa kuwa ni nzuri)...na kwa kuwaonea wananchi huruma ya kuwapa dawa mbovu wanazihold kwa muda halafu wanasingizia kuwa zimeharibika!
   
Loading...