Herbalist Dr MziziMkavu Platinum Member Joined Feb 3, 2009 Posts 43,114 Reaction score 34,957 May 16, 2015 #1 KWA UFUPI Tamati hapa nafika, wahairi nijibuni, Nipate kupumzika, ndoa yangu kuthamini, Natamani kuachika, ila watoto jamani, Dawa ya wivu ni nini? Nijibuni wahisani Mhariri langu swali, litue kwako mezani, Inahofu yangu hali, jibu liwe makini, Kimara wala si mbali, makazi yangu Jijini, Dawa ya wivu ni nini? Nijibuni wahisani. Ndoa iso muhali, kuoana kwa hisani, Wazazi walikubali, tufunge ndoa nyumbani, Tukafunga Kihalali, Na wasia kutupeni, Dawa ya wivu ni nini? Nijibuni wahisani. Ghafla kabadilika, mume wa ubani, Kutwa anakarahika, si mchana si jioni, Jambo asilo hakika, aniweka hatiani, Dawa ya wivu ni nini? Nijibuni Wahisani. Moyoni nasononeka, nyumba kukosa amani, Mawazo yamenifika, raha kamwe sioni, Jikoni ninapopika, ametulia pembeni, Dawa ya wivu ni nini? Nijibuni Wahisani. Kazini ninapotoka, hima nipite chumbani, Nieleze kwa hakika, ratiba yangu njiani, Nani alonitamani, kutaja niwe makini, Dawa ya wivu ni nini? Nijibuni wahisani Hodi jirani kafika, ajighubika chumbani, Nia yake muafaka, asikie yasemwani, Kisha anapoonoka, maswali tele kinywani, Dawa ya wivu ni nini? Nijibuni wahisani. Nisije kubabaika, bzipo mwilini, Hapo ndipo huridhika, mume wangu wahisani, Pumziye humshuka, kama atoka mbioi, Dawa ya wivu ni nini? Nijibuni wahisani, Waungwana natabika mume, huyu mume gani? Unyumba ulo hakika, ninampa kwa yakini, Hila za kila dakika, atabuni kitandani, Dawa ya wivu ni nini? Nijibuni wahisani, Penzi letu mashakani, wawili tulimo ndani, Nusura yaitajika, wahisani nijibuni, Wapi alipokwazika, kuniweka kifungoni, Dawa ya wivu ni nini? Nijibuni Wahisani, Tamati hapa nafika, wahairi nijibuni, Nipate kupumzika, ndoa yangu kuthamini, Natamani kuachika, ila watoto jamani, Dawa ya wivu ni nini? Nijibuni Wahisani, MAGDALENA MAREGESI (SIWEMA), SIMU 0713 840996 Dar es Salaam chanzo.DAWA YA WIVU NINI? - Swahilihub
KWA UFUPI Tamati hapa nafika, wahairi nijibuni, Nipate kupumzika, ndoa yangu kuthamini, Natamani kuachika, ila watoto jamani, Dawa ya wivu ni nini? Nijibuni wahisani Mhariri langu swali, litue kwako mezani, Inahofu yangu hali, jibu liwe makini, Kimara wala si mbali, makazi yangu Jijini, Dawa ya wivu ni nini? Nijibuni wahisani. Ndoa iso muhali, kuoana kwa hisani, Wazazi walikubali, tufunge ndoa nyumbani, Tukafunga Kihalali, Na wasia kutupeni, Dawa ya wivu ni nini? Nijibuni wahisani. Ghafla kabadilika, mume wa ubani, Kutwa anakarahika, si mchana si jioni, Jambo asilo hakika, aniweka hatiani, Dawa ya wivu ni nini? Nijibuni Wahisani. Moyoni nasononeka, nyumba kukosa amani, Mawazo yamenifika, raha kamwe sioni, Jikoni ninapopika, ametulia pembeni, Dawa ya wivu ni nini? Nijibuni Wahisani. Kazini ninapotoka, hima nipite chumbani, Nieleze kwa hakika, ratiba yangu njiani, Nani alonitamani, kutaja niwe makini, Dawa ya wivu ni nini? Nijibuni wahisani Hodi jirani kafika, ajighubika chumbani, Nia yake muafaka, asikie yasemwani, Kisha anapoonoka, maswali tele kinywani, Dawa ya wivu ni nini? Nijibuni wahisani. Nisije kubabaika, bzipo mwilini, Hapo ndipo huridhika, mume wangu wahisani, Pumziye humshuka, kama atoka mbioi, Dawa ya wivu ni nini? Nijibuni wahisani, Waungwana natabika mume, huyu mume gani? Unyumba ulo hakika, ninampa kwa yakini, Hila za kila dakika, atabuni kitandani, Dawa ya wivu ni nini? Nijibuni wahisani, Penzi letu mashakani, wawili tulimo ndani, Nusura yaitajika, wahisani nijibuni, Wapi alipokwazika, kuniweka kifungoni, Dawa ya wivu ni nini? Nijibuni Wahisani, Tamati hapa nafika, wahairi nijibuni, Nipate kupumzika, ndoa yangu kuthamini, Natamani kuachika, ila watoto jamani, Dawa ya wivu ni nini? Nijibuni Wahisani, MAGDALENA MAREGESI (SIWEMA), SIMU 0713 840996 Dar es Salaam chanzo.DAWA YA WIVU NINI? - Swahilihub
tejateja JF-Expert Member Joined Feb 26, 2015 Posts 1,626 Reaction score 979 May 16, 2015 #2 That's yo best companion on earth. Shikilia huyo huyo. Wengine tukienda bar tunarudi siku ya pili yake hatunaga wivu....
That's yo best companion on earth. Shikilia huyo huyo. Wengine tukienda bar tunarudi siku ya pili yake hatunaga wivu....
I ISIMBA Senior Member Joined Feb 7, 2013 Posts 144 Reaction score 30 May 17, 2015 #3 As i am a professional docta, dawa ya wivu ni metakelfin za italy na hedex... Try it wadau mtakija kunipa feedback...
As i am a professional docta, dawa ya wivu ni metakelfin za italy na hedex... Try it wadau mtakija kunipa feedback...