Dawa ya vipele kwenye ngozi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dawa ya vipele kwenye ngozi

Discussion in 'JF Doctor' started by nnunu, Mar 8, 2011.

 1. nnunu

  nnunu JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 656
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Habari?,

  Samahani naomba niambiwe tiba ya vipele kwenye ngozi kwa mtoto au doctor bingwa zaidi wa magonjwa ya ngozi kwa watoto.


  Nimezunguka kwa madoctor wengi sana hapa ,mfano agakhan,tmj,tumaini,Dr hammeir,Dr ndodi na amepimwa vipimo mbalimbali hajaonesha kama ana tatizo lolote.

  Kwenye suala la usafi namfanyia usafi wa hali ya juu sana,hajawahi kurudia kuvaa nguo,nguo zake ni matilio ya pamba,anaoga mara 2 asbh na jion,vitu vyake vya kuchezea nasafisha kila wiki, chakula chake namwandalia mwenyewe mara nyingi.

  Baadhi ya ma DR walishauri asipewe sukari,soda,juise za viwandani vyote hivyo nimezingatia,juise nampa niliyotengeneza mwenyewe bila kuweka sukari,ila uji wake namwekea asali ilihakikishwa na mtaalam wa asali kuwa ni asali nzuri, na chakula chake anapewa visivyokobolewa hata unga wa uji natengeneza mwenyewe kwa usalama zaid.

  Kwa bahati nzuri muda mwingi nipo naye kwasababu ni mjasiriamali so muda wa kuwa pamoja nawe naupata bila tatizo. Japo hapati homa, wala haumwi umwi, shule anaenda bila tatizo na darasani anafanya vizuri sana, tatizo NGOZI YAKE SIYO NYORORO MUDAMWINGI ANA VIPELE VIDOGO VIDOGO VYA JOTO, havimwashi wala kumuuma, nimempaka mafuta ya nazi nilitengeneza mwenyewe,haijasaidia, sasa hivi nampaka vaseline ya watoto na kumwogeshea sabuni ya mbuni, niliacha kutumia johnson baby nilipoona haimsaidii.

  Doctor wa mara ya mwisho alisema suluhisho ni kuishi naye sehemu za baridi kwa sababu joto la Dar linamwathili, ila mvua ikinyesha siku 3 au zaidi na joto likipingua anakuwa na ngozi nzuri mpaka inapendeza,kuna kipindi nilisafiri naye kwenda lushoto alikuwa na ngozi nzuri kupita kiasi kwa sababu kule kuna baridi sana,niliporudi naye Dar vipele vikarudi tena,pia joto likiongezeka vipele vinaanza tena.

  Sijawahi kumpaka dawa za cream kwa kuhofia kuharibu kinga yake ya ngozi.Kama dawa ni kuishi naye sehemu ya baridi ,je hakuna dawa ya kutibu tatizo hili?, na mwisho wa tatizo hili ni miaka mingap?? ana miaka 5 sasa.

  Nampenda sana mwanangu napenda kumwona akiwa na ngozi isiyo na kipele kama zilivyo ngozi za watoto wengine pamoja na ngozi zetu sisi wazazi wake, tafadhali naomba msaada wenu.

  Pia samahani kwa kuandika ndefu inaweza kuwachosha ,nisamehe katika hili nia yangu ni kutoa maelezo ya kutosha.

  Asanteni.
   
 2. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Sasa wewe daktari kashakushauri na mengine ulishafanya ukaona mabadiliko kwa mwanao.
  Unataka ushauri gani tena jamani?
  Haya mpake karolaiti.
   
 3. k

  kamili JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 714
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Dawa ya vipele kwenye ngozi........????
  Bila hata kuandika kwamba unampenda sana mwanao, maelezo yako yanaonesha kwamba unampenda mwanao kupindukia na hili mimi naona ni jambo jema sana. Wasiwasi wangu ni hizo tiba unazutumia hivi ni za muhimu kweli? Mwenyewe umeshathibitisha kuwa ni joto ndio linaharibu ngozi ya mwanao. Na kama ni joto hakuna dawa inayoweza kumtibu isipokuwa kama una uwezo wa kubadilisha hali ya hewa au kwa kumhamisha kwenda sehemu ambazo hazina joto, au fedha ambazo unazitumia kwa wataalamu waweza zitumia kwa kubadilisha mazingira ya nyumbani. Hapa nina maana chumba anacholala kiwe na singbpard zuri, madirisha makubwa ambayo hayana top, na ikiwezakana umuwekee na kiyoyozi. Kwa sababu mara nyingi joto linaloumiza sana ni lile la usiku kitandani. Na tena hakikisha kama ni muhimu kujifunika shuka usiku basi ajifunike shuka nyepesi ya pamba. Na mchana avae nguo nyepesi za pamba.
  Mafuta ya nazi unayompaka ni miongoni mwa mafuta yanayongeza joto, ndio maana watoto wachanga huwa wanapakwa mafuta hayo ili wasipate baridi.
  Kuwa makini na baadhi ya ushauri unaopewa hasa kwa masuala ya chakula, mafuta, na dawa, kumbuka siku hizi ni soko huria, na tuna wataalamu huria. Kuna watu wanatangaza wana dawa zimethibitishwa hata na mkemia mkuu kumbe................ ukiwa na tatizo tosheka na wataamu wetu wanaolipwa mshahara na serikali yetu ambao mshahara huo hata wewe umeuchangia kupitia kodi yako.
  Mpe pole atapona.
   
 4. N

  Nalonga JF-Expert Member

  #4
  Mar 12, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Habari nzuri,pole sana kwa tatizo la ngozi ya mwanao.....nadhani kwa kupitia maelezo yako inaonekana mtoto wako anamzio (allergy) na hakuna dawa mahususi ya mzio,zaidi ya kuepuka vile viamshi vya huwo mzio,nenda hospitali akafanyiwe skin test ili kuweza kujua ni nini huwa ina trigger hiyo allergy yake ili uweze kumuepusha navyo....Pia jaribu kwenda katika kituo kimoja cha tiba za kichina kipo pale Magomeni mikumi ukajaribu dawa zao.
   
 5. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,016
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  M-post ulaya, esp Kiev au Moscow atapaenjoy
   
 6. nnunu

  nnunu JF-Expert Member

  #6
  Mar 13, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 656
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Asante kwa ushauri wenu mzuri, kuhusu mafuta ya nazi nimepata uelewa nilikuwa sijui kama yanaongeza joto na ndiyo maana hayakumsaidia kabisa kipindi nampaka...kuhusu kubadilishabadilisha ma dr hili nimelizingatia sana nina mwaka sasa sijaenda tena hospitali kutibiwa hivi vipele vya joto, huwa naenda kwa matatizo mengine tu. Baada ya dr bingwa wa watoto aliyeniambia kuwa dawa pekee ni kuishi naye sehemu zenye baridi ...kila nipatapo nafasi najitahidi kwenda naye mikoa yenye baridi ili angalau aondokane navyo na hakika ngozi yake inakuwa laini na nyororo kipindi chote tunachokuwa wote huko. Nawashukuru sana sana wote mliotoa ushauri wenu,,asanteni...japo huyo aliyesema nimpake kalorite kidogo ameniumiza lakin nimemsamehe kwa 7bu kila mtu kikatiba ana uhuru wa kutoa maoni yake ........tutaendelea kuwasiliana jf.
   
 7. k

  kasinge JF-Expert Member

  #7
  Apr 9, 2015
  Joined: May 22, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Habari za kulea? Bila shaka mtoto amekuwa mkubwa! Vipi vipele viliisha? Anaendeleaje? Hata mimi katika tafutatafuta, ndo nimekutana na thread yako. Mi ni katoto ka miezi mi 2.5 na kameanza kutoka vipele vinasambaa mwilini. Naomba experience yako.
   
 8. w

  washeby Member

  #8
  Jun 26, 2015
  Joined: May 28, 2015
  Messages: 32
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Habari Wakuu,

  Naomba msaada wa kujua dawa ya vipele vya mchafuko wa damu.

  Mwanangu anajikuna mpaka anatoka vidonda.
   
 9. tomoko

  tomoko Senior Member

  #9
  Jun 26, 2015
  Joined: May 2, 2012
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pole sana kwa motto, nakushauri nenda hospitali ili kujua tatizo ni nini
   
 10. swissme

  swissme JF-Expert Member

  #10
  Jun 26, 2015
  Joined: Aug 15, 2013
  Messages: 12,586
  Likes Received: 15,042
  Trophy Points: 280
  Kweli wewe mzazi unashindwa kwenda kupata vipimo na dawa hospital unakuja kuhuliza nenda sasa hivi hospital mpeleke mtoto akatibiwe ok.


  swissme
   
 11. C

  Chakwale JF-Expert Member

  #11
  Jun 26, 2015
  Joined: May 17, 2015
  Messages: 477
  Likes Received: 344
  Trophy Points: 80
  Huyu atakuwa Ni Mlezi tu si Mzazi
   
 12. L

  LONGIDARE Member

  #12
  Jun 26, 2015
  Joined: May 21, 2015
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo itakuwa scabbies nenda duka la dawa tafuta lotion ya scabbies, halafu tiba nyingine ni usafi fua nguo kila siku na kupiga pasi kila siku abadilishe mashuka
   
 13. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #13
  Jun 26, 2015
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kama ni mtoto wako kweli mpeleke hospitali!
   
 14. x

  xerophyte Member

  #14
  Jun 26, 2015
  Joined: Oct 21, 2014
  Messages: 75
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kanunue BBE lotion kisha jitahidi kumuweka safi huyo mtoto, mavazi na mwili wake.
   
 15. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #15
  Jun 26, 2015
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,788
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Ana allergy huyo,acha kumpa maziwa ya ng'ombe,karanga samaki wa bahari kwa muda uone
   
 16. nameless girl

  nameless girl JF-Expert Member

  #16
  Jun 26, 2015
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 3,905
  Likes Received: 715
  Trophy Points: 280
  Wakitokea watu watano tofauti wanakwambia aina tofauti za dawa utatumia ipi? na vipimo vya kumpa huyo dogo je, utagoogle au utauliza tena?
  Nenda hospitali.
   
 17. kachui

  kachui Member

  #17
  Jun 27, 2015
  Joined: Apr 10, 2015
  Messages: 45
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Pole sana ndg kwn matatizo ktk dunia yanatupata ss na tunayatafutia njia cc wenyewe mm cha kukushauri jaribu kutumia karanga iliyosagwa (tui LA Karanga) Mara mbili kwa siku asubh na jioni unampaka sehemu zote za mapele baada ya kumaliza kuoga hakika atapona mtoto wako ndg .Pole sana
   
 18. K

  Kamau Kingu Member

  #18
  Jun 27, 2015
  Joined: Feb 8, 2015
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  this is too much mkuu!!
   
 19. m

  mkosafedha JF-Expert Member

  #19
  Jun 27, 2015
  Joined: May 19, 2015
  Messages: 1,333
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Dawa ya vipele mpeleke bagamoyo akaoge.
   
Loading...