Mwana Mtoka Pabaya
JF-Expert Member
- Apr 22, 2012
- 15,117
- 16,506
Hatuhitaji dawa tu - ambayo hatuna in the first place-, tunahitaji a paradigm shift in medicine. A sort of escape velocity from the current mire of drug resistance. At this point tukipata dawa in 5 years it is only a matter of time before another strain of HIV will develop resistance, a cat and mouse game.
Acha mimi niishie hapa,
ni upotevu wa muda kuongea na mtu wa aina yako.
I believe
that those in research laboratories has
already put that into consideration.
Kuna tofauti kubwa kati ya watu wanaoshinda maabara kutafuta tiba na kushinda kwenye mitandao kutafuta umaarufu.
Dawa ya ukimwi itapatikana, kama sio leo basi kesho. Microbes na waendelee kuwa 'dynamic' kama ulivyo mdomo wako, lkn kwa kuwa maradhi yoote yalipatiwa tiba kwa mtindo huu, sioni shaka katika hilo.
Siamini kama una lolote unaloweza kuisaidia dunia kuhusu hili zaidi ya kuchat JF na kupaka wanja. Alamsik!
Matibabu ya magonjwa tofauti yaligunduliwa kwa njia tofauti, kwa majibu maalum toa swali maalum.
Lakini koote huko dawa hazikutangazwa kuwa dawa kabla ya majaribio. Majaribio ni kanuni ya msingi kabisa ya sayansi.
Kati ya mimi ninayekataa kukubali kirahisi na hao wanaokubali kirahisi kwamba wamepata dawa ya UKIMWI nani anajifanya anajua sana namna UKIMWI unavyobadilika?
Hao mnaowanukuu wenyewe wanawaambia wanahitaji miaka mitano ya majaribio, nyie watu wa kupewa dawa tu mshaanza kushangilia dawa ya UKIMWI imepatikana? Wakija kuwaambia baada ya mwaka mmoja wa majaribio tulikosea, tulifanya assumptions ambazo katika majaribio zimeonekana si kweli, mtasemaje? Mtaendelea kusema "dawa ya UKIMWI imepatikana"?
It ain't over til it's over. Unashangilia ushindi kabla ya dakika 90?
Wanajua, ndo maana hawajasema dawa ya UKIMWI imepatikana, wamesema wanahitaji miaka mitano kufanya majaribio.
Ukiniona mie mja mtwana dhalili kama nina akili sana ni kwa sababu tu labda wewe ni mwanagenzi zaidi, si kwa sababu mimi nina akili sana /s .
we bwana mkubwa acha kuchanganya watu dawa za kupunguza makali zilipotikana zilitangazwa hivi na mda wa utafiti uliwekwa ili kujua side effect tu
Dawa za kupunguza makali ya UKIMWI au a dawa za UKIMWI?
Hata Cofta inaweza kuwa dawa ya kupunguza makali ya TB lakini si dawa ya TB.
yaani username yako inaendana na majibu unayoyatoa
Don't judge a book by its cover.
Hujajibu masuala muhimu yaliyoletwa.
Kusema dawa ya UKIMWI imepatikana wakati majaribio hayajamalizika ni kiranga kushinda majibu ya kiranga ya Kiranga.
hata sijui unachobisha ni nini mpaka naona uvivu kubishana na wewe labda nikusaidie dawa imepatikana na inaonesha inao uwezo wa kuua kabisa virus totauti na arv ambayo haina uwezo wa kuua virus miaka 5 ni ya utafiti tu wa kujua side effect