Kwame Nkrumah
JF-Expert Member
- Dec 2, 2008
- 886
- 376
Tumelalamika sana kuhusu jinsi chombo hiki cha umma kinavyoendeshwa. Tumeshuhudia jinsi gani mikutano isiyo na maana ya CCM inavyopewa nafasi kubwa kwenye taasisi hii. Takwimu za kupotosha ukweli, uandishi wa habari usio na viwango, kukosa habari zenye kusema ukweli kuhusu serikali na kwa ujumla kutokufanya kazi ambayo wamiliki wa taasisi hiyo [ yaani sisi] tulitegemea kutoka kwayo.
Jei hamna njia za kisheria, kikatiba kumaliza tatizo hili? Tumeshuhudia juzijuzi kamati ya bunge ya miundombinu imekataa bajeti ya wizara ya uchukuzi, je kamati ya mashirika ya umma inayoongozwa na Mh. Zitto inashindwa kuzuia bajeti ya wizara au bajeti ya taasisi hii? Kamati hii inaweza kutumia nguvu iliyonayo [ power of the purse ] kumaliza tatizo hili.
Tumesikia juzi Mh. ktk semina elekezi akiagiza mawaziri kutumia vilivyo vyombo vya habari kueleza mafanikio ya serikali, unafikiri sisi tutapata nafasi kweli?