DAWA YA PENZI

DAWA YA PENZI

mzizimpya

Member
Joined
Feb 11, 2018
Posts
78
Reaction score
22
DAWA YA PENZI
[emoji116][emoji116]soma hadi mwisho
Palitokea Mwanamke, aliyekuwa ametolewa,
akashindwa kuishi vizuri na mumewemumeweZ. Kwa hivyo
mumewe hakuridhika naye akaamua atafute
mwanamke atayemfaa zaidi, aishi naye. Kwa
wivu, yule mke wa kwanza, akatafuta dawa ya
kuweza kumrudisha mume wake. Akatafuta dawa
aina nne. Aina ya kwanza, ilikuwa ya kujipaka
mwilini, aina ya pili, ya kutilia yule mawanaume
kwenye chakula, aina ya tatu, ilikuwa ya
kuoganayo, aina ya nne, ilikuwa ya kuchoma
kwa moto. Hizo dawa aliamini zitamfanya mume
wake, amwache mke wa pili, na kwamba
mapenzi yao yataongezeka, kwa hivyo wataishi
pamoja tena. Baada ya kuzipata dawa hizo na
kuzitumia kikamilifu, bado hali ikawa ile ile,
hakuna lililobadilika. Mumewe akaendelea
kuishi na mkewe wa pili. Yule mke wa kwanza,
akaenda kwa bibi kizeemmoja ambaye alisifiwa
kuwa mganga hodari akamwomba amsaidie. Bibi
kizee hakusita akamwambia akatafute ubongo
wa Fisi, yaani akamuue Fisi ampasue na kuuleta
ubongo ukiwa bado mzima! Ubongo huo, ndio
utatumika kutengenezea dawa ya mapenzi.
Mwanamke akarudi nyumbani akaanza kufikiria
jinsi atakavyomtega Fisi na kumuua. Akapata
wazo la kununua nyama na kuikata vipande,
kuviweka njiani ambapo fisi hupendelea kupita
mara kwa mara. Kesho yake akakuta ule mtego
mtupu, na nyama imeliwa. Akanunua nyama kwa
wingi akaiweka toka pale alipotega jana yake
njiani pote mpaka nyumbani kwake. Fisi
walipofika, kwa uroho na ujinga wao kana
tunavyowafahamu, wakaanza kula vile vipande
vya nyama mpaka ndani ya nyumba ya yule
mwanamke. Akamkuta yule mwanamama
amejitayarisha vizuri na shoka. Kwa nguvu zake
zote. Akampiga kipigo kimoja tu na yule Fisi
akafa hapo hapo. Akampasua kicwani akatoa
ubongo, na akaenda nao kwa bibi kizee mganga.
Alipofika, bibi kizee akauliza: “Mwanangu,
umeniletea ile dawa niliyokutumia?”
Mwanamama akajibu. “Ndiyo mama, lakini
nimeipata kwa shida sana!” Akamkabidhi bibi
kizee ule ubongo wa Fisi. Alipokwisha upokea
akakaa kitako akafikiri sana. Halafu akasema:
“Mwanangu, sasa nitakueleza kila kitu vizuri
sana umetumie akili na ujuzi mwingi, kutega Fisi
na kumwua. Sasa nenda ukatumie akili na ujuzi
wako wote ulionao, ili uweze kupata mapenzi ya
mumeo, ili uweze kupata mapenzi ya mumeo
tena. Nina maanisha kusema, lazima uwe msafi,
uvae vizuri na upikie chakula kizuri mume wako.
Vile vile, jaribu kujipendezesha kwa mume wako
kwa kila hali. Utaona mumeo anarudi nyumbani
na kumuacha mke aliyekuwa naye sasa hivi, na
mataishi kwa amani na furaha. Aliporudi
nyumbani, akafanya, yote aliyoambiwa na yule
bibi kizee. Haukupita muda, mumewe
akamfukuza mke wa pili na akarudi nyumbani
kwa mke wake wa kwanza. Wakaishi vyema kwa
miaka mingi sana mpaka vifo vikawatengenisha.
FUNDISHO:- Inaaminika kuwa, watu
wanapoishindwa kuishi pamoja katika ndoa,
hutumia dawa za kienyeji kwa sababu ya
kusitawisha maisha yao. Wapo akina mama
wengi amabao wanaamini kabisa kwamba kuna
dawa ya mapenzi. Lakini ukweli ni kwamba,
dawa ya mapenzi ni moja tu nayo ni:
Kuhakikisha kwamba, kina tafadhali naomba
share story ili wasio jua WAJIFUNZE # like _ page yetu ya facebook ili kuendelea kujifumza ukitaka ku like page tafadhali gusa maneno ya blue hapa chini Kisha chagua facebook like ili uendelee kupata story nzuri zenye mafunzo #share_kwenye magroup mengine tafadhali [emoji117][emoji117][emoji117][emoji117]
 
Siku nyingine unapo copy na kupaste uwe una edit ikae vizuri.
 
Back
Top Bottom