Dawa ya muungano hii hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dawa ya muungano hii hapa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by oba, May 1, 2011.

 1. oba

  oba JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nimekuwa nikifuatilia mijadala mbalimbali juu ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuwa Tanzania na kugundua kuwa japo muungano ni mzuri na wa kudumishwa kwa nguvu zote una mapungufu. Mapungufu hayo yamezua hoja nyingi na kupelekea wengine kupendekeza muungano uvunjwe. Mapungufu hayo ni pamoja na lile la kuwa na serikari ya zanzibar na ile ya muungano bila kuwa na serikali ya Tanganyika, iweje nyumba ijengwe ndani ya nyumba nyingine?iweje kuwe na serikari huru ndani ya serikari nyingine?
  Maoni yangu ni kuwa, muungano ni mzuri na unapaswa kudumishwa; sikubaliani na hoja ya kuuvunja!napendekeza mabadiliko ya muundo wa muungano yatakayovunja serikari ya mapinduzi ya Zanzibar na kuwa na kuwa na serikali moja tu ya jamhuri ya muungano wa Tanzania . Jamhuri igawanywe katika majimbo; pemba liwe jimbo, unguja liwe jimbo na bara igawanywe kwenye majimbo kama itakavyoonekana kuwa bora
  Kila jimbo liwe na utawala wa ndani chini ya gavana na mabunge ya majimbo kwa ajili ya kuendesha serikari za majimbo. Kuwe na central government itakayoongozwa na raisi wa jamhuri, iwe na wizara nne; wizara ya ulinzi, mambo ya nje, fedha na mambo ya ndani. Kuwe na bunge la muungano lenye wajumbe kutoka kila jimbo. HAPO MUUNGANO WETU UTADUMU!
  Hayo yote yanawezekana kama yatajumuishwa kwenye katiba mpya.
  Naomba kuwasilisha! I stand to be corrected.
   
 2. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #2
  May 1, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  Mbona huo ndio mpango wa CDM!
   
 3. s

  salisalum JF-Expert Member

  #3
  May 1, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 379
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  soma maoni niliyoyatoa kwenye thread ya


  Re: Vitambulisho vya Utaifa visitengenezwe kabla suala la Muungano halijapatiwa Ufumbuzi.

  Tanganyika na Zanzibar ziliungana April 26, 1964. Haijalishi ziliunganaje cha muhimu ziliungana ikawa nchi moja full stop. Hatuwezi kila kizazi kingine kikija tunapangua taifa letu. Zanzibar ni sehemu ya Tanzania na Tanganyika ilikufa mwaka 1964 kwa utashi wa raia wa Tanganyika, wakati huo wakiwa karibu million 10 na Wazanzibari laki 3.

  Kile walichofanya Zanzibar katika katiba yao waliyopitisha juzi ni uhaini na uhuni. Na inatakiwa wale waliosababisha wachukuliwe hatua za kisheria. Kumega sehemu ya Jamhuri ya muungano na kumpa mtu mwingine madaraka ya kugawanya mipaka ya sehemu hiyo nje ya yule aliyechaguliwa kidemodrasia kama Raisi mwenye mamlaka, walifanya kosa la uhaini. Kinachotutesa waTanzania ni kukosa uongozi thabiti wa kukemea na kuchukua hatua.

  Down in 50 years most of us won't be there, tutakuwa taifa la namna gani lenye kugawika kila wakati watu wanapotaka kivyao. Tanzania ni nchi moja, wanachofanya wale walidiriki kufanya kule Zanzibar hakivumiliki hata kidogo. Ni upuuzi mkubwa kufikiria Zanzibar kuwa nchi, ni sawa na kusema Mtwara au Lindi au Mwanza iwe nchi.

  Watanzania wengi ni kizazi kilichopatikana ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hatujui Tanganyika, Ni miaka 47 imepita tangu Tanganyika na Zanzibar kama nchi pekee kufariki. Zilikufa, na hazitafufuka kamwe! Nimesema ni udhaifu wa viongozi wetu wa sasa ndio unaotuweka katika utata. Sifa mojawawapo ya kiongozi bora ni mtu mwenye maono (vision), viongozi tuliowapa dhamana ya kulinda nchi yetu hawajui wajibu wao. Jambo la ku-temper na mipaka ya nchi ni jambo serious sana, wale waliofanya hivyo Zanzibar walipaswa kuchukuliwa hatua. Ndiyo maana Rais aliyepita (Mkapa) alionya kile kiitwacho muafaka. Watu wachache wenye roho ya madaraka kule Zanzibar ndio walio influence insertion ya clauses za kuvunja nchi yetu. Halafu viongozi wetu wanacheka, wanasema katiba ya Zanzibar imeimarisha zaidi Muungano, ni jambo la kijinga sana hili! Watu wanafanya usanii kwenye mambo ya msingi.

  Nyerere alikataa ushauri wa Karume wa kudisolve kabisa sovereignty ya nchi hizi na leo inatupa shida. It was possible to disolve Zanzibar and Tanganyika completely in fact Tanganyika ilishapotea kabisa. Kusita sita huku ndio kunawapa wahuni nafasi ya kudhoofisha nchi yetu. Badala ya ku-focus kujenga dola lenye nguvu sasa tunawaza kuvunja nchi, tutatumia muda mwingi kugombana tu.

  Kinachotakiwa sasa hivi ni kukamilisha Muungano ambao Nyerere aliuchelewasha kuwa nchi moja na kuwa na raisi mmoja na taasisi zenye nguvu zitakazosimamia maendeleo ya Tanzania moja. Hii mambo ya kuwa na raisi wawili na makamu watatu kwenye nchi moja eti tu kuridhisha matakwa ya kakundi ka watu na hasa wataka uongozi ni jambo la kukemewa kabisa.

  Tuna mifano mizuri tu ya kuimarisha muungano wetu, kwa mfano kuwa na majimbo yatayopewa madaraka ya ndani ikiongozwa na watu walichaguliwa. Hivyo Zanzibar, Unguja, Kusini (Lindi, Mtwara, Ruvuma), Kati (Dodoma, Singida etc), Pwani (Dar, Moro, Tanga ...), Ziwa au maziwa makuu (-----) na kadhalika yaweza kufaa au hata vinginevyo. Lakini hili la kuwa na raisi wawili ndani ya nchi moja halifai kabisa.

  Kama hili haliwezekani (yaani kuwa nchi moja chini ya rais mmoja) la kuwa na serikari tatu ndiyo haliwezekani kabisa wala Wazanzibari wasiwaelekeze huko wakidhani wabara watafurahi. Selikari tatu ni kizunguzungu kitakachokwamisha maendeleo yetu kwa miaka mingine 50 kama sio 100 ijayo. It will be sad, very sad but probably we will accept to part peacefully - Lakini nchi itaendelea kuitwa Tanzania na siyo Tanaganyika. Hivyo basi vitambulisho viendelee, Kama Wazanzibari wa sasa watang'ang'ana kutoka kwenye muungano basi sehemu itayobaki itaendelea kuitwa Tanzania.

  Tanzania, Tanzania, Nakupenda kwa moyo wote.

  Viongozi bado mna nafasi ya kuikoa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Chukueni hatua sahihi kwa wale wanaoleta fyokofyoko za kuvunja muungano. Kwenye kujenga umoja wa nchi yatakiwa muwe serious sana, Msivumilie watu wa namna hiyo hata kama ni marafiki zenu.

  Rais Kikwete ametamani sana kuleta utengamano kule Zanzibar na kwa na namna fulani kwa muda mfupi ujao Zanzibar itatulia, lakini si sustainable. Raisi wetu ame trade off sana principles za kujenga strong future ya nchi hii kuleta tu amani ya muda mfupi kule Zanzibar. Ni risk kubwa sana hii. Yetu macho na masikio. The most sustainable system ni kuondoa sub autonomy section ya nchi moja. Kama Zanzibar haitakuwa na raisi watogombania nini? Sana sana itakuwa oh wenzetu wa bara wanapata hichi sisi hatupati.....​
   
 4. Bornvilla

  Bornvilla JF-Expert Member

  #4
  May 1, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 925
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Majimbo! Siku moja watakuja watu wa majimbo kutaka kujitenga na hapo kila jimbo litataka kuwa huru nchi itakuwa vipandevipande.Mi wazo la serikali za majimbo siliafiki hata kidogo.Marais kama watatoka majimbo fulani tu kwa muda mrefu huo utakuwa mgogoro tosha wa kuivunja nchi.Mfano Mwal alisema Muhaya na Mchaga hawezi kuwapa kuongoza nchi. Kumbuka mkoa wa Mara na Kigoma iliwahi kuleta madai ya kujitenga.Mpaka hapo huoni itakuwa tatizo? Kabila la wasukuma walitaka lugha ya kisukuma iwe lugha ya taifa hivyo majimbo yataleta Udini na Ukabila! Hayo yote hatuyataki tunataka nchi moja tu! Kwa suala la muungano niliwahi kuliandikia hapa lakini post haionekani basi unaweza fungua blog ya kidau.blogspot.com halafu nadhani utaridhika kua Muungano hata kwa dawa hauvunjiki ila utaboreshwa tu.
   
 5. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #5
  May 1, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Dawa ya muungano ni kuuvunja kisha kujenga ukuta wa kutenganisha Tanganyika na Zanzibar kama ule wa West Bank. Zanzibar ni tatizo
   
 6. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #6
  May 1, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Hayo yanawezekana tu kama tukiikabidhi nchi kwa CHADEMA.watu wasiojiamini na vilaza kama CCM hawawezi kuelewa hicho ni kitu gani.
   
 7. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #7
  May 4, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Mawazo hayo ni ya Kitanganyika na wala msisumbue bongo zenu kwa mawazo potofu kama hayo.

  Hata siku moja Zanzibar haitapoteza utaifa wake kwa tamaa za kikoloni kama hizi.

  Hapa nasema kwa ufupi tu maana nna shughuli kidogo na sikutaka inipite lakini

  Zanzibar for Zanzibaris, Tanganyika mtajua wenyewe mlioiua.

  Wewe jipendekeze tu kwa hao bwana zako, iko siku utajuta.
   
 8. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #8
  May 4, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  kwa kisukuma tunasema la tete vide. una uhakika na hayo uyasemayo? au unatumia maneno ya mtaani kudanganya watu ndugu yangu? duh! fanya utafith kabla hujasema.
   
 9. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #9
  May 4, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  Mikwara mbuzi hiyo mkuu! huyo jamaa hapo juu ni muelewa na amebandika kitu imeenda shule.
   
 10. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #10
  May 4, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kwanza kabisa tunahitaji serikali ya Tanganyika, halafu mambo mengine yatafuata baadaye.
  Faida:
  Tutakuwa na bunge la Tanganyika, litakalohakikisha watanganyika wana uhuru
  Tutakuwa na baraza la mawaziri la Tanganyika, kulinda vitu kama madini yetu
  Zanzibari wao tayari wako fiti
  Si sahihi kuwaita mawaziri wasio wa Muungano, kuwa ni wa jamhuri ya muungano
  Hapo hata katiba itajadilika.:israel:
   
 11. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #11
  May 4, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  haaa ndani ya ccm na wewe ni gamba mkuu!
   
 12. ATUGLORY

  ATUGLORY Senior Member

  #12
  May 4, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hapo umenena hmethod. na kwenye Ukuta huo tutegeshee mabomu ili wazanzibari wasipate nafasi ya kuja Tanganyika tena, lakini kwanza tuondoe wazanzibari waliolowea Tanganyika!!!!!!!
   
 13. N

  Nonda JF-Expert Member

  #13
  May 4, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mwenye Muungano, Mwalimu Nyerere anasema hivi;

  "Kwa kweli hata kesho Nchi za Afrika ya Mashariki zikiamua kuungana, na Tanzania ikawa ni mshiriki, naamini kuwa ni rahisi zaidi kushirikisha Tanzania yenye Serikali Mbili - ya Zanzibar na ya Tanganyika - kuliko Tanzania yenye Serikali Mbili, ya Tanzania na ya Zanzibar. Wapendao Utanganyika watakuwa wazalendo zaidi, badala ya kuwa wasaliti, wakiazimia Afrika ya Mashariki iliyoungana kuwa Nchi Moja. kuliko Tanzania iliyotengana ikawa nchi mbili."


  Ukurasa 11. Uongozi Wetu Na Hatma Ya Tanzania (by Nyerere)


  EAC ipo? Jee EA Federation inakuja? Wamesema fast track, au?


  Dawa hiyo hapo juu, Hivi mwalimu Nyerere"imeenda shele"?
   
 14. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #14
  May 4, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hili ndio jawabu lako kwa leo:

  maridhiano-znz.jpg
   
 15. oba

  oba JF-Expert Member

  #15
  May 4, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hakuna uhuru usiokuwa na mipaka, tunaposema majimbo hatuna maana kuwa yatakuwa na sehemu huru ndani ya jamhuri, ndiyo maana wazo la msingi linapendekeza serikari kuu ndiyo itakayokuwa na mamlaka ya majshi yote na ndiyo itakayotoa sra mama kwa maendeleo ya jamhuri kwa ujumla wake. Kwani kilichozuia kigoma isifanikiwe kujitenga ni kwa kuwa ni mkoa katika muungano wa tanzania? La hasha, ni kwasababu kigoma haina jeshi la pekee yake kiasi cha kuanzisha uasi juu ya serikari kuu ya jamhuri. That is my comment!
   
 16. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #16
  May 4, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Gaweni Tanganyika yenu majimbo, sisi inatosha kama tulivyo. Na wacheni kuzuia mabadiliko kama mlivyozoea kufanya kwa kuikalia Zanzibar kwa nguvu za dola. Ufupi, tumewachokaaaaaaaaaaaaa.


  View attachment 29274  haya tena basi jamani.jpg
   
 17. oba

  oba JF-Expert Member

  #17
  May 4, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Miongoni mwa vitu vinavyonikera katika muundo wa serikari ya jamhuri ya muungano wa Tz ni kama vifuatavyo;
  1.Serikali kama muhimili kati ya mihimili mitatu kuongozwa na mawaziri ambao ni wabunge wanaounda muhimili wa pili wa bunge.
  2. Bunge kama muhimili wa pili kujazwa na wabunge wa kuteuliwa ambao hata hawana kazi yoyote zaidi ya kupora jasho la watanzania kwa njia ya posho.
  3. Serikali kupitia kwa raisi kuwa na uwezo wa kudetermine key figures za kuunda muhimili wa mahakama kwa kuwateua jaji mkuu, majaji na watendaji wakuu bila kupitishwa na bunge au kuhojiwa na mtu yeyote.
  Serikali ambayo mawaziri wake watakuaw siyo wabunge ili kuondoa mgongano wa maslahi, ile itakayofuta nafasi ya wabunge wa kuteuliwa na itakayo kuwa haiathiri utendaji wa mahakama kwa kuingilia muundo wake hiyo nitaifurahia na kuiunga mkono.
  Mawazo yangu tu, I stand to be corrected!
   
 18. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #18
  May 4, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hoja zako nzuri lakini hapa sio pahala pake. Iko thread ya Katiba ya JMT humu jamvini, peleka huko tafadhali.

  Hapa ni "muungano" usio dawa ila kuvunjika tu. Ikiwa kwa miaka 47 haukupata dawa, ni kufa tu.

  Zanzibar for Zanzibaris, majimbo bara huko.
   
Loading...