Dawa ya meno au dawa ya mswaki?

Dawa ya meno au dawa ya mswaki?

mchungupwani

Member
Joined
Jun 2, 2015
Posts
13
Reaction score
2
Kipi kiswahili sahihi kati ya kusema dawa ya meno au dawa ya mswaki?

Kama ni dawa ya mswaki kwani mswaki unaumwa nini ? Kama ni dawa ya meno kwa nini ukienda hospitali ukiwa unaumwa meno hupewi colgeti.

Karibuni wadau!
 
iitwe Kinga ya meno, si dawa ya mswaki,
Ina Kinga meno yasishambuliwe na vijidudu.

Au dawa ya kukinga meno yasishambuliwe na vijidudu.
 
Ingawa kiswahili hakijitoshelezi katika hili, ili kuleta maana sahihi zaidi ni kusema "Dawa ya meno" yaani Dawa ya kusafishia meno! Bahati mbaya si kila ""Dawa" inatibu! Kama zilivyo dawa ya 'kusafishia kidonda' ndivyo ilivyo, si "dawa" ya kutibu.
 
Kiatilifu kazi yake ni kuzuia na ukisema dawa, kazi ya dawa ni kutibu ugonjwa.
 
Ingawa kiswahili hakijitoshelezi katika hili, ili kuleta maana sahihi zaidi ni kusema "Dawa ya meno" yaani Dawa ya kusafishia meno! Bahati mbaya si kila ""Dawa" inatibu! Kama zilivyo dawa ya 'kusafishia kidonda' ndivyo ilivyo, si "dawa" ya kutibu.

eti Kiswahili hakijitoshekezi. watanzania na fikra mgando. ama kweli uko westernized zaidi. but Kiswahili kinajitosheleza
 
Sio sahihi kuiita 'dawa ya mswaki' kwa vile haitibu mswaki.

Kwanza mswaki sio kiumbe hai kwa hiyo hauugui, utautibuje. Pia sio sahihi kuiita dawa ya meno kwa vile haitibu meno.

Infact the so called tooth pastes ambazo wengi tunatumia ni hatari sana kwa meni yetu>wajinga ndio waliwao.
 
hahaha uzi unabowa lkn wacha nichungulie kidogo na mm kama ukienda hosptal hupewi colgate sasa kwann unapoumwa unapoenda dukani kununua dawa flan ina maandishi maumivu ya kizidi muone dakta sasa hapa nan bora daktar au dawa husika
 
eti Kiswahili hakijitoshekezi. watanzania na fikra mgando. ama kweli uko westernized zaidi. but Kiswahili kinajitosheleza

Sifa mojawapo ya kila lugha duniani ni kukua na kujiongeza kimisamiati.. Ni ukweli usiopingika kwamba kisw chetu kina limitations nyingi sana hasa inapokuja kwenye matumizi yalio globally zaidi!

Hizo dawa na miswaki vimeibuka recently, miaka hyo before colonial era tulikuwa tunatumia miti kusafisha meno.. So product or item or goods mpya zinapoingia wataalamu hutafuta namna ya kufny translation n most of translated words yana ukakasi as that one mentioned above..

Kama unabisha utakuwa na matatizo binafsi!
 
Mkuu, lugha ni sauti za nasibu... Maana yake ni kuwa hakuna uhusiano kati ya sauti tunazotumia na tunachomaanisha.. Hata neno 'dawa' halina uhusiano wa kiufundi na kitu kinachotibu, ndio maana neno hilo hilo linaweza kuwa halina maana kwenye lugha nyingine.

Lugha zote duniani zina viroja kama hivyo, mathalani kwenye Kihispania kuna nomino za kike na nomino za kiume, kwenye Kiingereza kuna maneno kama 'guinea-pig', huyu si nguruwe na hana asili ya Ginee, lakini aitwa hivyo.
 
Back
Top Bottom