google helper
JF-Expert Member
- Jun 11, 2013
- 9,667
- 13,877
wajinga ndio waliwao, nalo ni la kutafuta mganga ? kweli
Masharti ya mganga ndivyo yanavyosema lakini
Masharti ya mganga ndivyo yanavyosema lakini
Habari za wakati huu wana MMU.Leo nimeamua kuwashirikisha kisa kilichomtokea rafki yangu wik end iliyopita.
Ni hivi,jamaa kuna demu alikuwa anamfukuzia kwa takriban nusu mwaka sasa lakini demu anamchomolea.Basi siku moja tukiwa tumekaa maskani jamaa alijiapiza kuwa safar hii lazima ampate kwa njia yoyote ile hata kwa mganga ataenda.Baada ya kusema hivyo kama zali akapita Mmasai kashika mizizi flani hivi anauza,jamaa akamuulzia masai kama anayo dawa ya mapenzi, masai akasema anayo na akamuonesha.
Kuna mzizi mmoja ukiushika demu yeyote ukimsimamisha anasimama hata kama anaharaka na kweli jamaa alijarbu kwa dada mmoja hivi ambaye ananata sana hapo mtaani cha ajabu huyo dada alisimama na akakubali appointment na jamaa.Basi baada ya kuona dawa zinapiga kazi jamaa akanunua miziz aliyokuwa anataka kisha akagewa masharti yake.Masharti ilikuwa ni kwamba wakati anaongea na huyo demu anaemtaka(akiwa anamtongoza) aweke mzizi mdomoni na kuanza kuutafuna,alaf pindi demu anamjibu jamaa anatakiwa ile mizizi aliyoitafuna awe anamtemea demu usoni kidogo kidogo ila kwa haraka mpaka iishe mdomoni ( na demu ndio atatiki)
Basi jamaa last wiki akaenda hadi mtaani kwa yule demu aliyemfukuzia muda mrefu,kufika pale akautupia mzizi mdomoni kisha akaanza kutema madini yake.Jamaa anasema isingekuwa mapenzi aliyonayo kwayule demu angeutema maana ni mchungu kuliko mwarubaini.Ilifika kipindi akawa anakunja sura hadi demu akamuulza kama anaumwa.
Jamaa akajikaza kiume hadi akamalza mistari yake.Sasa utata ulikuja wakat demu anatoa majibu,jamaa kila akitaka kujarbu kumtemea usoni ile mizizi anasita maana ilikuwa giza halijaingia (mida ya saa 5:30 jioni) alaf demu alikuwa anamwangalia msela usoni.Jamaa akajikaza kisabuni akamtemea mara ya kwanza usoni,yule demu akastuka kwanza alaf ikawa kama amekasirika,jamaa ikabidi azuge kidogo.Demu alivyoendelea kuongea tena jamaa akamtemea tena demu usoni,unaambiwa yule demu lilimtoka kofi ilo na tusi moja la nguoni alaf akasepa
Ndege akawa amepeperuka,alaf yule jamaa nae alimeza baadhi ya mate na mzizi kutokana na lile kofi.Jamaa alirudi home kwao yuko hoi kalegea akanywa lita kadhaa za maziwa ndio hali ikarudi sawa ule mzizi aliogewa cjui ni sumu au vipi.
Alivyonisimulia kisa chake nilitaman kucheka ila nilichuna kwasababu hali yake ilikuwa bado haijawa vzr.Ila nimejifunza kitu kimoja kuwa dawa ya mapenzi ni pesa hawa waganga watatuua na mizizi yao
ha ha ha ha ha uuuuupsi