Dawa ya malaria

Kasuku Mdogo

Member
Jun 2, 2016
14
23
1.Juisi ya aloe vera (mshubiri)
Juisi ya Aloe Vera huongeza kinga ya mwili. Mu-aloe-vera una viinilishe vingi sana muhimu kwa afya ya binadamu. Una vitamini A, B, C na E. Mmea huu una orodha ndefu ya madini muhimu kwa mwili na vimeng’enya vingine muhimu.
Tengeneza juisi freshi nyumbani na uchanganye nusu glasi juisi hii ya aloe vera nusu nyingine kwenye glasi jazia na juisi yoyote ya matunda uliyotengeneza mwenyewe nyumbani na unywe alasi moja kutwa mara 2 kwa siku 7 hadi 14.

2.Unga wa Habbat soda
Habbat soda yenyewe ni dawa kwa kila ugonjwa isipokuwa kifo. Inafahamika kutibu magonjwa mengi zaidi ya miaka 3300 iliyopita. Chota kijiko kikuba kimoja cha uga wa habbat soda na uchemshe kama chai na maji nusu lita, ikichemka ipua na chuja kama chai.Kunywa kikombe kimoja kutwa mara 2 kwa siku 7 mpaka 14 malaria yako lazima iwe imepotea.

Mambo muhimu kwa mtu yeyote anayeumwa na malaria kila mara

Kunywa maji mengi kila siku mpaka glasi 10

Kama ni mlevi na unakaa bar mpaka usiku wa manane jaribu kubadili staili, ama ununuwe ukanywe nyumbani au upunguze kakaa muda mrefu kwenye bar au uache kabisa pombe. Kukaa masaa mengi bar kunakufanya kuwa karibu na mbu na pia kunywa pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako.

Jishughulishe na mazoezi ya viungo mara kwa mara.
 
Hapo kwenye huo mlolongo wa tiba asilia fanya kuhongezea na hizi...
1.Majani ya mwarobaini yachemshwe kisha yatumike maji yake n yakilala tu kesho yakupasa uchemshe mengine
2.Majani ya mbono na hata maji yanayopatikana kwenye magomr yake ni dawa.
3.Majani ya mihogo pamoja na tende vyote kwa pamoja vichemshewe.
4.juice ya lemon ndio baba wa dawa zote za malaria
 
Back
Top Bottom