Fyengeresya
JF-Expert Member
- Oct 10, 2011
- 751
- 349
Hatimaye chama tawala,CCM,kimepata dawa ya kumdhibiti mgombea wa Urais kupitia CHADEMA/UKAWA,Ndugu Edward Ngoyai Lowassa. Dawa husika inatengenezwa na wapambanaji wa ufisadi hapa nchini ambao wameapa kumuanika Lowassa ili watanzania wamjue. Tayari mikakati ya mtu-kati imesukwa.
Katika timu hiyo, itakayoshiriki bega kwa bega katika kampeni za kumnadi Magufuli,wanatajwa Sitta, Mwakyembe,Ole Sendeka,Mwigulu Nchemba,Lusinde aka Kibajaji na Nape Nnauye. Pia wapo wanaKitengo.
Upepo wa Lowassa umeonekana kuvuma kwa kasi ukisomba na kupeperusha watu na vitu. Tishio linakaribia mwisho zitakapoanza kampeni. CCM iko vizuri,itamdhibiti hadi awe mahututi kisiasa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
ukweli wa ccm leo utakuwa uwongo wenye kunuka mbele ya wa TANZANIA !!
LOWASSA NI MTU MTAKATIFU NDANI YA NAFSI ZA WATANZANIA 80% WATAKACHO ONGEA CCM MDA HUU NI SAWA NA MFA MAJI HAACHI KUTAPATAPA!!
Usimsahau kiungo mkongwe maalim Seif kati kati. Hii timu ya UKAWA sijui utaiambia nini.pande hiyo akina nape mropokaji na nchemba na sitta pande hii watu mahiri akina tundu antipasi, john john professa safari jussa ismail kwa hiyo ninyi semeni uongo na uzushi sisi tunakuja kupangua uongo wenu na uzushi wenu kwa hoja na data zilizokamilika. ifikapo oktoba 25 mtajua kama yenu ni dawa au pipi
Wewe unaye sema Lowassa ni Fisadi ndio utueleze huo ukweli wa mungu wako...! Mnafiki wewe usitaje jina la mungu bure..!!kusema uongo ni dhambi ha km ni mzaha.... imani ya dini yangu huniambia... kwa kauli hiyo kwa ushahidi wa MUNGU aliyejuu kuwa lowasa si fisadi????
Na wewe ututafutie majibu ya maswali haya:-Lakini watafute na majibu ya swali la
1. " Kwa nini iwe sasa??!!"
2. "Je asingehama!!??"
Watuwekee wazi kwanza waliochikua zile bilions za Escrow za stanbic ambapo kumekuwa na kigugumizi mpaka leo!
Pili wamsaidie magufuli kuelezea matumizi halali ya zile 252b ambazo alidanganya bunge na ukaguzi wa CAG wa january mwaka huu umegundua kuwa matumizi ya kiasi kikubwa cha hiyo hela hayaeleweki.
Tatuwatuelezee vizuri tuhuma za mgombea wao kuuzia nyumba ndugu zake waliokuwa wanafanya kazi tempo wizarani kwake! Na jewatarejeshanyumba za serikali ambazo walijiuzia kwa bei waliojipangia wenyewe! Na wawaeleze watanzania hasara iliyopatikana mpka sasa ya mawaziri kuishi hotelini kwa miaka mingi kisa hamna nyumba! Nasikia kuna waziri amekaa hoteli mpka bill ikafika 100m !
Kimsingi ccm wametosha acha wajaribu na wengine tuone jamani!
Na wewe ututafutie majibu ya maswali haya:-
1. Kwa nini walimkata asigombee?
2. Kwa nini alisubiri akatwe ndio haondoke?
3. Kwa nini ukawa walikuwa wanasema kwa nguvu zote wana ushahidi wa yeye kuhusika na ufisadi lakini sasa wanaubishia?
4. Kwa nini wazee kama Slaa na Lipumba wanakaa pembeni?