Dawa ya CCM ni kulinda kura!!

samirnasri

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,388
213
Nimeamini ccm wamekua na tabia ya kuchakachua matokeo pale wanapoachiwa mwanya wa kufanya hivyo lakini wakikabwa koo kama walivyofanya vijana wa arumeru kwenye uchaguzi wa juzi, au walivyofanya vijana wa mwanza, mbeya, Arusha, dar n.k kwenye uchaguzi wa mwaka juzi ccm hawachomoki.

Wana arumeru walikaba hadi penati na kivuli kiasi kwamba mmbinu za ccm za kuchakachua zikakwama. Mtu alikuwa akikatiza na mfuko wowote anakaguliwa kuona kunanini, gari lolote lilikuwa likipita lilikaguliwa, hata mtu akiende na hotpot vijana walikagua kuhakikisha kama kweli kuna chakula ndani kada wa ccm akienda mahali alifuatiliwa kwa nyuma kujua kulikoni e.g. mchemba aliyeingia kanisani kusali eti mchungaji akamuomba atoe neno, sijui alikuwa anatoa neno kama nani wakati yeye sio kiongozi wa arumeru na wala sio kiongozi wa kitaifa aliudhuria misa kama muumini mwingine yeyoye. Mimi niliwahi kusali ibada tofauti na mkapa na jaji werema lakin baada ya misa wakasepa. Hizo zilikuwa ni njama za kutaka kupiga kampeni siku ya uchaguzi. Vjana wa CDM walikua wakifuatilia nyendo zake.

Nimefurahishwa sana na spirit ya wana meru wame play role kubwa sana katika ushindi wa chadema. Hongereni sana. Ndio maana nasema CCM wakikabwa hadi kivuli hawachomoki. Hivyo CDM wanapaswa kuimarisha kikundi chao cha ulinzi na usalama wa chama ili 2015 vijana waendelee kuwakaba hadi kivuli. CCM wanabeza nguvu ya umma lakini ni nguzo muhimu sana katika mafanikio ya CDM.
 
Emanueli Nchimbi na Makongoro Mahanga hawa wanajua kukimbia na masanduku ya kura,mchana kweupe,tuwe makini nao 2015.!
 
0digg

arumeru-nassari.jpg
 
Pia tusisahau kuwahimiza vijana wote wenye sifa kijiandikisha kwenye daftari la wapiga kura na wakati ikufika wakapige kura ,mpaka hapo ccm itakuwa historia, amen
 
Kamanda Lema alikuwa anaongoza kikosi cha ardhini katika kulinda kura na kamanda Mbowe alikuwa anaongoza kikosi cha anga katika kulinda kura Arumeru.
 
wakuu ni kweli unaweza kulinda kura, ila wanaweza kucheza na daftar la wapiga kura kama hili la vijibwen,
 
chadema wamepata lesson nzuri sana arumeru'kumbe ccm ni wezi na Mungu aliamua kuwaumbua hawa waabudu shetani'chadema wakae chini waangalie jinsi ya kuunda kikundi maalum cha wapambanaji'wapenda mabadiliko'wazalendo wenye uchungu na nchi yetu''naomba sana na mimi niwemo kwa sababu nina hasira ya kuona ccm ikizikwa'mikoa ya kusini itatuchelewesha lakini bado tuna muda wa kutosha kujiandaa'kila mkoa wakipatikana wapambanaji 1000 ccm itatupwa mbali na kuzikwa rasmi
 
Tunapaswa kujipanga kuanzia sasa kuwa na vikosi kila mkoa vyenye kupambanua mbinu zote za magamba na kudhibiti kura
 
Tarehe 16 , makamanda wooote hakuna kulala, ni kulinda kura mpaka dakika za mwisho.hiyo ndio siri ya ushindi!
 
Back
Top Bottom