Dawa ya allergies

Dawa ya allergies

pilato93

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2014
Posts
6,967
Reaction score
7,659
Wakuu Habari ya jioni,

Natumai mko vyema, nilikuwa nahitaji. Msaada wa dawa ya allergies mpaka sasa nimeshatumia dawa hizi Centrizine na predesoline lakini bado sijafanikiwa kutibu tatizo, ambalo nimeambia ni allergies kwani nina vipere vinaniwasha sana vidogo vidigi na vingine ni kama vinamaji

Nashukuru
 
Pole sana mkuu ,ebu tumia vitunguu swaum uviloweke kidogo baada ya mda unakunywa,alafu hivyo vipere kama viko sahem moja unaweza saga kiazi mbatata lile rojo lake unapakaa hapo
 
Wakuu Habari ya jioni,
Natumai mko vyema, nilikuwa nahitaji. Msaada wa dawa ya allergies mpaka sasa nimeshatumia dawa hizi Centrizine na predesoline lakini bado sijafanikiwa kutibu tatizo, ambalo nimeambia ni allergies kwani nina vipere vinaniwasha sana vidogo vidigi na vingine ni kama vinamaji
Nashukuru
Kama Prednisolone na Cetirizine hazijafua dafu, ni vyema kurudi nyuma na kutafuta chanzo cha allergy yenyewe.

Mfano:
1: kuna kitu kipya unatumia, chakula, mafuta ya kupaka vs kupikia, sabuni, nguo
2: Kuna mtu mwingine kwenye familia/kama ipo ana tatizo kama lako?
3: Vipele viko sehemu gani hasa ya mwili?
4: Kuna mtu alikuja kukutembelea au ulienda sehemu kwa kipindi ambacho muwasho ulianza?
5: Muwasho ni mkali zaidi wakati gani usiku vs mchana?

NB: Hii inaepusha kumwaga maji kuzima moto huku ukiacha petroli inaendelea kumiminika kwenye moto huohuo. Tuanze kuzuia kisababishi.
 
Vipere ni mikononi na kwenye mapaja maeneo pachu havina muda maalum kuwasha
 
Attachments

  • DSC_0017.JPG
    DSC_0017.JPG
    209.6 KB · Views: 41
Back
Top Bottom