Dawa hii hapa!!

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
21,885
Reaction score
29,675
Habari zenu wanaMMU,.

Kumekuwa na vilio vingi sana hapa jamvini hususan katika suala zima la uzazi, wanaume kwa wanawake wameingia katika ndoa huku wakiwa hawana uhakika katika suala la kuzalisha nikimaanisha mmoja wa wazazi kama siyo wote katika ndoa kutokuwa na uwezo wa kuzalisha au nguvu za kiume ama za kike kutokuwa na uwezo wa kutunga mimba,.

Sasa mnaonaje watu wakajihakikishia mapema kama wanao uwezo wa kuzaa kabla ya kuingia katika ndoa na kutambulika katika jamii kama mume na mke ili kuepuka mifarakano isiyokuwa ya msingi katika ndoa!!

Tushauriane wadau,.
 
Dini imekataza kuzaa nje ya ndoa.
Unataka kuhalalisha zinaa?
 
Dini imekataza kuzaa nje ya ndoa.
Unataka kuhalalisha zinaa?

siyo zinaa, vilio vimezidi na kama wote watakuwa fiti si watajenga familia jamani!!
 
watajihakikishia kwa njia gani mkuu. funguka basi.
 
Uwezo wa kuzalisha haujawa tatizo kubwa hivyo tuwe wakweli, unamaanisha wasio na uwezo wa kuzaa wasiingie kwenye ndoa ?
 
Huo ndo mpango mzima. Kuuziwa mbuzi kwenye gunia hapana. Mnaenda honeymoon mtoto anaachiwa beki3 au bibi.
 
Iman yko ipo wap???wangapi wamezaa ndan nje ya ndoa na mtoto akafa na baada yakuolewa asizae tena???Mungu hajaribiwi!!!!
 
Kwa mujibu wa vitabu vitakatifu hiyo tunaiita zinaa, lakini kwa mawazo ya kawaida watoto wengi ni watoto haramu so sioni kama ni vibaya ukiwa na mtoto kisha ukaoa. Mbaya ni kukataa kutunza na kuoa, sio mbaya

Sent from my BlackBerry 8900 using JamiiForums
 
I dont understand why people consider marrige as some kind of contract agreement!Kuzaa majaaliwa bana!!!

raha ya ndoa iko wapi kama siyo kuwa na watoto??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…