Da'Vinci meres about the future: Je, yajaayo yanafurahisha?

Da'Vinci meres about the future: Je, yajaayo yanafurahisha?

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2016
Posts
36,443
Reaction score
110,233
SALUTE COMRADES...
images (4).jpeg

Kama mnavyofahamu kichwa cha mwanadamu aliye hai na timamu wa akili lazima mahali alipo lazima kichwa kiwe kinawaza , nimekaa nikawa nafikiri mambo flani kichwani nikaona ngoja niwashirikishe na nyie ma GT ili nione kama fikra zangu zina make sense. Haya hapa ndio niliyokua nafikiria kichwani.
• Population kati ya Christians & Muislims
Nimekaa nikawaza nikaona miaka 100 au 200 ijayo inawezekana idadi ya wakristo itakua ndogo zaidi kuliko Islams, kwanini nasema hivo? Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2015 wakristo tupo 2.3 Billion dunia nzima na Waislam 1.8 Billions. Sasa ipo hivi, ndoa za kikristo haziruhusu kuoa mke zaidi ya mmoja na hasa kwa sisi wakatoriki kwenye semina tunaambiwa unapofikiria kuzaa hakikisha unamwandalia mtoto huyo mazingira mazuri from pre-natal stage to post-natal stage kasha hadi akifika wakati wa kujitegemea yeye mwenyewe. Hivyo kutokana na hilo mtu anazaa watoto kidogo ili kuwatengenezea maisha bora watoto hoa kama kielimu, chakula,mavazi + malazi. Wakati sisi tunafanya hivyo huku ndugu zetu waislamu wanaoa zaidi ya mke mmoja na wengine wanaoa hadi wake wanne, wanazaa watoto wengi bado hujahesabu watoto wa michepuko (pia wakristo wanamichepuko yenye watoto) pia ndoa za kikristo zimekua complicated sana, I mean ghalama za ndoa ya kikristo zipo juu sana kulinganisha na za wenzetu waislamu hivyo kupelekea vijana wengi wa kikristo kuokopa kufunga ndoa. Kwa mantiki hiyo nafikiri kwamba baada ya miaka 100 ijayo idadi ya wakristo duniani inaweza kupungua na kua chini zaidi.
FT_17.04.05_projectionsUpdate_globalPop640px.png


• Kupungua kwa idadi ya watu wanaoamini katika Mungu
Miaka 500 iliyopita binadamu ndio waligundua kua hii dunia ni duara na yenyewe ndio inzunguka badala ya jua, zaidi ya miaka 3950 iliypita binadamu alikua anajua chanzo cha wanadamu alikua mwanamke mmoja na mwanaume,zaidi ya miaka 30 iliyopita binaadamu akatoa nadharia yake kua dunia ilikua haikaliwi na mtu hapo mwanzo mpaka pale ulipotokea mlipuko mkubwa (the Big bang) huko angani (space).
>>>
images (3).jpeg

Ninachoona kutokana na kuendelea na kuhama kwa teknolojia na sayansi (Transformation and development of science & technology) kutapelekea idadi kubwa ya watu kutoamini uwepo wa Mungu na kuamini zaidi sayansi hasa miaka ijayo ambapo teknolojia itakua imekua kwa hali ya juu. Kwa mfano kama umefuatilia gunduzi za mwanasayansi Elon Musk kuhusu kubadili dunia kua ya kijanja (smart world) kwa kutumia project zake mbalimbali kama 4D printing,Project zake kwenda kuishi sayari ya Mars, Hyperloop transportation nk nk au Teknolojia ya kurudisha uhai kwa kutumia barafu/baridi Pia kutokana na mambo mbalimbali yaliyotabiriwa ambayo kwa sasa yanatokea kuhusu Anti-Christ administration.
TIP. Mwaka 1958 kunamwandishi aliandika kitabu kuhusu safari za mwandamu kwenye sayari zingine akaandika kua binaadamu atakayefanikisha wanadam kutawala sayari ya Mars anaitwa MUSK
images (2).jpeg
images (1).jpeg
images.jpeg


• Kuungana kwa makanisa ya Kiprotestant na kanisa Katoliki
Sasa imetimia miaka 500 toka Fr. Martin Luther kutengwa na kanisa katoliki na kuanzisha makanisa ya kilutheri, japo makanisa hayo yamekua yakilisema vibaya kanisa katoliki lakini miaka hii makanisa mengi ya kiprotestant yamekua yakiiga mambo mbalimbali yanayofanywa na wakatoliki tena mambo mengine yalikua wanayasema vibaya lakini nao wanayafanya mfano, melody za uimbaji na tone za usalishaji (slow mode) kuweka misalaba kanisani, jumuia ndogondogo, kucheza kanisani, na mengine mengiii. Hivyo basi japo walilisema kanisa katoliki vibaya lakini wanafanya mambo yanayofanywa na wakatoliki hivyo naona tu ipo siku wataimba ule wimbo wa Lucky Dube unaoitwa Back to my root, Yes they will be back to their roots... Hata mwana mpotevu alisamehewa.

Hayo ni mawazo yang tu naweza kua nisiwe sahihi kwa hilo lakini ndio maaana nimeyaleta kwenu GTs nanyi mjadili.

Maoni ya Mwandishi
Naomba niwashauri ndugu zangu waislamu kua jitahidini muikamatie elimu vizuri maana kwenu suala la elimu dunia nyie naona mmelipa kisogo wakati hata Mungu mwenyewe kasisitiza kuishika elimu ipasavyo, elimu ndio msingi wa kila kitu katika dunia hii ndio maana wenzenu wakristo dini na elimu vinaenda sambamba kama mtaendelea kuitelekeza elimu mwisho wa siku kama nilivyosema hapo juu wakristo watakua wachache lakini wenye elimu ya dini na elimu dunia wakati waislamu watakua wengi duniani halafu wasio na elimu, hivyo tu panga pangua mtaendelea kutawaliwa na wakristo wachache wenye elimu.
Biblia inasemaje? Mathayo 28:20 “……Na tazama nipo pamoja nanyi sikuzote, hata ukamilifu wa dahari” Ufunuo 15:17 “…….nami nitawachunga kwa fimbo ya chuma” Katika vifungu hivo Mungu anawatia moyo na kuwaahidi watu wake kua kama Kuku anavyolinda vifaranga vyake visichukuliwe na mwewe au mchungaji anavyolinda mifugo yake isiraruliwe na mbwa mwitu /wanyama wakali basi ndivyo BWANA MUNGU anavyolilina na atalilinda kanisa lake (waliomwamini na kushikamana nae) lisipotee. Hivyo basi hata ukipata vikwazo kiimani vyovyote usitetereke yupo Yesu anayekupigania.
Mwisho kabisa niwaombe radhi wale wote ambao andiko langu litawakwaza kwa namna moja au nyingine
images (5).jpeg
images (6).jpeg

-Da’Vinci
 
Mkuu Da'Vinci Hongera kwa kuleta Mada fikirishi, ila nadhani swala la waislamu kuoa wake zaidi ya mmoja si ishara tosha kwamba waislamu watakuwa wengi kuliko wakristu.. kwanini?

Kwa mkondo wa maisha Jinsi ulivyo ni ngumu waislamu kuoa mke zaidi ya mmoja hasa kutokana na swala la uchumi..

Pili waislamu walioa wake wawili au zaidi kipindi masuala ya women empowerment hayajashika kasi.. kwa jinsi wanawake walivyo sasa ni ngumu sana kwa mwanamke kuridhia mke mwenza ndani.. ukimleta wa pili umempoteza wa kwanza..

Tatu..Wakristu watazaliana sana hasa kwa sababu si lazima ndoa ili wakristu wazaliane.. kumbuka si wote wataoa au kuolewa..

Divine Khan
 
Shule niliyosoma UKWATA na TYCS kuna muda walikuwa wanasali pamoja mpaka nikawa nawaambia Martin Luther akifufuka atawachapa viboko kwa kumsaliti.(muungano wa haya madhehebu u karibu sana)
Kwa ukristo huu wa sasa bora tupungue tu,Waislamu wakiwa wengi habari za ushoga na ndoa za jinsia moja zitapungua sana(mashoga jiandaeni kukatwa vichwa kudadeki zenu).
Nimeipenda Biblical quotation uliyotoa.
 
Mkuu Da'Vinci
Kwa mkondo wa maisha Jinsi ulivyo ni ngumu waislamu kuoa mke zaidi ya mmoja hasa kutokana na swala la uchumi..
Mkondo wa maisha upi? Kwanini we ngumu? Kumbuka sijaongelea Tanzania tu nimezungumzia worldwide.
Pili waislamu walioa wake wawili au zaidi kipindi masuala ya women empowerment hayajashika kasi.. kwa jinsi wanawake walivyo sasa ni ngumu sana kwa mwanamke kuridhia mke mwenza ndani.. ukimleta wa pili umempoteza wa kwanza
Hapo juu umesema kea hali ya sasa inaweza kua ngu lakini mm naona ndio inaweza pelekea wanawake kukubali kuolewa kwa Polygam
Hebu cheki data ya wanaosema no na yes polygam
images.png
Tatu..Wakristu watazaliana sana hasa kwa sababu si lazima ndoa ili wakristu wazaliane.. kumbuka si wote wataoa au kuolewa..

Divine Khan
Wakristo rate ya kuzaliana ipo chini kuliko m
Muslim-births-outnumber-Christian-births-by-2035-186x300.png

https://www.google.com/url?sa=t&sou...FjAFegQIAhAB&usg=AOvVaw0_TegBOuifXQ93KA6xgfis
 
Kwa akili zangu za usiku miaka michache baada ya mwaka 2025 dunia itachafuka sana.
Kile kipindi cha miaka 7 ya "shibe" kitakuwa kinaingia ukingoni, ambapo itatanguliwa na Rais wa Marekani ambaye atakuwa maarufu sana kama John Kenedy kutawala kwa muhula mmoja, baada ya hapo ni civil war in America.

Na baada ya mwaka 2063, dunia itaingia kwenye era nyingine kabisa.
Era ambayo imesubiriwa kwa muda mrefu sana.

Ni akili zangu tu za usiku.
Ila mwanangu maneno haya yatunze sana, yana hekima nzito ndani yake.
 
Shule niliyosoma UKWATA na TYCS kuna muda walikuwa wanasali pamoja mpaka nikawa nawaambia Martin Luther akifufuka atawachapa viboko kwa kumsaliti.(muungano wa haya madhehebu u karibu sana)
Kwa ukristo huu wa sasa bora tupungue tu,Waislamu wakiwa wengi habari za ushoga na ndoa za jinsia moja zitapungua sana(mashoga jiandaeni kukatwa vichwa kudadeki zenu).
Nimeipenda Biblical quotation uliyotoa.
Sio kwa ukristo wasasa. Sema wakristo wa sass.... Mm ukisema ukristo basi najua unausema ukatoliki maana ndio imagine pekee thabiti iliyosimama
Thank you kwa Appreciation
 
Hongera kwa kufikiri miaka 100 ijayo safi sana. Yawezekana pia kuna kundi la wapagani ambalo haliamini chochote linaongezeka kwa kasi
Ahsante Sana
Kiuhalisia kabisa hilo kundi linakua kwa kasi hasa western countries..
Wengi ni wakristo jina
 
Kusema ukweli hamna prediction hapa, kaa tulia andika upya huwezi ku predict future kwa kugoogle story, soma vitabu, makala, vatilia vipindi kuhusu future eg sci-fi cha DS. Ukiandika usiwe na haraka, tumia Ms word ku andaa story alafu ukimaliza copy u pest hapa jf.
 
Shule niliyosoma UKWATA na TYCS kuna muda walikuwa wanasali pamoja mpaka nikawa nawaambia Martin Luther akifufuka atawachapa viboko kwa kumsaliti.(muungano wa haya madhehebu u karibu sana)
Kwa ukristo huu wa sasa bora tupungue tu,Waislamu wakiwa wengi habari za ushoga na ndoa za jinsia moja zitapungua sana(mashoga jiandaeni kukatwa vichwa kudadeki zenu).
Nimeipenda Biblical quotation uliyotoa.
Una uhakika kuwa mashoga watapungua? Fanya research mkuu! Chunguza % kubwa ya machoko hapa bongo ni wa dini gani utapata jibu
 
Kwa akili zangu za usiku miaka michache baada ya mwaka 2025 dunia itachafuka sana.
Kile kipindi cha miaka 7 ya "shibe" kitakuwa kinaingia ukingoni, ambapo itatanguliwa na Rais wa Marekani ambaye atakuwa maarufu sana kama John Kenedy kutawala kwa muhula mmoja, baada ya hapo ni civil war in America.

Na baada ya mwaka 2063, dunia itaingia kwenye era nyingine kabisa.
Era ambayo imesubiriwa kwa muda mrefu sana.

Ni akili zangu tu za usiku.
Ila mwanangu maneno haya yatunze sana, yana hekima nzito ndani yake.
Sikupingi yote yanawezekana kabisa maana matukio mengi tu yanotokea yakiwa yamepangwa kwa miaka mingi..
Ref. Tukio la J.F. Kennedy na Abraham Lincoln,World war I, Kuzama kwa Titanic etc
 
Kusema ukweli hamna prediction hapa, kaa tulia andika upya huwezi ku predict future kwa kugoogle story, soma vitabu, makala, vatilia vipindi kuhusu future eg sci-fi cha DS. Ukiandika usiwe na haraka, tumia Ms word ku andaa story alafu ukimaliza copy u pest hapa jf.
Nilichogugo no picha tu zilizokua naona zinafanana na mawazo yangu.. Is it a crime? Thanks for your contribution..
 
Sio kwa ukristo wasasa. Sema wakristo wa sass.... Mm ukisema ukristo basi najua unausema ukatoliki maana ndio imagine pekee thabiti iliyosimama
Thank you kwa Appreciation
nimekulia kwenye ukatoliki na kupata sakramenti tatu lakini kwa mtazamo wangu ukatoliki unachangia sana ukristo kuonekana umepinda(dhaifu) halafu wanafuata walokole uchwara(wapiga dili).
Nikipewa uwezo wa kufuta dini moja(au dhehebu) hapa duniani naifuta RC na kuwaacha Waislamu.
Samahani kwa kukuonyesha chuki yangu.
 
Mkuu Da'Vinci Hongera kwa kuleta Mada fikirishi, ila nadhani swala la waislamu kuoa wake zaidi ya mmoja si ishara tosha kwamba waislamu watakuwa wengi kuliko wakristu.. kwanini?

Kwa mkondo wa maisha Jinsi ulivyo ni ngumu waislamu kuoa mke zaidi ya mmoja hasa kutokana na swala la uchumi..

Pili waislamu walioa wake wawili au zaidi kipindi masuala ya women empowerment hayajashika kasi.. kwa jinsi wanawake walivyo sasa ni ngumu sana kwa mwanamke kuridhia mke mwenza ndani.. ukimleta wa pili umempoteza wa kwanza..

Tatu..Wakristu watazaliana sana hasa kwa sababu si lazima ndoa ili wakristu wazaliane.. kumbuka si wote wataoa au kuolewa..

Divine Khan
Ni kweli wa suala la kuoa wake wengi sio factor kubwa ingawa ni moja ya factor ya future ya uislam hapo badae lakini zaidi ni relevance ya maadili ya kiislam katika ulimwengu,suala la kukithiri Kwa vitendo vya kishoga makanisani, contradiction ya biblia yenyewe kimaandishi mfano mpaka sasa wamarekani wengi Sana wameamia kwenye uislam na hasa wanawake licha ya propaganda nyingi zilizo zinazo sema Islam is against women nk na Hali inavyohashiria uislam utapaaa Sana miaka 20 ijayo kulingana na Mambo yanavyotokea duniani hivi sasa na mabadiliko mbalimbali duniani hasa kimaadili
 
nimekulia kwenye ukatoliki na kupata sakramenti tatu lakini kwa mtazamo wangu ukatoliki unachangia sana ukristo kuonekana umepinda(dhaifu) halafu wanafuata walokole uchwara(wapiga dili).
Nikipewa uwezo wa kufuta dini moja(au dhehebu) hapa duniani naifuta RC na kuwaacha Waislamu.
Samahani kwa kukuonyesha chuki yangu.
It's better to be honest..
Kua na amani
 
Kusema ukweli hamna prediction hapa, kaa tulia andika upya huwezi ku predict future kwa kugoogle story, soma vitabu, makala, vatilia vipindi kuhusu future eg sci-fi cha DS. Ukiandika usiwe na haraka, tumia Ms word ku andaa story alafu ukimaliza copy u pest hapa jf.
Wewe ndivyo unavyofanyaga?
 
Back
Top Bottom