Shekaina Glory
Senior Member
- Jun 18, 2025
- 180
- 85
Akiongea mbele ya wachambuzi wa habari na uchumi, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia Nchini (PPPC), Bw. David Kafulila, alisisitiza kuwa migogoro mikubwa ya dunia siku za usoni haitatokana na mafuta au gesi, bali maji. Watafiti wanasema huenda Vita ya Tatu ya Dunia ikapiganwa kwa sababu ya maji, hali inayoibua changamoto na fursa kubwa kwa Tanzania.
Kafulila alibainisha kuwa 16% ya eneo la Tanzania ni maji, na taifa linamiliki sehemu kubwa ya Ziwa Tanganyika, ziwa lenye kina kirefu zaidi Afrika na moja ya hifadhi kubwa za maji safi duniani. Aidha, Ziwa Tanganyika pekee linahifadhi takribani 17% ya maji safi yote duniani, jambo linaloifanya Tanzania kuwa miongoni mwa mataifa machache yenye hazina ya kipekee ya kimkakati.
Alisisitiza kuwa maji ni rasilimali adimu, haiwezi kubadilishwa, na ndiyo msingi wa maisha, kilimo, viwanda na usalama wa taifa.
Kwa mujibu wa takwimu za Serikali ya Awamu ya Sita:
- Bajeti ya sekta ya maji imeongezeka kutoka Sh. bilioni 733.28 (2020/21) hadi Sh. trilioni 1.15 (2025/26).
- Miradi 630 imetekelezwa, ikijumuisha vituo vya kuchotea maji 6,553, na kunufaisha wananchi zaidi ya milioni 4.3 katika vijiji 1,390.
- Upatikanaji wa huduma za maji vijijini umeongezeka kutoka 70.1% (2020) hadi 83% (2024); na mijini kutoka 84% hadi 91.6%.
- Vijiji/mitaa vilivyounganishwa na huduma za maji vimeongezeka kutoka 5,528 (2021) hadi 10,779 (2024).
- Miradi mikubwa ya maji imewanufaisha wananchi zaidi ya milioni 21, ikiwa ni pamoja na Same–Mwanga–Korogwe, Kidunda, Tabora–Nzega–Igunga–Singida, na Mradi wa Miji 28 wenye thamani ya Sh. trilioni 1.3
Kafulila alisisitiza kuwa Tanzania inapaswa kulinda na kutumia kikamilifu vyanzo vyake vya maji kwa maendeleo kwani kesho itakuwa ya shida kwenye maji, Ameeleza kuwa kwasasa Umeme sio hoja tena kwani umepata mbadala ndio maana nchi kama Rwanda tayari zinatumia kinyesi na taka ngumu kuzalisha nishati (biogas na waste-to-energy). Miradi ya aina hii imesaidia kupunguza uchafuzi wa mazingira, kuongeza ajira, na kuimarisha upatikanaji wa nishati safi kwa maelfu ya kaya vijijini na mijini.
Mfano ni mradi wa biogas vijijini Rwanda ambao umewezesha mamia ya kaya kutumia kinyesi cha binadamu na mifugo kuzalisha gesi safi ya kupikia na umeme. Pia, Rwanda inajenga kituo cha umeme wa taka mjini Kigali kitakachozalisha hadi 15 MW za umeme, kikiwa kielelezo cha ubunifu wa Afrika katika kutumia rasilimali zilizopo.
Kafulila aliishia kwa kutoa wito:
Mfano ni mradi wa biogas vijijini Rwanda ambao umewezesha mamia ya kaya kutumia kinyesi cha binadamu na mifugo kuzalisha gesi safi ya kupikia na umeme. Pia, Rwanda inajenga kituo cha umeme wa taka mjini Kigali kitakachozalisha hadi 15 MW za umeme, kikiwa kielelezo cha ubunifu wa Afrika katika kutumia rasilimali zilizopo.
Kafulila aliishia kwa kutoa wito:
“Kesho dunia itapigania maji – sisi tayari tunayo. Tukiyalinda vyanzo vyetu vya maji na tukijifunza kutoka mifano ya majirani zetu kama Rwanda katika kutumia taka na kinyesi kuzalisha umeme, Tanzania inaweza kuwa si tu taifa la amani, bali pia nguzo ya uchumi na usalama wa kimataifa.”