David Wakati azikwa Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

David Wakati azikwa Dar

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Dec 6, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 6, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Waombolezaji wakiondoa jeneza lenye mwili wa Mkurugenzi wa zamani wa Mkuu wa Radio Tanzania Dar es Salaam (TBC), David Wakati, baada ya misa ya kumuombea iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Alban jijini Dar es Salaam na kuelekea kwenye makaburi ya Kinondoni kwa mazishi jana.


  Aliyekuwa Mkurugenzi wa Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) ambayo hivi sasa inayojulikana kama TBC ll Taifa, David Wakati, alizikwa jana katika makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
  Misa ya kumuombea marehemu ilifanyika katika Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Alban ambapo Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Dk.Valentino Mokiwa, aliongoza sala ya kumuombea marehemu na kusema kuwa atakumbukwa na Watanzania wengi kwa ucheshi wake na mchango alioutoa katika tasnia ya habari.
  “Katika kusherehekea miaka 50 ya uhuru kama historia ya utangazaji itaandikwa, hakika jina la David Wakati halitakosekana katika sura zake nyingi kwa mchango mkubwa alioutoa,” alisema mmoja wa wanafamilia wakati akisoma historia fupi ya marehemu
  Aidha, misa hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na watu mashuhuri, akiwemo Mwanasheria Mkuu wa zamani, Jaji Mark Bomani; Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Lewis Makame; Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi; Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi na Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Paul Rupia.
  Marehemu Wakati alifariki dunia Desemba Mosi, 2011 katika hospitali ya Regency na ameacha watoto watatu, ambao ni Mandela Kenneth, John Kuchi na Steve Biko.  CHANZO: NIPASHE

   
 2. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #2
  Dec 6, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  R.I.P Mzee wakati,nitakukumbuka kwa utangazaji uliotukuka na pia nakumbuka wakati ule Dr SAS ni balozi wetu kule Yuno mzee alikuwa kila trip anaenda yeye kutangaza mambo yanayojiri hapo Yuno laivu bila chenga kupitia RTD,siku hizi hayo mambo hakuna sijui kwa nini
   
 3. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #3
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mwenyezi mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema.
   
Loading...