Bila shaka, David Mosher aliamini kuwa mchumba wake, Heather, angepona tatizo alilokuwa akipambana nalo, kansa ya titi. Ndiyo maana alimwahidi kumwoa pindi atakapopona.
Lakini ilipogundulika kuwa tatizo limeshavuka hatua ya kutibika, na kwamba mchumba wake alikuwa na muda mfupi tu wa kuishi, hakubadili msimamo. Aliamua kutimiza ahadi yake kwa kufunga naye pingu za maisha wodini.
Tukio hilo lilitukia mwaka 2017 nchini Marekani.
1. Ndoa ilifungishwa hospitalini
2. Tukio lilihudhuriwa na wanafamilia na marafiki wachache
3. Japo Heather alikuwa amedhoofika sana, bado alimudu kula kiapo cha ndoa kwa furaha. Ilikuwa ni kati ya siku aliyofurahi sana.
4. David na Heather walikuwa wanafahamu kuwa wana muda mfupi sana wa kuwa pamoja.
5. David anasimulia kuwa japo ilikuwa ni siku ambayo alipaswa kufurahi, kwake ilikuwa kama ibada ya mazishi. Alijua mkewe angekufa muda si mrefu.
6. Masaa kumi na nane baada ya ndoa kufungwa, Heather ambaye kwa wakati huo alijulikana rasmi kama mke wa David, aliaga dunia. Kauli yake ya mwisho ilikuwa ni kiapo cha ndoa. Baada ya hapo, hakufungua kinywa mpaka mauti yalipomkuta.
7. David Mosher alihuzunika sana lakini alikuwa na amani moyoni kwa kuwa aliitimiza ahadi yake.
Tukio hilo linakufundisha nini?
Source: QUORA - Photo taken in 2017 at the wedding of Heather and David