Mhere Mwita
JF-Expert Member
- Jan 24, 2012
- 235
- 1,275
Katika vita ya Ufisadi Magufuli zingatia ushauri huu Rais wangu!
Leo Jan 25, 2017, Taasisi ya Kimataifa ya Transparency Internation inayohusika na Masuala ya uwazi na vita dhidi ya Ufisadi duniani imeitaja Tanzania, Kenya, Africa ya Kusini na Nigeria kama nchi ambazo bado zimeshindwa kufanya vzr sana katika vita dhidi ya ufisadi. Kwa Tanzania imendelea kushika nafasi ya pili baada ya Rwanda huku Kenya ikiwa nyuma ya Tanzania. Ambapo kwa mwaka huu 2016, Tanzania imepata alama 32 ambazo ni hatua mbili ukilinganisha na mwaka 2015 ambapo ilipata alama 30 , lakn nyuma ya 2013 ambapo ilipata alama 33 na 2012 alama 35.
Jambo muhimu na kubwa nilopenda ambalo hakika ni vema Rais wetu akazingatia ni ushauri uliotolewa kwa maRais wa Afrika ambao waliingia madarakani kwa tiketi ya kupiga vita Ufisadi. ambapo wamashauliwa kufanya mambo makubwa 3 ili kuhakikisha wanaishi ahadi yao ya vita dhidi ya ufisadi;
1.Lazma watekeleze ahadi hiyo kwa kuhakikisha misingi ya Demokrasia, Utawala bora na Haki za binadamu inaheshimika
2.Wahakikishe tasisi zinazosimamia uwajibikaji wa serikali zinaimalishwa(bila shaka vyombo vya habari, Bunge na Taasisi za kiraia zinapaswa kupewa nguvu kutimiza wajibu).
3.Kujenga mfumo thabiti wa uchaguzi ambapo Umma utakuwa na nguvu ya ama kuwaruhusu waendelee au kuchagua mbadala.
Naomba kujua kwa maoni yako,Rais wetu anaishi misingi hii muhimu ktk vita ya ufisadi kwa kiasi gani? shauri usitukane wala kukejeli.