David Kafulila ndani ya kipindi cha Dakika 45, ITV

David Kafulila ndani ya kipindi cha Dakika 45, ITV

Seaman88

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2012
Posts
417
Reaction score
156
Leo saa tatu atakuwa mh David Kafulila katika kipindi cha dakika 45 ITV.

Atazungumzia mengi usiyoyafahamu kuhusu ESCROW na sakata la mabehewa feki pia kushuka kwa thamani ya shilingi.
 
Jembe Ukawa jamaa huwa hakoseagi stay tune!
 
Namkubali kafulila sana....hapendi sifa za kijinga kama yuda iskariot
 
tunagombea sana remote wife ana angalia channel zake dstv sisi wengne tunataka siasa. je hakuna radio inayorusha hicho kipindi?
 
tunagombea sana remote wife ana angalia channel zake dstv sisi wengne tunataka siasa. je hakuna radio inayorusha hicho kipindi?
 
Amezungumzia Escrow,kwamba kama rais alisema pesa si za umma iweje wale jamaa wafunguliwe mashtaka.anatoa mfano hapa,ni lini watu wakashtakiwa kwa kugawiwa pesa na Bahresa
 
Mtangazaji anahoji kuwa haoni kama uibuaji wa Escrow umekosesha misaada.anajionaje yeye kuwa ni moja ya wakwamishamishaji
 
Anasema bajeti kuacha kutegemea wahisani ni sizitaki hizi mbichi kwa kuwa hawawezi kupata misaada au mikopo kutoka kwa wahisani.
 
Na bado Wahisani wamekata misaada kutokana na ufisadi wa ESCROW.

Sasa kifuatacho, wakiahirisha uchaguzi, ndo nchi itawekewa Vikwazo. Napenda tu wazuie pesa zao walizoweka USWISS.

Hureee, Magamba waambieni NEC waahirishe uchaguzi mkuu ili Pesa za USWISS zitaifishwe mfe kwa Presha..
 
Msaada wa MCC2 haujasaini mpaka sasa kutokana na serikali kushindwa katika good governance.Waziri alidanganya bunge.ule mpunga ni zaidi ya trilioni 1
 
Anaeleza kuhusu mabehewa,anaeleza jinsi uchakachuaji ulivyofanyika.Mzabuni alilipwa kabla ya mzigo kufika.iweje kuna wazabuni wamefanya kazi hawajalipwa mpaka leo.Anataka mawaziri wawajibike
 
TBS imekufa bidhaa feki zinajaa Tanzania

Mfano, mabati feki

TBS ina ufanisi mdogo sana
 
Kafulila ameivua serikali ya CCM nguo na kuiacha uchi wa mnyama, ni aibu kubwa kwa serikali hii, watanzania tujifunze kukinai, ccm wanatupeleka kubaya, tusipochukua hatua tutakufa maskini na kwa mungu tutaadhibiwa kwa kukubali kudhulumiwa na kakikundi ka wahuni wachache
 
leo saa tatu atakua mh devid kafulila katika kipindi cha dak 45 ITV...atazungumzia mengi usiyoyafaham kuhusu escro na sakata la mabehewa feki.....pia kushuka kwa thamani ya shilingi.

UKAWA jamn acha tu....go on ngeedere go on son tel d trut en shame d devil
 
Back
Top Bottom