David Kafulila atunukiwa Tuzo kwa hoja ya Escrow

David Kafulila atunukiwa Tuzo kwa hoja ya Escrow

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
11174842_10152974108013640_8056904449216816788_n.jpg
Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila anapewa award na taasisi ya HUMAN RIGHTS DEFENDERS kwa kazi ya escrow.

Mgeni rasmi ni balozi wa Jumuiya ya ulaya. Shughuli hiyo itafanyika asubuhi hii katika ukumbi wa Blue Pearl Ubungo Plaza.

Akihutubia huko Muhambwe Kigoma juzi David Kafulila alilaani wanasiasa wanaotaka kudandia hoja ya Escrow ili kujipatia umaarufu huku wakiwa hawana hadhi yoyote kuzungumzia hoja hiyo.

Kafulila pia aliwataka wananchi kuhakikisha wanachagua wagombea wote wanaotokana na UKAWA kwenye uchaguzi mkuu ujao.

===
Wakuu hapa nawawekea kwa kifupi kile ambacho kilikuwa kinaendelea katika hili tukio......Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, leo wameazimisha "Siku ya Watetezi wa Haki za Binadamu" ambapo katika Siku hii pia Mtandao wa THRDC wamemkabidhi Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi) ngao ya heshima baada ya kuonyesha jitihada binafsi za kutetea sakata la Escrow.

attachment.php

Ernest Sungura, Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania, (TMF) amesema katika kuelekea katika uchaguzi mkuu, wanahabari wanatakiwa kulindwa na vyombo vinavyoweza kudhamiria kuwakingia kifua kutokana na wao kuandika habari za uchunguzi ambazo mara kwa mara zimeonekana kugusa maslahi ya watu mbalimbali moja kwa moja.

Wawakilishi kutoka nchi za Umoja wa Ulaya nchini, na Washauri wa Masuala ya Haki za Binadamukatika nchi za Umoja wa Mataifa wameeleza kuwa, kama Serikali haithamini haki za mtu moja moja ipo hatari kubwa ya kupoteza nguvu kazi ya taifa kwa jambo ambalo lingeweza kutatuliwa kwa njia rahisi.

Balozi wa Jumuiya ya Ulaya chini, Filberto Sebrregondi, amesema umefika wakati wa kila mwananchi kutambua kuwa wimbi la kuminywa haki za watu wasio na uwezo lin akuwa kwa kasi nchini, licha ya kubainisha kwamba amefurahishwa kwa namna washiriki walivyoonyesha ushirikiano kwa mwamvuli wa mitandao hiyo ya kutetea haki za binadamu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk.Helen Kijo-Bisimba, akiongea katika maadhimisho hayo, alisisitiza kwamba haki za binadamu ndizo zinazowafanya wanadamu waishi na kwamba mtu yeyote asipofanya utetezi wa haki za binadamu…anataka ubinadamu wa wengine uishie njia panda.

Mratibu wa THRDC, Onesmo Ole Ngurumwa, akiongea mara baada ya ufunguzi wa siku hiyo, alisema maaadhimisho haya ni ya pili kufanyika Tanzania ambapo kwa mara ya kwanza yalifanyika mwaka 2013.

Ametaka siku hii itambuliwe kimataifa na isiwe nchini tu, huku akisisitiza kwamba wanaofanya utetezi huo waangalie usalama wao katika harakati za kupigania haki za wengine.

Maadhimisho hayo yameenda sambamba na maonyesho ya watetezi hao, ambapo hao ikiwemo Kampuni ya Jami Media (Wamiliki wa mitandao maarufu ya kijamii nchini ya FikraPevu.com na JamiiForums, TGNP Mtandao, TAMWA, LHRC, HAKI ARDHI INSTITUTE, JUKWAA LA KATIBA, TAWLA, SIKIKA, ZLSC, TAS, TACOSODE, TANLAP, LEAT,Human Rights Comission, TVVA, Haki Catalyst, German Foundation, German Embasy,SANA, na CESOPE.
attachment.php


Waliotukukiwa tuzo

Watetezi waliotambulika na kupewa zawadi ya kuwa watetezi bora wa mwaka 2014 kutokana na mazingira hatarishi waliyofanyia utetezi wao ni David Kafulila aliyepokea tuzo ya Wajasiri wa kuibua maovu (Whistle blower), Mtetezi Mwanamke wa mwaka 2014 ni Bi. Salma Hamoud na Mtetezi wa haki za binadamu vijijini akiwa ni Maanda Ngoitiko.

Adhimisho hili limekuja baada ya siku mbili za warsha ya Universal Periodic Review, warsha ambayo ililenga kuleta pamoja asasi za kiraia ili ziweze kufuatilia utekelezaji wa Mapendekezo 107 yaliyotolewa na nchi wanachama za Umoja wa Mataifa na kukubaliwa na nchi.
 
Zitto ni hovyo kibara mkubwa na mpenda sifaa wa kupindukia.
 
akit weye pesanhovyo hovyo kwZittowhovyomhovyoakia maslai
yao.Zitto badirika mkuu kama ni hela umeshavuta nyingi
 
Namkubali sana huyu tumbili,ni bora kuwa tumbili kuliko kuwa mwanadamu fisadi.
 
Hongera Kafulila. Unastahili kabisa. Sio wale wanaojipaka damu waonekane wachinjaji kumbe ni wauza bucha tu!!
 
Hakika anastaili lakin hata yule aliyempenyezea taarifa hizo atafutwe apewe tuzo
 
kafulila na vyama vya siasa ktk Ukawa sasa wataona kwamba wamebahatika sana kupanda boat iliyo na Mungu.Na utulivu wao umewaepusha kufa na huyu jamaa wa kujilipua
 
Katika nchi zenye binadamu waliokamilika na wanaotumia akili tuzo hii ni kubwa na heshima lakini kwa binadamu kama Watanzania wengi tunadhani kumiliki ghorofa na land cruiser kwa pesa za escrow ni heshima zaidi!
 
Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila anapewa award na taasisi ya HUMAN RIGHTS DEFENDERS kwa kazi ya escrow.

Mgeni rasmi ni balozi wa Jumuiya ya ulaya. Shughuli hiyo itafanyika asubuhi hii katika ukumbi wa Blue Pearl Ubungo Plaza.

Akihutubia huko Muhambwe Kigoma juzi David Kafulila alilaani wanasiasa wanaotaka kudandia hoja ya Escrow ili kujipatia umaarufu huku wakiwa hawana hadhi yoyote kuzungumzia hoja hiyo.

Kafulila pia aliwataka wananchi kuhakikisha wanachagua wagombea wote wanaotokana na UKAWA kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Safi saaaaana! Dogo anastahili kutambuliwa zaidi na zaidi, nilisema siku chache zilizopita kuwa kuwa Kafulila ni jembe na ana baraka zote za National Leader wa Taifa hili - tuna wazalendo wachache sana wa aina ya David ambaye baadhi yao yalimwita mnyama TUMBILI.

Hili ni moja ya mapigo yanayo mmaliza ZZK na mamburula wake ambao amewafanya kuwa bendera kufuata upepo!
 
Leo Mh Kafulila anapewa award na taasisi ya HUMAN RIGHTS DEFFENDERS kwa kazi ya escrow. Mgeni rasmi ni balozi wa Jumuiya ya ulaya. asubuhi hii Blue Pearl. Ubungo Plaza.

Hongera mheshimiwa kwa kazi nzuri, Panyabuku la Lumumba lilisema lenyewe ndilo lililopigania escrow, tayari ccm washalipatia tuzo yake ya kuua upinzani nchini.
 
Back
Top Bottom