David Kafulia kuzungumza yaliyojiri NCCR: LIVE ON STAR TV

Mh. Kafulila, kwakuwa umeweka wazi kuwa chadema haukufukuzwa isipokuwa ulijiengua mwenyewe, je, upo tayari kuachana na kesi ya mahakamani na kurudi chadema au ujiunge na CCM ili ulitetee jimbo lako?
 
Naomba kafulila ajb nn klchomfanya atoke CDM km kwel hakufukuzwa awe wazi tujue watanzania.
 
maswali muliyomuuliza yanatosha kumuonyesha ajue kua ni mbovu.cha msing ajirekebishe arudi cdm tutampokea kama hatakua mamluki

Olyset kama umemuona ni mbovu kwa nini unamuhitaji chadema ..hapa ni kumpa nafasi mwenyewe aeleze yaliyotokea na ndipo kutoa conclusion kama hizi
 
Yahaya naomba kafulila atueleze kuhusu ile barua iliyokuwa hapa jf last week akiomba msamaha kwa mwenyekiti tena kwa kulia na kupiga magoti na kumwita mwenyekiti baba'alikuwa na maana gani?
 
Mh Kafulila naomba uondoe utata kwenye kesi ya msingi uliyofungua,maana ndg machali alikuja na kipande cha mahakama akisema umeomba nccr wasiendelee kukujadili. Ivo haujaomba kusitisia maamuzi ya chama ya tar16. Je ni kweli ivo?na kama ivo huoni kuwa wakili wako kakuingiza mkenge?
 
Kafulila, kama mahakama ya wanasiasa ni wananchi mbona umeenda mahakamani? Kwanini hukuwashitaki nccr kwa wananchi?
 
Napenda jinsi Kafulila anavyojibu hoja kwa utulivu bila jazba wala maneno ya kashfa kama walivyofanya Machali na Ruhuza.
 
Swali...ndugu kafulila sisi wapiga kura wako tukikuomc urudi chama imara,chenye demokrasia chadema ili uungane na wapinzani wa kweli uendeleze harakati utatukubalia au mahakama ikiamua vinginevyo basi kura zetu tumpe mwingine?
 
Hiv kafurila ulipoungana na hamad rashd kupeleka hoja ya neno kambi lasmi ya upinzan,ulitumwa na nccr?
 
Swali kwa kafulila; unapohoji hualali wa kikao cha watu takribani 60, kwa hoja kuwa wewe umechaguliwa na watu wengi zaidi, unamaanisha hata sisi wananchi tuhoji uhalali wa nyie pale bungune kufanya maamuzi kwa niaba yetu sisi tuliye wengi??
 
Tatizo ni Uenyekiti .. EL Alisema Tatizo ni Uwaziri Mkuu

Kafulila bado Kijana Tulia tu jipange upya
 
wa SAUT Mwanza. CUF walimaanisha nini kusema kupitia kwa Ndg. Mtatiro kuwa watauheshimu uamzi wa mahakama lakini hawatatengua uamzi wao dhidi ya Mohamed Rashid? Je, CUF iko juu ya sheria za nchi?
 
nini suluhu ya hii migogoro inayotokea kwenye vyama maana watanzania tumechoka na habari hizo za migogoro badala ya kuwatumikia wananchi nyie mnatumia muda mwingi kwa ajili ya kutatua migkutatua migogoro.
 
Kafulila wewe ni muungwana ,nikiangalia tofauti ya Mada ya week iliyoisha kati ya viongozi wa NCCR Mageuzi kwanza walikuwa wakiongea kwa Jazba kubwa wakikukandamiza na wewe kuonekana unamakosa makubwa mtovu wa nidhani na kila lawama kwako ,Lakini kwako imekuwa tofauti unaongea kwa umakini bila kumchambua mtu yoyote vibaya na umesimamia kwenye point zaidi ,.. all the best mie ni msikilizaji na imani haya malumbano yenu yataisha na ujipange vyema sasa
 
davd kafulila usife moyo ndugu yangu, ndio ubaya wa vyama vyetu vya kisiasa wakisikia tu unataka kugombea nafasi za juu katika chama matatizo, waulize kina MARANDO, PR SAFARI, HAMADI, SHIBUDA, na wangine wengi so usife moyo kaza buti

serikari/mahakama/wadau ndo wakati muafaka huu kufanya mabadiliko katika katiba kuruhusu mgombea binafsi,
 
Namuuliza kafulila kutokana na trend ya kutimuliwa ktk vyama viwili chadema(mwanzo) na nccr(sasa),hapo hawezi onekana kwamba yeye ndio mwenye matatizo?

Yahaya tuwekee hapa jamvini wote tuone hata sisi hatupati star tv

Satellite downlink parameters for Star TV
SR 4900 KS/s
FEC 1/2
Frequency 3884MHz
Polarization LHCP
Sat IS 906
 
wa SAUT Mwanza. CUF walimaanisha nini kusema kupitia kwa Ndg. Mtatiro kuwa watauheshimu uamzi wa mahakama lakini hawatatengua uamzi wao dhidi ya Mohamed Rashid? Je, CUF iko juu ya sheria za nchi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom