David Cameron calls Nigeria and Afghanistan 'fantastically corrupt'

David Cameron calls Nigeria and Afghanistan 'fantastically corrupt'

Kwani uongo? Tatizo waafrika sisi tukiambiwa ukweli tunageuka mbogo
 
  • Thanks
Reactions: kui
Cameron angekuwa na uwezo wakuongea hayo maneno mbele ya hao viongozi wa nchi anazoziita mabingwa wa rushwa ningemuona shujaa ila hii ya kwenda kuongea kinafiki kwa malkia namuona kama mtu mwoga na asiye jiamini..!
 
Ni kweli, lakini hata Hitler alisema waisraeli ni wauaji. Baada ya hapo unafahamu kilichofuata kwa waisraeli waliokuwa wakiishi Ujerumani. Hii tunaita mbwa kala mbwa hakuna wa kumlalamikia mwenzake.

Lakini kwenye hiyo kanda iliyovuja, yule pasta anaonekana akimwambia malikia kuwa, ila huyu rais mpya (buhari) na serekali yake sio mafisadi, malikia nae akajibu kweli eeeh? Mwisho wa kunukuu, hii inaonesha cameron alikuwa anaongelea utawala wa goodluck J ambao kwa kiasi kikubwa ulitikiswa na skendo za ufisadi na rushwa mpaka kesho.
 
amesahau namna mzee wake alivyokua akikwepa kulipa mamilioni ya mapaundi kama kodi..
 
Kwani Nigeria rushwa imeisha???!!!
Mbona waafrika tunapenda kusifiwa ...
Hata kama anapambana na rushwa haina maana rushwa kwa serikali ya Nigeria imeisha...hata kama Rais wa sasa wa Nigeria ni malaika
 
Hebu
Kwani Nigeria rushwa imeisha???!!!
Mbona waafrika tunapenda kusifiwa ...
Hata kama anapambana na rushwa haina maana rushwa kwa serikali ya Nigeria imeisha...hata kama Rais wa sasa wa Nigeria ni malaika
Kwani huko uingereza ndio imeisha,yy mwenyewe fisadi kuu,mbona hajisemi,acheni upuuzi wenu eboh, kwani hakuna njia nyingine ya aL washenzi kutusaidia kutatua matatizo yetu zaidi ya kutukana
 
amesahau namna mzee wake alivyokua akikwepa kulipa mamilioni ya mapaundi kama kodi..
Yaani mm mwenyewe huwa nashangaa sisi mijitu meusi ,kila anachosema mzungu hata kama tusi bhac tumekuwa watu wa hewala tu,eti hatupendi ukweli...!!???
 
Haya Nigeria inaongoza kwa kuwa nchi safi...zero tolerance kwa rushwa....happy???!!!!
 
Back
Top Bottom