Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 969
- 1,939
Serikali ya Uingereza imethibitisha kuwa taarifa za kiafya za watu 500,000 waliojitolea kwenye mradi mkubwa wa utafiti (UK Biobank) ziliwekwa sokoni kwa ajili ya kuuzwa kupitia mtandao wa Alibaba nchini China.
Taarifa hizo zimeondolewa utambulisho kwani hazikuwa na majina, anwani, wala namba za simu. Hata hivyo, zilijumuisha taarifa nyeti kama vile jinsia, umri, hali ya kiuchumi, mtindo wa maisha, na baadhi ya vipimo vya kibaolojia vya wahusika.
Aidha, Uvujaji huu umetokana na watafiti kutoka taasisi tatu za kitaaluma ambao walikiuka mikataba yao ya matumizi ya data hizo baada ya kupewa idhini ya kuzitumia kwa ajili ya utafiti.
Taarifa hizo ziliondolewa haraka sana kwenye mtandao wa Alibaba kufuatia ushirikiano kati ya serikali ya Uingereza, China, na mtandao huo. Pia, watafiti na taasisi zilizohusika kukiuka mkataba wamesimamishiwa uwezo wa kupata data hizo.

Waziri wa Teknolojia wa Uingereza, Ian Murray, ametoa hofu na kueleza kuwa hakuna mtu yeyote aliyefanikiwa kununua taarifa hizo kabla hazijaondolewa mtandaoni.
SOURCE: BBC