Tumeoshwa akili kiasi kwamba hatufikirii kwa uwezo wetu bali kwa mwongozo wa watu wengine!!Ni aibu kweli mtu kujikataa na asili yako namna hii!!
nafuu umekuja. Maana kwenye ile thread ya wakati ule ulisema: "...Nwy sioni ukweli wowote maana wadada kibao nao wako na wazungu!!!"
Sasa unaamini ni kweli?
Ishu sio kua na mzungu au kua na mtu mweupe bali ni kile kinachomsukuma mtu kumchagua huyo mweupe!!Wapo hao wenye hayo mawazo ya kupata mtoto mwenye ngozi mng‘aro na wanaoolewa kwa sababu tofauti kabisa!!
mimi kinachoniudhi most....
unakuta una mpenzi wako mswahili...
unajitahidi kumfanya ajisikie yeye ni queen fulani hivi....
but wakitokeza wazungu au waarabu....
unakuta mdada wa kiswahili anakuwa mnyonge mnyonge hivi...
i hate that
Exactly...
Kuna ndugu yangu anafanya kazi ofisi moja hapo dar. Karudi kutoka nje. Kuna mzungu hapo ofisini. Kazi yake haileweki, lakini kajifanya ni boss wa hapo. Watu wanamuogopa kweli. Unakuta hana hata qualification.
A bit off topic lakini angalia hii video uone hawa waandishi wanavyouliza maswali kipumbavu! Yani niliangalia nikashikwa na hasira! Ishu ya Dowans kuna maswali makubwa kibao, yeye anauliza kuhusu capacity! Kutokujiamini ni mbaya mno!
This is the reason why I don't even think of living in Ist world countries. Wazungu wame wa brainwash hawa ndugu zetu na kuwafanya waone kila kitu walichonacho ni cha hovyo. Nadhani ndio maana hata huko US blacks ni failures in life kwa kuwa wamekuwa bullied maisha yao yote. I love my country. Na si skin tu hata mambo mengine.
Nilisoma kitabu cha gifted hands, nikawachukia sana wazungu. Yaani hata walimu wanawashauri wanafunzi wa asili ya kiafrika wazingatie sana masuala ya arts si masomo mengine kama science. Maanake black waishie kuwa wasanii tu.
Nadhani ndio maana kina Jay Zee wamekuwa wanatembelea sana Africa kwani wame learn kuwa its here where they belong.
Of course ishu sio kuwa na mzungu. Nadhani hujanipata vizuri! Kwenye ile thread nyingine tulikuwa tunazungumzia kuhusu wasichana wa kiafrica kuchukia pale ambapo mwanaume wa kiafrika anapotoka na mzungu. Na hii ni kwa sababu ni ngumu kwao kupata wazungu. Nikaongeza kuwa hii ni zaidi kwa wasichana walio na very dark skin.
Wewe ndio ukajibu kuwa hakuna ukweli na hiyo statement....
Sasa nadhani tukubali kuwa kuna ukweli!
Mimi nakubaliana na wewe kuwa tumeoshwa akili. Kuna kitu kinaitwa subliminal message. Ijapokuwa definition yake inaweza isiendana in total na ninavyoeleza hapa, lakini nadhani mtaelewa picha.
Mara nyingi ukiangalia movies, wasichana wazuri ni weupe. Ukiona picha ya Yesu, ni mzungu. Ukiangalia cartoons hasa kwa watoto, superhero ni mzungu. Hii inajenga perception kichwani kwa mtu kuwa white = good. Ni mbaya kweli! Na natumaini tutaweza kubadilisha hii. Ndio maana napenda Actors kama Denzel Washington, Samuel L Jackson, maana wana break hiyo pattern. Lazima tuanze kujenga image ya Black is beautiful!
mimi kinachoniudhi most....
unakuta una mpenzi wako mswahili...
unajitahidi kumfanya ajisikie yeye ni queen fulani hivi....
but wakitokeza wazungu au waarabu....
unakuta mdada wa kiswahili anakuwa mnyonge mnyonge hivi...
i hate that
Ushamba tu...sindo wale wale wanaoacha wapenzi wao kwaajili ya wazungu then wanaishia kutumiwa n kuachwa!!
Hiyo statement ya wasichana wakiafrika wanachukia mwafrika akitoka na mzungu kwasababu ni ngumu wao kupata mzungu siwezi kuafikiana nayo hata nikiwa nimelala!
Ila mengine uliyosema ni kweli kabisa...kwa wale ambao akili zao sio indepent wanaamini weupe na uzungu ndio bora!!Binafsi naamini mimi ni bora kwahiyo hata aje mtu wa bluu hatonitisha....kinachotakiwa ni watu waanze kujiamini...otherwise tutakua kawa wale wamarekani wanaobleach watoto wao wadogo !