Darhotwire

[emoji16][emoji16]
Darhotwire na yule Askari wa samora Avenue.
Blogu ya pekee nilikuwa nasoma kwa kiswahili ilikuwa Issa michuzi
E mail address ilikuwa ni yahoo tu
Kuchat yahoo messenger
Kupiga simu nje unaenda cafe
Worldsex ilikuwa bonge la mtandao
Wengine tulikuwa tuna hack time watcher na jicho lake baya lile

Nakumbuka iringa kulikuwa na cybercafe pale bottoms up casino

Na nikiwa dar ni akiba then unamaliza siku na ice cream za Azam pale.
 
Baadae ikaja the utamu. Hii ilikuwa balaa jingine mjini hapa. Nadhani mmiliki wa Regency Park hotel hawezi isahau
 
Nilikuwa chuo kipindi hicho nikiwa bado mshamba ndio nimekuja Dar kuanza chuo nilikuwa nawaona tu mademu wakishinda humo Dar Hotwire et al mi zangu ilikuwa Yahoo tu

Utakua ulitokea kijijini KABISA! Au ile mikoa iliyokua nyuma sanaaa! Yani darhotwire umeenda kuijulia daslam? 😂😂😂😂
 
Hivi ile iringa net haikuwepo kipindi Cha darhotwire? Nimekuja iringa 2011 nkaikuta inabamba Sana!!
 
Sisi tuliozaliwa country side apo vumbi tu.[emoji23][emoji23]
 
Utakua ulitokea kijijini KABISA! Au ile mikoa iliyokua nyuma sanaaa! Yani darhotwire umeenda kuijulia daslam? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mwaka 2000 hata wewe nina uhakika ulikuwa huijui hiyo hotwire...Kiwira sio nyuma sana ni kijiji kilichoendelea kabisa pale Rungwe...binafsi kompyuta nimejua kutumia juzijuzi tu 2003.
 
Mie nilikuwa natumia jina ili ili na kipindi nilijiita kwa ufupi FD. Niliwahi kung'oa mtoto mmoja wa Mikocheni baadae akaenda Sweden ameolewa na mtasha huko
 
Moment niliyokuwa na enjoy ni kujiongezea muda dakika chache kabla muda wangu kuisha na kuendelea kuperuz

Hakyanan kuna ma 'IT admin' wengine bure kabisa!
 
Huwezi kuzungumzia Darhotwire ukaacha kuzungumzia Nakiete Mwenge au ITV, Ile ya ITV kulikuwana Shule ya MOA. MOA kulikuwa na Masista duu kwelikweli.
 
Nilikuwa napitia kusoma tu. Sikujua habari ya kutafuta wachumba humo.
Mie nilikuwa natumia jina ili ili na kipindi nilijiita kwa ufupi FD. Niliwahi kung'oa mtoto mmoja wa Mikocheni baadae akaenda Sweden ameolewa na mtasha huko
 
Mwaka 2000 hata wewe nina uhakika ulikuwa huijui hiyo hotwire...Kiwira sio nyuma sana ni kijiji kilichoendelea kabisa pale Rungwe...binafsi kompyuta nimejua kutumia juzijuzi tu 2003.
Mkuu mie email yangu ya Kwanza nimefungua 2001 ila compyuta haikua inshu kwangu shule nlosomea ilikua eneo la watu wenye uwezo so watoto kadhaa kwao walikua nazo
 
Enzi za win 95, 98 na 2000...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…