Darasa na 20%

Fredinho

JF-Expert Member
May 18, 2016
967
1,000
Hatua aliyofikia msanii Darasa imenikumbusha miaka kama 6 iliyopita wakati msanii 20% alipofikia kiwango chake cha juu mno kimuziki,pamoja na kuwa 20 pa alikuwa na nyimbo nzuri kama maisha ya bongo na mama neema lakini kilele chake cha mafanikio kimuziki kilifika rasmi mwaka 2010 baada ya kutoa nyimbo tatu kali: Ya nini malumbano,Ningekusamehe na 'wimbo wa taifa' TAMAA MBAYA.

Kila mtu alimjua 20 pa, kama zawadi kwa kazi yake nzuri watanzania walimpa tuzo 5 katika usiku ule wa kukumbukwa sana (ambao baada ya hapo uigizaji umekuwa mwingi kwa baadhi ya wasanii kupewa tuzo 6 au 7 ili tu ionekane nao wamevunja rekodi,ingawa mpaka leo mimi naamini ni 20% na nyimbo zake zilizogusa sana ndie msanii pekee ambae wingi wa tuzo zake ulimstahili).Kilichomtokea baada ya hapo hatujui lakini 20 amepotea sababu kuu inaweza kuwa menejimenti mbovu au kutokuwa na nidhamu ya kazi,kwani wengi tulijuwa kuwa lile lilikuwa jukwaa la 20 kupaa zaidi......

Darasa anapita njia ya 20% ila natamani kumuoana akifika juu juu na mbali zaidi.Licha ya kuwa Darasa amekuwa na nyimbo nzuri huko nyuma kama sikati tamaa na nishike mkono lakini ni kweli kuwa mwaka huu ndio umemtambulisha na kumpa darasa jukwaa kubwa zaidi kwa nyimbo zake tatu: Kama utanipenda,Too much na "wimbo wa taifa" MUZIKI (ni kama 20% mwaka 2010),Naimani kama Kili awards ikifanyika mwanzoni mwa mwaka ujao basi Darasa anaweza kuvunja rekodi ya tuzo kama 20% 2010 na hakuna atakaebisha.

Nategemea Darasa atapita njia tofauti na 20% na kama anavyosema mwenyewe ataendelea kutoa bampa to bampa,nategemea atatumia jukwaa hili na kilele hiki alichofikia kulipeleka gemu to the top top kama anavyodhamiria,kufika kileleni ni rahisi ila kudumu kileleni kumewashinda wengi.
KILA LA HERI DARASA
 

essaugervas

JF-Expert Member
Jun 25, 2016
586
250
historia ya 20% yupo wap,, na hanafanya nini saiz anayo rafiki yake mkibwa afande sele,kikubwa mimi nadhan kilichomwangusha 20% ni bangi na sembe,,
 

maalimu shewedy

JF-Expert Member
Jul 20, 2016
860
1,000
Huyu jamaa anaeleweka sana kwenye nyimbo zake, ila yeye mwenyewe anashindwa kujielewa kuwa anaimba nini.....!!

Tunamuhitaji Rais Rodrigo Duterte amnyooshe huyu mtu.
 

Jorochere

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
1,000
2,000
Huyu classroom hawez kudumu kwenye "game " juzi tu kala mzinga na gari,,, naskia ni cha pombe "kinoma"
 

Iceman 3D

JF-Expert Member
Sep 3, 2016
20,629
2,000
Ila 20% ki ukweli bangi za mwaka ule atakuwa ali ziagiza kwa kina bob marley huko jamaica kwenyewe, maana aliimba nyimbo zooote zina maana na zoote zika bamba, na kipindi hiko mziki ulikuwa hauna timu zisizo na makocha kama leo, ila mchizi alibamba kwe kweli
 

Betri yenye chaji

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
738
1,000
Naumia sana nikimkumbuka 20% alikua ni moja ya wasanii wangu hata hivo sijawai kuacha kusikiliza nyimbo zake, bangi na ujinga vimechangia kua alipo sasa
 

Fredinho

JF-Expert Member
May 18, 2016
967
1,000
Enzi za 20% kulikuwa hamna instagram. Insta inasaidia sana kupromote kazi za wasanii
Instagramu ni muhimu ila haiwezi kuwa sababu kiviiiile AY,FA,FID Q,Kiba,Diamond, Jide N.K walianza kabla ya insta na bado wanadunda tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom