Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,095
- 79,493
DARASA LA TATU B.
Anaandika, Robert Heriel.
''Ngengengeee........kengeeee''
Ilikuwa sauti ya kengele ya shule ya namba. Kengele hii hupigwa saa kumi na mbili na nusu asubuhi kuhesabu wanafunzi waliowahi. Na kama hukuwa umewahi basi viboko vingekuhusu.
Nilikimbia kwa upesi ili nisichelewe kuhesabiwa. Lakini nikagundua sitoweza kufika kwa wakati kama nitapitia kwenye lango kuu. Nikaona njia sahihi ni kuruka Uzio wa miiba jambo ambalo nilijua ni kosa kwa sheria za shule. Lakini sikujali nilichojali ni kupata namba. Nitajali vipi kwa asubuhi ile ilhali nilijua hakuna mwalimu ambaye muda huo angeniona. Nilifanikiwa kuruka lakini masikini darasa langu lilikuwa limeshahesabiwa namba.
Nilijaribu kumbembeleza Kiranja lakini alikataa kata kata. Nilitamani nimpige lakini nikaona nitaharibu zaidi.
Tulifanya Usafi kila darasa katika eneo lake. Baadaye tulienda kumwagilia bustani za shule kila mmoja alikuwa na bustani yake. Ilipendeza sana. Nilifikiri siku moja nami nitakuwa na nyumba yangu. Nitaifanyie usafi kama nilivyokuwa nafanya pale shuleni. Nyumba yangu nitaipanda bustani kama nilivyokuwa napanda bustani pale shuleni. Hayo yalikuwa mawazo yangu nikiwa nimesimama pembeni ya bustani yangu iliyokuwa imejaa vipepeo wazuri wenye rangi ya kuvutia.
Kengele iligongwa. Ilikuwa ni kengele ya kukaguliwa usafi. Tulienda Mstarini Naam ndiyo Paredi. Hofu ilitanda moyoni mwangu. Mapigo ya moyo yalikimbia upesi mno.
Niliogopa mno kutokana na kuwa Nguo zangu zilikuwa chafu. Sikufua. Usiseme nilikuwa mchafu. Utathubutuje kusema nilikuwa mchafu ilhali nyumbani kwetu zaidi ya wiki nzima Maji hayatoki katika kijiji chetu. Maji yaliyokuwepo ni maji ya kupikia na ya kuendea msalani. Sitaki kukumbuka kuwa nyumbani tulikosa hata pesa ya Sabuni. Nitafuaje nguo jamani embu niambieni mimi mwanafunzi wa Darasa la tatu B. Niambieni nijue.
Kama hiyo haitoshi hofu yangu ilichagizwa na kukosa namba ya kuwahi asubuhi. Looh! Tena ilikuwa ni zamu ya mwalimu desh desh. Mbona leo nakufa.
Tulifika Mstarini na kila darasa lilijipanga kwenye sehemu yake. Kiranja aliamrisha Guu pande. Kisha Guu sawa. Looh! Ama kweli ilikuwa Guu pande haswa na Guu sawa la kibabe. Soksi zangu za pundamilia zilizolegee Lastiki kwa uchakavu zilikuwa zikishuka chini. Loh! Masikini Taikon ndivyo ilivyo.
Sasa tuliimba wimbo wa Taifa. Wimbo wa taifa letu la Tanzania. Ulikuwa wimbo kama Sala na kuliombea taifa letu na Wananchi wa Tanzania. Wimbo wa taifa ulinifanya nitafakari mistari michache iliyoufanya moyo wangu uchangamke. ''Hekima, Umoja na amani hizi ni ngao zetu''
Hakika mshororo huu ulinipa amani ya moyo.
Tulimaliza nyimbo zote ikiwa ni pamoja na wimbo wa Tanzania Tanzania, Tazama Ramani, na Nyimbo ya Shule. Nyimbo hizo zilinisahaulisha uchafu niliokuwa nao. Zilinisahaulisha kosa la kuchelewa namba.
Ngoma zilianza kupigwa hiyo ilikuwa ishara ya Wachafu wapite mbele. Khaaaah! Moyoni niliomba angalau mvua inyeshe tuambiwe twende darasani. Thubutu ilikuwa ni dua la kuku walahi lililomkosa Mwewe.
Alafu wapiga wangoma walikuwa mahiri sana. Ngoma iliamsha hisia za hofu na wasiwasi mioyoni mwa sisi wachafu.
''Wenye kucha ndefu, Mbele. Nywele ndefu nao mbele. Wasiofua nguo Nisiwakute huko. Wasiopiga mswaki ole wao niwakute huko''
Ilikuwa sauti ya Mwalimu wa Zamu mwalimu Desh desh.
Wengine walitoka lakini mimi nilinyuti nikijifanya bedui lililoshindikana. Walimu walianza kuingia katikati ya mistari kutafuta waliojificha. Walijua tuu kuna wabishi na mabandidu ambao bila nguvu yasingetoka.
Chaaah! Mama wee kuna mwalimu alikuwa anakuja kule nilipokuwa. Ni kama alivuviwa na roho. Alinikamata sikio na kunipiga kwenzi. Wanafunzi wengine walinicheka. Hahahaha!! Wanafunzi wasafi hao. Wera wera!
Mara nikiwa mbele nikasikia Mwalimu mmoja jina kapuni akisema alafu wewe asubuhi umeruka uzio. Shika chini. Nikipigwa bakora nne za Shaashaa.
Tulichapwa Wachafu. Waliokosa namba za kuwahi asubuhi nako nimo. Taikon hukuwa na bahati.
Tulianza kwenda darasani kwa mchaka mchaka huku tukiimba nyimbo za kizalendo. Nakumbuka wimbo wa ''IDD AMIN AKIFA MIMI SIWEZI KULIA. NITAMTUPA KAGERA AWE CHAKULA CHA MAMBA''
Wimbo huo ulinirudisha nyumba miaka ya 1978/79 kwenye vita ya Kagera ambapo nchi ya Tanzania chini ya Mwl. Nyerere na nchi ya Uganda chini ya Dikteta IDD amini Dada, nchi hizi zilikuwa kwenye vita ambapo Nchi yetu ilipata ushindi mnono kutokana na Mashujaa wetu waliojitolea kumpiga Nduli Idd Amini Dada.
Wakati wengine wakiingia Darasani sisi Darasa la Tatu B Darasa letu lilikuwa nje. Tulikuwa tunasomea nje kutokana na uhaba wa madarasa. Tulikaa chini. Tulichafuka lakini tutafanya nini ikiwa hakina madawati. Alafu kesho yako unahitajika uje ukiwa msafi ilhaki kijiji hakina maji na nyumbani ni masikini hata kipande cha sabuni ni shida Loooh!!
Mwalimu wa hesabu aliingia. Sura yake ilionyesha kutofurahia kazi yake. Iweje afurahie ikiwa darasa lake ni nje. Vumbi lilimpuliza kila mara alijifuta na kitambaa cha mkononi. Nywele zote zilijaa vumbi.
Mara kwa mara alilalama na kututolea maneno ya karaha. Tulijua ni kwa sababu ya hali duni ya mazingira ya kazi yake. Kitabu kilikuwa ni kimoja ambacho sisi wanafunzi na mwalimu tulikuwa tunakigombania hali iliyokifanya kiwe kimechanika. Looh! Hilo ni darasa la tatu B.
Iweje tujua hesabu ikiwa hakuna vitabu. Iweje tujue kusoma ikiwa mazingira duni. Iweje tujue kuongea kimombo kwa hali ile.
Ilifika saa nne ilikuwa ni muda wa kunywa chai. Sikuwa na pesa ya kununulia kipande cha mkate na chai. Nilibaki kuzurura tuu. Wengi tulikuwa masikini. Ilibidi tuuze visheti na mabumunda ya waalimu na hapo tulijipatia posho ya andazi moja moja. Hata hivyo sio kila siku tilikuwa tukipewa.
Tuliingia tena darasani. Walimu waliingia lakini tulikuwa tumechoka sana. Nusu ya darasa lilikuwa limelala kwa uchovu wa njaa. Hilo ni darasa la tatu B.
Mitihani ilipofika nusu ya darasa walifeli. Iweje wafaulu ikiwa wana njaa. Wanasomea chini. Hawana vitabu. Waalimu wenyewe walikuwa wachache. Mwalimu mmoja anafundisha darasa la kwanza mpaka la saba tena masomo mawili loooh!
Mida ya jioni kurudi nyumbani iliwadia. Ilikuwa ni desturi kuona wanafunzi wanapigana mida hiyo. Tena kwa vile tulikuwa tukitembea kwa umbali mrefu tukipita katikati ya mashamba ya Matikiti, au miwa, Au mapapai. Basi tulikuwa tukiiba. Tungefanyaje ikiwa siku nzima hatukuwa tumekula kwa siku nzima. Looh!!
Siku moja tulikamatwa kwa kuiba kwenye shamba la matikiti. Tulipelekwa kituo cha polisi. Tulichapwa viboko na kuwekwa ndani. Huku wazazi wetu wakiwa wameenda kuitwa.
Walipofika walituchapa zaidi na kutoa fidia. Wazazi wangu, Ndugu zangu Wenyeviti wa kijiji na Mapolisi. Ni kweli tumeiba. Sisi ni watoto wenu lakini hatukupenda kufanya hivi. Ni njaa ndugu zangu. Tunajua wizi sio mzuri na kila siku mnatufundisha hivyo.
Watafanya nini Wazazi, Viongozi wa kijiji na mapolisi ikiwa ndio hali halisi ya umasikini.
Waliazimia kuwa wataitisha mkutano wa kijiji kujadili changamoto za Darasa la tatu B ili kuboresha elimu ya kijiji chetu.
Nilirudi nyumbani. Nilifua tuu kola ya shati na soksi. Usiku uliingia. Nilichukua Koroboi nakuanza kusoma hesabu na kujifunza kingereza. Lakini moshi wa kibatari ulikuwa ukinisumbua machoni na puani. Nilitamani kijiji chetu kiwe na umeme kama ilivyo kwa mjini.
Kibatari kilianza kuzima kwa kukosa mafuta ya taa. Mwanga ulianza kufifia na hatimaye kibatari kilizima na kiza kikatawala.
Ndivyo hali halisi ya Darasa la Tatu B.
Robert Heriel
Taikon Wa Fasihi
0693322300