Darasa la Siasa

Darasa la Siasa

Ili itikadi iweze kuenezwa/kuuzika ni lazima iende sambamba na hitaji kuu la umma unaoufanyia siasa, hapa ndipo vyama vyetu vinapofeli na kujikuta vinakuwa vyamsimu.

Kwa Afrika ya leo imekubwa na ombwe la vyama vya siasa kutokuwa na itikadi inayoaminiwa na wanachama wa vyama husika, Tatizo hili limeikumba hata siasa ya nchi yetu kwa sasa, Leo tuna vyama visivyokuwa na itikadi inayoeleweka ya vitendo.

CCM ilifanikiwa ki-itikadi chini ya mfumo wa chama kimoja kutokana na itikadi urithi ya kihafidhina iliyolenga ukombozi wa nchi na Utaifa (chini ya TANU); baadae siasa ya Ujamaa na kujitegemea ililenga kumwinua Mtanganyika.

Tangu kupigwa mweleka kwa azimio la Arusha mwaka 1992 na kuzaa azimio ls Zanzibar la mwaka 1992, CCM imekuwa inahubiri itikadi ya Ujamaa, lakini upande mwingine, inatekeleza itikadi ya soko huru, tena bila ya mchujo (ubepari).
Ukosefu huu wa msimamo kiitikadi wa ccm ndio tiketi ya mparaganyiko wa chama hiki na sasa kinaelekea ahera kabisa, huku chagizo la Ufisadi likisindikiza kifo hicho kwa ccm.

Lakini tuna vyama vilivyopata umaarufu kutokana na sababu ambazo hazihusiani na UMMA kubaini ubora wa itikadi ya chama baada ya kufananisha na itikadi za chama/vyama vingine vilivyopo, Badala yake, umaarufu wa vyama hivi unatokana na UMMA kuvikubali kwa sababu nyingine nje kabisa ya ubora wa itikadi zao. Mathalani ni umaarufu wa NCCR miaka ya 1995 na ule wa Chadema miaka ya 2005 – hadi sasa.
Ili somo letu liende vizuri ni vema nifafanue baadhi ya mambo katika hili, neno ‘kujipatia umaarufu’ badala ya ‘kujipatia mafanikio’, ni kwasababu tofauti na ‘mafanikio’ ambayo hutokana na itikadi, mara nyingi ‘umaarufu’ hutokana na vitu vya mpito, na huwa haudumu kwa muda mrefu.

Wanafunzi wangu mtakumbuka umaarufu wa NCCR miaka ya 1995; umaarufu wa Chadema hauna tofauti kubwa sana kwa sababu mafanikio tunayoyaona hayatokani na watu kuipokea kwa uthabiti wake itikadi ya chama, bali kwa vitu vya msimu ama matukio tu, ambavyo vinaweza meguka kirahisi.

Pia tuna vyama vilivyopata mafanikio kisiasa (sio umaarufu) kutokana na itikadi zao. Lakini vyama hivi vina udhaifu mmoja mkubwa juu ya itikadi zao: Itikadi hizi zinaendana na hali halisi ya upande mmoja tu wa jamii badala ya jamii nzima. Mathalani CUF na mafanikio ya kiitikadi visiwani ambayo imekuwa vigumu kuyarudia Bara. Mafanikio ya sasa ya CUF visiwani Zanzibar hayana tofauti kubwa na mafanikio ya TANU Tanganyika miaka 1960. Mafanikio ya CUF yanatokana na itikadi inayohanikizwa na Utaifa /Ukombozi dhidi ya Utawala wa Tanganyika. Pamoja na mafanikio yake huko Zanzibar, itikadi ya CUF haina mashiko upande wa Tanganyika kwakuwa haina hanikizo la hitaji la umma wa Watanganyika.


Udhaifu wa itikadi ya CUF utapitia hatua tatu za maisha: (1) Itikadi ya uhuru na Utaifa iliyozaa matunda hadi sasa Zanzibar, (2) baada ya utaifa kupatikana, CUF itakumbwa na changamoto za kutekeleza ahadi ilizozitoa wakati wa mapambano ya kudai utaifa kutoka Tanganyika na hali itazidi kuwa ngumu zaidi iwapo patatokea vyama vingine vya upinzani upande wa Zanzibar, (3) Iwapo vitajitokeza vyama vipya vyenye nguvu Zanzibar, itikadi ya CUF itazidi kuishiwa makali kutokana na kushindwa kutekeleza ahadi za ukombozi (kama ilivyotokea kwa CCM), na vyama vitabaki kukosoana huku CUF ikionekana sio lolote na vyama vya upinzani Zanzibar vitaendeleza kasumba yakusahau kabisa kwamba adui yao ni itikadi zenye kuishi maisha marefu.


Udhaifu huu wa ki-itikadi ndani ya vyama vya siasa unawakosesha wananchi fursa ya kuunda muono na mtazamo wa kisiasa unaofuatana na imani za kiitikadi zinazotambulika, na nyepesi kueleweka au kutofautisha. Hii ndio sababu kubwa inayopelekea wananchi kuunga mkono watu au vyama kishabiki zaidi kuliko kuunga mkono vyama hivyo kutokana na kushiba itikadi za vyama.

Tofauti na nchi zilizokomaa kisiasa, kwa Tanganyika na Zanzibar suala la wanachama kuhama hama vyama ni suala la kawaida. Kama vyama vingekuwa vinaendesha siasa za ki-itikadi, jambo hili lisingetokea kwani itikadi ya vyama nchini kwamjibu wa katiba zao inatofautiana kabisa.

Katika demokrasia iliyokomaa na yenye kuendeshwa ki-itikadi, kitendo cha wanasiasa kuteteana kwa sababu binafsi, au wanasiasa kuhama hama vyama, ni kitendo cha kujimaliza kisiasa. Ni katika nchi kama Tanganyika na Zanzibar pekee ambapo leo mwanasiasa anaweza jitoa CHADEMA, CCM, au NCCR na kwenda chama kingine bila ya hofu yoyote na akaendelea kuhudumu siasa za kitaifa tu. Hiki ni moja ya vielelezo vikubwa juu ya udhaifu wa vyama vyetu ki- itikadi.

Katika mazingira ya kawaida, kitendo cha kiongozi kuhama chama ni sawa na kukana imani (itikadi) yake na kukumbatia imani (itikadi) nyingine. Kwa mwanachama kufanya hivi sio jambo la hatari sana, lakini ni la hatari sana kwa viongozi.

Ni mapungufu haya ya ki-itikadi ndiyo hupelekea vyama vyetu kunadi ilani na sera zinazofanana, badala ya kuwa na ushindani mkali wa mtazamo unaotokana na itikadi. Katika siasa za sasa, vyama vyote vinashindana kwenda Ikulu, sio kuleta jambo jipya linalotokana na itikadi zao, bali kutekeleza sera zile zile za soko huria zilizojaa uholela.

Vyama pia vinapoteza muda mwingi sana kushindania yasiyo na umuhimu sana yakiwa yametapakaa kama vile haki za raia, utawala wa sheria, na vita dhidi ya ufisadi. Siasa juu ya masuala haya zimekosa uthabiti na kuungamana kutokana na udhaifu wa ki-itikadi. Vile vile kutokana na udhaifu wa ki-itikadi, umaarufu wa vyama mara nyingi (kama sio mara zote), unatokana zaidi na hulka za viongozi waliopo katika vyama hivyo, hasa nguvu zao katika jamii wanazotoka, bila ya kujali vyama wanavyotoka au itikadi wanazoziamini.

Mapungufu ya ki-itikadi yanapelekea vyama kushiriki katika ushindani wa siasa kama vile ni soko la kushindana ubora wa bidhaa. Vyama vinajikita zaidi katika ushindani wa nani ana sera na ilani bora zaidi kuliko mwenzake, bila ya uwiano na itikadi zao. Vyama vinajali zaidi kuja na bidhaa zinazoendana na mahitaji ya soko kwa wakati huo. Idara za uenezi, siasa na itikadi hazijishughulishi kuzunguka nchi nzima kujenga chama na kusambaza itikadi zao ili kushawishi wananchi kuwa wafuasi wa kudumu, na pia wawe wapiganaji wa kutetea na kulinda itikadi zao katika maeneo wanayoishi. Nguvu ya chama cha siasa ipo kwenye matawi na mashina, huko ndiko watu wengi wanaishi. Lakini cha ajabu ni kwamba, Idara za itikadi, siasa na uenezi, zinatumia muda mwingi kwenye Redio, TV na magazeti kama vile nguvu ya chama ndio zipo huko.
Mara nyingi vyama hukumbuka umuhimu wa matawi na mashina wakati wa uchaguzi tu.

Kwa Tanganyika na Zanzibar ya leo, udhaifu huu ndio unaozaa UMMA usiokuwa na msimamo wa kudumu wa kisiasa, na wengine wengi kutoona umuhimu wa kushiriki katika siasa. Wananchi wengi wamechoka na vyama vya siasa, kwani havitekelezi yanayohubiriwa. Isitoshe, mara nyingi, kauli na vitendo vya vyama vilivyopo hupishana. Hiki ni kikwazo kikubwa sana cha dalili ya zuio la ustawi endelevu wa vyama vyetu vya siasa, na demokrasia kwa ujumla.

Umuhimu wa Itikadi ya Chama
Kama moyo ulivyokuwa na umuhimu kwa uhai wa binadamu, itikadi ni moyo wa chama cha siasa. Moyo wa chama (itikadi) ndio husukuma damu ili kuviwezesha viungo vingine vya chama (katiba, kanuni, taratibu, mwongozo, ilani na sera), vifanye kazi zake kwa uhakika na ukamilifu. Itikadi utengeneza mtazamo, msimamo, malengo na matarajio kuhusu masuala mbali mbali yanayozunguka maisha ya jamii. Na mitazamo, misimamo, malengo na matarajio haya huathiri matendo na shughuli za kisiasa ndani ya jamii husika.
Wananchi hutegema sana itikadi kama moja ya njia zao kuu za kuwasaidia kuelewa masuala mbalimbali ya kiulimwengu, kwani itikadi hutoa mwongozo na kusaidia uwepo wa misingi ya kuratibu jinsi gani jamii iendeshe masuala yake ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, katika hali ya ufanisi, nidhamu na utulivu




Mwisho wa kipengele cha itikadi za vyama.


Itaendelea...
 
Baada ya sikukuu somo letu litaendelea

Naona unavyo lazimisha mada yako ipewe attention ila wapi.

Wana JF wamekupuuza; hakuna anae jiangaisha kusoma upuuzi wako.

Sasa umeamua ujaze comment zako kwenye uzi wako mwenyewe. Kweli umepuuzwa.

Acha kupoteza muda, kama huna "deal" kwenye kazi yako ya ufundi mchundo unaweza kunitafuta nikupe "deal" ya kuosha magari yangu.
 
Naona unavyo lazimisha mada yako ipewe attention ila wapi.

Wana JF wamekupuuza; hakuna anae jiangaisha kusoma upuuzi wako.

Sasa umeamua ujaze comment zako kwenye uzi wako mwenyewe. Kweli umepuuzwa.

Acha kupoteza muda, kama huna "deal" kwenye kazi yako ya ufundi mchundo unaweza kunitafuta nikupe "deal" ya kuosha magari yangu.

Hujui maana ya darasa, endelea kujitoa ufahamu ila wanaojua wametuliana wanafuatilia darasa hatua kwa hatua.
 
Naona unavyo lazimisha mada yako ipewe attention ila wapi.

Wana JF wamekupuuza; hakuna anae jiangaisha kusoma upuuzi wako.

Sasa umeamua ujaze comment zako kwenye uzi wako mwenyewe. Kweli umepuuzwa.

Acha kupoteza muda, kama huna "deal" kwenye kazi yako ya ufundi mchundo unaweza kunitafuta nikupe "deal" ya kuosha magari yangu.
Kka acha wvu ss twafaidka
 
Kka acha wvu ss twafaidka

Amepuuzwa sana huyu nashangaa anaandika na kujijibu mwenyewe.. Hivi ukiachana na kuandika makala za malalamishi na zisizo na facts huyu YERICKO NYERERE anajishughulisha na nini.?
 
Amepuuzwa sana huyu nashangaa anaandika na kujijibu mwenyewe.. Hivi ukiachana na kuandika makala za malalamishi na zisizo na facts huyu YERICKO NYERERE anajishughulisha na nini.?

Ni mfanyabiashara ninaemiliki kampuni ya ujenzi na umeme.

Somo linakukaa sawa au kunasehemu umeachwa?


Twende pamoja mkuu....
 
Ni mfanyabiashara ninaemiliki kampuni ya ujenzi na umeme.

Somo linakukaa sawa au kunasehemu umeachwa?


Twende pamoja mkuu....

Somo limenikaa sema unachoniuz ni kuisema vibaya ccm bila kusema mazur yake mkuu..

Tuko pamoja..
 
Somo limenikaa sema unachoniuz ni kuisema vibaya ccm bila kusema mazur yake mkuu..

Tuko pamoja..

Hayo kama yapo katika somo hili basi huo ndio uhalisia wa ccm, kama hayapo basi sio sehemu ya somo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom