Darasa la Siasa

Darasa la Siasa

...

.1. Maana ya siasa.

2. Itikadi za vyama vya siasa

3. Katiba za vyama vya siasa

4. Siasa za kisasa

5. Maisha ya mwanasiasa

Asante Kamanda

Nashauri kabla ya kuingia darasani zeLumumba wapimwe gauge ya ubongo ...i
 
Tunasubiri kwa hamu zote somo hilo...

Ahsante..

Karibu sana mkuu, somo letu litakuwa pana hivyo linaweza kuchukua mda mrefu sana kulimaliza,

Tutachambua kila kitu na kila mswahili atajua na kuamua.
 
Kabla hatujaangazia itikadi za vyama, nataka tujifunze na tuelewe, Itikadi ni nini?

Itikadi ni mkusanyiko wa imani unaoshirikiwa na kikundi cha watu fulani.

Kuna aina kuu mbili za itikadi:

Itikadi za kisiasa, na itikadi za kiepistemolojia (ni sehemu ya falsafa ambayo inahusu utafiti wa jinsi tunavyojua mambo).

Itikadi ya kisiasa ni upangiliaji unaohusu mawazo ya kimaadili na vipi nchi itaendeshwa.

Itikadi za kiepistemolojia ni upangiliaji unaohusu mawazo ya kifalsafa, ulimwengu, na jinsi gani watu wanapaswa kufanya maamuzi.

Kuna aina nyingi za itikadi. Moja kati ya hizo ni pamoja na Ukomunisti, Usoshalisti, na ubepari

Hizi ni itikadi kubwa sana za kiuchumi na kisiasa kwa ujumla katika dunia hii ya tatu.

Tutaendelea.........
 
Hoja ya wale wazee walioasisi muungano ilikuwa kuweka muundo ambao Wazanzibar hawatamezwa wala Tanganyika hawatabebeshwa mazigo kwa vile waliona
- Serikali moja Zanzibar watamezwa
- Serikali tatu Tanganyika watabebeshwa mzigo
Hivyo serikali mbili ndiyo suluhisho. Kila anayesimama ikiwa pamoja na Maria Sarungi,Tundu Lissu wanaleta porojo tu wameshindwa kuifunja hoja hii, achilia mbali hoja ya gharama ya ukubwa wa gharama ya kuendesha serikali tatu.
 
Hili nisehemu ya somo letu?
 
Tutasikia mengi mwaka huu.

Pamoja na kusikia mjumbe mmoja leo akieleza kuwa moja (anayetoka Zanzibar na kuunga S2) ya sababu ni "kutumia ardhi ya Tanganyika kama soko na kilimo" kama sababu za Muungano - bado naamini Muungano ulikusudiwa kulinda mapinduzi ya utawala wa kisultani ambao Nyerere alikuwa mmoja wa wapangaji na wawezeshaji!!

Nchi si idadi ya wananchi wala gharama za uendeshaji. Ikiwa Zanzibar ina uwezo wa kushughulikia mambo yasiyo ya muungano, inakuwaje Tanzania Bara (kimsingi ni Tanganyika) isiwe na uwezo huo?? Hii ni kero ya Muungano na wasioiona wanataka liwe ni upepo wa kisiasa - et utapaita.
 
Hili nisehemu ya somo letu?
- CUF hawana maslahi na muungano (kura za muungano) wanadhani itakuwa rahisi kushinda Zanzibar ikiwa pekee.
- Chadema hawana maslahi na muungano(kura za muungano) wanadhani itakuwa rahisi
kushinda Tanganyika ikiwa pekee.
- Hivyo lengo ni kuua muungano na kushinda uchaguzi hayo mengine wanazunguka tu.
 
Na ccm hatutaki kushindwa watoto wetu watakwenda wapi lazima watoto wa jk, mtoto waridhiwani mtoto kitukuu cha kawawa mjuukuu wa huseni mwinyi na mjukuu wa January' waendeleye kuongoza na lazima tuendeleye kuwambia ndio mzee kwani nini bwana ccm oyeeeeeee
 
Muezeshaji naomba kujua mahusiano ya siasa na propaganda.

Ili siasa itimilike nilazima ihuishwe na propaganda,

Kwakawaida propaganda ni sawa na mafuta kwenye gari,

Sasa propaganda nazo zipo za aina nyingi,

Kuna propanda ya siasa,
Propaganda ya kivita,
Propaganda ya uchumi
na Propaganda ya kiroho,

Kila propaganda ina miiko yake.
 
Tunaweza kusema pia siasa ni nani na anapata nini.Siasa inamhusu kila binadamu atake au asitake kama vile Aristotle alivyowahi kusema; "Human being by nature is a political animal".
 
kutoka kumshambulia Zitto kwenye mitandao mpaka kwenye somo la siasa/sihasa kwenye mitandao. kweli wazee wa chopa 3 kata 3 +kalenga/chalinze mmevurugwa vya kutosha.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom