Darasa la saba

Darasa la saba

genius

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2011
Posts
430
Reaction score
338
Darasa la saba wamemaliza mitihani yao mwisho. Hongera kwa watoto wote na pia wazazi na walimu. Hongera kubwa kwa jamii yote iliyowapa nafasi watoto kusoma kwa utulivu.

Wazazi wengi watakuwa busy kutafuta shule zenye majina makubwa na zenye ufaulu mkubwa. Ni jambo jema sana lakini, ningependa pia wazazi wenzangu mjue mambo machache:-

1./ Shule nyingi zenye majina makubwa zinafanya usahili kwa ajili ya kuchukua very smart and talented kids. Yaani wale wenye akili za ziada, hivyo kama mtoto wako ana akili sana ni sehemu sahihi kumpelekeka.

2./ Kwa kuwa wanachukua very smart pupils, na wanataka kushindana, mbio zao ni kumaliza syllabus mapema. Unakuta mwezi wa nne syllabus ya mwaka mzima imeisha wanaanza marudio ya papers etc.

Kwa mtoto avarage au mwenye uwezo wa kawaida hapa ndio anapata shida na confusion kwa maana hawezi kwenda na speed hizi.

3./ Zipo shule za kawaida, wanachukua watoto wa kawaida kabisa. Wana wafundisha taratibu pamoja na maswali. Wanatumia muda mrefu kumaliza syllabus lakini inawawezesha watoto kuelewa na kuvishika vyema.

Mwisho wa Mwaka wote wanakuwa wamemaliza sylabus na wote wanapata A au B. Shule inayowapeleka watoto taratibu na kwa kufuata sylabus pia zina tabia ya kuwabeba wasiojiweza mpaka mwisho, kwa kuwa fahari yao ni kufundisha na kubadili.

Ila shule zenu hizi zinazochuja watoto kila mhula fahari yao kubwa ni kushindana, kuitwa wa kwanza.

Kwao kuwa wa kwanza ni kuwashindilia watoto material kwa haraka na kuwafanyisha maswali mengi. Na matokeo yake watoto wengi wa shule hizi wakihama au kwenda vyuoni unawakuta wanakuwa wa kawaida sana na wengi wanakosa GPA nzuri. Kwa kuwa kufundisha watoto kwa ajili hii ya fasta ni nzuri kwa mitihani ya hapo kwa hapo lakini haijawahi kuwa bora kwa kubakiza maarifa ya muda mrefu na ukuaji wa akili.

Nchi za ulaya ziliacha siku nyingi sana kushindilia watoto sylabus ya Mwaka mmoja kwa miezi mitatu. Kwa kuwa haijawahi kuwafanya watoto kuwa bora zaidi ya kuwapa msongo wa mawazo.

Kumbuka maisha bora kabisa unayoweza kuishi duniani ni ya utoto. Watoto wapewe nafasi ya kusoma, kucheza na kufurahi. Wafundishwe na kucheza kwa kiasi.

Kwa wazazi walioko tayari kuanza kuambiwa mwezi March kuwa mtoto wako atarudia au mtafutie shule nyingine, basi ndio hizo shule za kushindana. March ni miezi miwili toka mtoto kaanza kufundishwa, kuna miezi nane mbele. Kwa nini mtoto hawezi, au walimu ndio hawawezi kwa kuwa hawako tayari kufundisha bali wanataka kushindana.
Wazazi tafuteni shule bora na sio shule za kwanza. Ukwanza wao ni kuwarudisha home wasioweza kusoma kwa haraka na kubakia na wanaoweza kushindana.

Usikubali kumfanya mwanao aamini hawezi wakati anaweza, usimwache akatishwe tamaa.

Nawatakia Wazazi wote selections njema za shule za watoto wetu.

Mwl. DI Haule
 
Wazazi these days wanaangalia “shule ipi ilifaulisha sana mwaka jana”. Yaani tunataka short cuts tu na quick fixes.

Shule zote zilizokuwa kwenye top10 matokeo ya form IV mwaka jana zimefanyisha watoto zaidi ya 2000 kuingia form one huku lengo ni kuchukua watoto wasiozidi 300
 
Upo sahihi kabisa maana wazazi kwa sasa vichwa vinachanganyikiwa hajui shule ipi bora na ipo bora shule.
 
Back
Top Bottom