VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Kama mtanzania mzalendo na mpenda demokrasia, mpendezwa wa siasa safi, upinzani imara na taifa lenye umoja, nimejitolea kutoa darasa hili la kisiasa kwa wapinzani wote nchini Tanzania. Darasa hili haliathiri kwa namna yoyote uanachama wangu wa CCM.
Darasa hili linalenga kuimarisha demokrasia na upinzani nchini mwetu ili tuweze kuchagua viongozi bora zaidi. Nitakuwa naeleza vitu hivi kwa kifupi sana na wapinzani watapaswa kujiongeza ili kuelewa nikisemacho.
HATUA YA KWANZA: Kubadili fikra za watanzania. Tangu kupata uhuru na kuanzishwa kwa CCM, watanzania wamejengwa katika fikra. Fikra ni kuamini bila kutetereka kiurahisi. Fikra hubadilishwa lakini taratibu na kwa umakini mkubwa. Huitajika ushawishi wa kutosha katika hilo.
Moja ya nguzo za CCM ni kuweza kujenga fikra kwa watanzania walio wengi kuwa WAJUMBE WA NYUMBA KUMI KUMI ni viongozi muhimu wa wananchi na hawaepukiki. Wajumbe hawa, mwanzoni, walikuwa ni viongozi wa kichama na kiserikali.
Baada ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa hapa Tanzania, Wajumbe hao walibaki kuwa ni viongozi wa kichama tu-viongozi wa wanaCCM. Hawa hawana mamlaka juu ya wasio wanachama wa CCM na hata wapinzani. Lakini, FIKRA iko tofauti. Wanaonwa ni wa kiserikali.
Kukubalika na kutumika kwa Wajumbe hawa wa nyumba kumi kumi (Wajumbe wa Shina) ni kukubalika kwa CCM. Wajumbe hawa 'huwamiliki' wananachi wao. Huwaambia cha kusema na kufanya. Hata uchaguzini, wananchi huchagua wanachochagua Wajumbe wao.
Wapinzani wanapaswa kuondoa FIKRA hii ya wananchi kuwaona Wajumbe wa Nyumba Kumi kuwa ni viongozi wa kiserikali. Hapo panahitajika ushawishi na elimu ya kutosha na kutisha. Si jambo dogo. Pakitikiswa hapo, CCM inatikiswa.
Nitaendelea.....
Mwafaaa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Nakala: Tetty