Daraja la kigamboni

Daraja la kigamboni

Jamani sio kupinga tu kizuri kikifanyika tusifie. Sio upinzani maana yake kupinga kila kitu.
 
Mbona kama limechukua mda mfupi zaidi au hilo ni la kupitishia vifaa wakati wanajenga daraja lenyewe??

Mkuu hilo sio daraja kiswahili hilo linaitwa jukwaa kwa ajili ya ujenzi wa hilo daraja. Jukwaa hilo litatumika kujenga daraja lenyewe na litatumika kwa gari la ujenzi kusimama kwenye hilo jukwaa na kusupply materials ya ujenzi wa daraja.
 
ngoja nikawahi viwanja huko kigamboni...manake daraja limesharahisisha maisha au labda tsunami iharibu mazingira,....
 
siri yenu nawamegea msimwambie mtu,kigamboni yote wakazi watahamishwa,afu litajengwa jiji lamaraha kama kule Miami au Honolulu,kiwe kitegauchumi cha sisiempty
 
nauliza tu
nondo za kujengea hazijatoka katika viwanda vilivofungiwa na TBS?
kama zimetoka china zitakuwa feki zaidi pia.
nina mashaka na ubora wa hilo daraja.


Hata nami nina mashaka sana na hizi dhana za kichina. Hili daraja likiisha, itanichukuwa sana muda kupita na gari kwenda kwa shangazi kule Mji Mwema. Yaani nipo nipo tu huku nikitafakari jinsi watu watakavyojirusha hapo darajani mara baada ya kwisha.
 
Jamani mmeona hiyo translation hapo kwenye bango?



Hahahahahahahha

Kiasi hao Maimuna wenzangu hapo wasivae helmeti maana hawajaelewa kilichomaanishwa

Tovuti? Tovuti gani?

Wao hawapo kwenye tovuti hapo
Nimeipenda sana hiyo tafsiri. Mswahili aliyepewa kazi hiyo ya ku tafsiri ni mhandisi aliyekuwa anachukia sana ngwini akidhani ni ukilaza
 
Sijui kwa nini mawazo hasi kuhusu ubora wa hili daraja yananijia sana kwamba daraja hili haliko kiwango?? mwenye uhakika anitoe wasiwasi na static calculations zinasemaje?
 
Back
Top Bottom