Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Sisi wabongo ni NOMA aisee! Tunaiba kuanzia ngazi ya familia hadi taifa. Daraja hili limeanza kutumika leo na limegharimu shilingi BILIONI 214 za Tanzania na tena ni fedha ambazo tumekopeshwa kwa hiyo tunadaiwa.
Cha kusikitisha, KAMERA nne (4) zilizowekwa ili kurekodi mwenendo wa watumiaji wa daraja hilo muhimu, ZIMESHAIBIWA. Hofu yangu ni kuwa wasije kuiba hadi DARAJA LENYEWE, maana hivi karibuni JPM alitangaza kuwa meli zaidi ya sitini (mijimeli haswaa) zilipotea bandarini katika mazingira ya kutatanisha.
Kuna mambo yanaudhi sana, Wakati unadhani umeiibia serikali kumbe unajiibia mwenyewe, utakamuliwa kodi hadi kwenye “pipi” ya mwanao dukani. “Bwege wewe”!
Mtatiro J
Source: DARAJA LA KIGAMBONI, KAMERA NNE... - Julius S. Mtatiro | Facebook
==================
Kanusho:
Habari hii SI KWELI. Hakuna Camera zilizoibiwa kwenye Daraja la Kigamboni.