Shoctopus
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 3,435
- 1,995
Assalamualaikum wana JF!
Moja kwa moja kwenye mada:
Mimi sio mkazi wa Kigamboni lakini nimefuatilia matatizo ya usafiri wa ferry boat kwa muda mrefu sioni jitihada za dhati za kutatua kero hii kikamilifu.
Mamlaka za Jiji la Dar es Salaam na Serikali kuu pamoja na wizara husika kwangu mimi ama hawana ubunifu au nia ya dhati ya kuondoa changamoto ya usafiri kwenda na kurudi kati ya city center na Kigamboni.
Nasikitika kusema kwamba hata daraja jipya la NSSF lilistahili kuwa pale ferry lakini bahati mbaya wahusika hawakuona hivyo, fedha nyingi zilitumika kwa ujenzi wake lakini tatizo la kivuko cha ferry liko pale pale! Ferry boat zinajaza watu wengi kupindukia na magari kiasi cha kuhatarisha maisha ya watu.
Bahati mbaya mamlaka husika nilizotaja hapo juu wakaona wajenge daraja lingine baharini! (Tanzanite bridge). Hapohapo wakaanzisha ujenzi wa mji mpya huko Kigamboni ambao nasikia umekwama! Sishangai! Kwa changamoto ya usafiri wa ferry boat na daraja la Kurasini/Kigamboni badala ya Kigamboni/CBD short cut, nani atahama Mbezi beach au Mikocheni kwenda Ndege village? Tena makazi ya hiyo village yenyewe ni kama makambi ya jeshi! (Yaani hii nayo ni topic pekee ya community planning disaster!)
Kwahiyo ukifanya hesabu za haraka kidogo za gharama za ujenzi wa madaraja ya Tanzanite na NSSF pamoja na hiyo Ndege village, fedha zake zingetosha kujenga underwater tunnel kati ya Kigamboni na CBD. Logic yake ni kwamba hii ni njia ya mkato (short cut) kwa wakazi wengi wa Kigamboni wanaotegemea usafiri wa daladala, kwa miguu na ferry boat zinazojaza kupindukia na kuhatarisha maisha yao kila siku.
Kuhusu tunnel yenyewe. Upande wa Kigamboni ingeanzia mbali kidogo penye nafasi ya kujenga lango la kuingia na kutoka kwa mgari hata kwa miguu.
Na upande wa pili tunnel ingetokezea Gymkhana area kwasababu hapajajaa majengo makubwa na kuna connection nzuri kwenda CBD, Mnazimoja, Salenda bridge nk. Vinginevyo hata Ikulu ingehama kupisha stesheni ya Kigamboni Tunnel. Na si vibaya jengo Hilo likaachwa kuwa sehemu ya stesheni na museum ili kuvutia utalii. (Hii nayo ni topic pekee ya historical sites preservation na strategic urban planning)
Baadhi yenu mtauliza maswali mengi kuhusu Ikulu na Gymkhana kuhamishwa nk. Kwanini Gymkhana isiende Kigamboni au mbele zaidi?
Na Ikulu si ipo Dodoma? Hamuoni kuwa mmepitwa na wakati kun'gan'gania pale ilipo kila siku panaingiliana na shughuli za wananchi kwa vin'gora na maofisi, mahakama, mahoteli, daladala na wapitanjia tu? Yaani utadhani kuna hatari fulani eneo lile! Kumbe ni ofisi na makazi ya Mkuu wa Nchi! Kwanini asitupishe? ( Hii nayo ni topic pekee ya kupunguza gharama za maintenance za Ikulu mbilimbili. Ni ufahari usio wa lazima.) Fedha itakayo patikana kwa kiingilio cha "Ikulu Museum" ingetumika kuiendeshea. Vile vile ikiwa na sehemu za kukodi kwa mikutano na huduma za restaurant nk.
Kuwenui wabunifu zaidi, hakuna soko la samaki la "kimataifa" pale, ni uchafu mtupu!
Mkifanya nilivyosema hapa juu na kushirikisha wataalamu haswa wa waterfront planning and development, eneo lile litakuwa kivutio cha kimataifa kweli! (Kama Rais SSH na msafara wake walifika au wangefika Pier 39, San Francisco alipokwenda California wangejua ninachosema.)
Kwahiyo mamlaka za Jiji la Dar es Salaam na Serikali kuu pamoja na wizara na wadau husika wakae pamoja na kuunda chombo kitakachohusika na project ya "DAR WATERFRONT REDEVELOPMENT AND KIGAMBONI TUNNEL, MASTER PLAN".
Nashauri alternative approaches kama ifuatavyo:
1. Apatikane msanifu ujenzi maarufu wa kimataifa kutoka Israel, USA, UK, au Canada, awe mshauri mkuu wa project. Ingawa sio lazima, vema akisaidiana na wataalamu wetu kama wapo.
2. Tutangaze 'project design competition' kwa level ya kimataifa na zawadi nono ili tupate proposal kadhaa toka wataalamu wa kimataifa. Kwa njia hii tutapata mawazo na solution kadha wa kadha zitakazopanua uelewa wa wataalamu wetu katika miradi ya aina hii. Hatuwezi kuwaachia akina Amos Makala na Jiji tu kwenye project kama hii, wataleta Coco beach ingine!
3. Tukiwa serious mradi huu utapata support ya wawekezaji wa ndani na nje ya Tz kwasababu utafungua new business opportunities kwa hoteli na biashara nyingine na kupanua ajira. Uboreshaji wa mazingira utavutia watalii na shughuli au fulsa mpya za kiuchumi Kigamboni na maeneo yote ya jiji.
Tumejaza magorofa marefu pale waterfront yoote, mengi ni maofisi ya Serikali iliyohamia Dodoma! Wakati wangeachia maeneo yote haya yangegeuzwa kuwa sehemu za biashara na vivutio vya utalii!
Kama ilivyo tuna Ikulu mbilimbili, na wizara za serikali nazo zina ofisi mbilimbili Dom na Dar, Za nini? Kiuhalisia Tz tuna makao makuu mawili ya Serikali! Huu ni ubadhirifu wa fedha za walipakodi! Kwanini tuendelee kukamuana matozo wakati vyanzo mbadala vya mapato tunavichezea?
Mamlaka husika za Jiji na Serikali pitieni ramani ya mwambao wote wa bahari kuanzia stesheni ya boti za Zanzibar mpaka Gymkhana na (Aga Khan hospital) na orodha ya majengo yenu eneo lote la waterfront yatakayopisha mradi huu. Kama vipi muyapige 'X' kabisa! Yaani yaingizwe kwenye redevelopment plan hii. Vinginevyo tutaendelea kudanganyana kwamba Dar ni jiji la kisasa wakati sivyo.
Najua Aga Khan hospital ni private property, sio rahisi kuhamishwa, lakini ni rahisi kuigeuza hoteli ikabaki kuwa yao ili wapewe eneo jingine wajenge hospitali kubwa kama inavyosemekana walikuwa waijenge Arusha.
Msongamano wa watu kwenye ferry boat hauleti picha nzuri na salama ya Jiji la kisasa!
Soko la samaki la feri halina hadhi ya muonekano, usafi, na mazingira kimataifa badala yake linaharibu mandhari ya eneo lote!
Kule n'gambo Kivukoni college zamani si ilikuwa hoteli? Isogezwe mbele kupisha project hii eneo hilo.
Ikulu haitakiwi kuwepo pale ni pafinyu na inaingiliana na traffic circulation eneo lile. Lakini ni hatari kwa wapitanjia kutokana na ulinzi wake na misafara kwenda na kurudi ya wakubwa.
Hospitali za Ocean road na Aga Khan zihame ili pawe na Sea front hotels and restaurants za kimataifa. Tutumie ocean view kwa WATALII badala ya WAGONJWA. Yaani mnataka watalii nao waende Coco beach!
Hii ni mifano tu ya jinsi ya kubadili sura ya jiji na maeneo haya ili yaendane na matumizi bora na sahihi ya fukwe zetu.
ULINZI, USAFI, USTAARABU NA UKARIMU.
Mambo haya manne yafanyiwe kazi ili sura ya Jiji la Dar ipande hadhi kimataifa. Solution mojawapo ni kupunguza kabisa msongamano CBD kwa kuboresha usafiri kwenda na kurudi toka maeneo yote pamoja na Kigamboni.
Zamani tulikuwa na taa za barabarani kuwezesha watu kwenda mjini kuvijnjari usiku. Sasahivi ni hatari kuwa town na fukweni usiku. Kwanza maeneo yote ni maofisi ya Serikali, mahakama na mahospitali. Usiku kuko giza na kimya kama makaburini au makanisani!
Tuwe wabunifu na wakarimu kwa fikra mbadala. Jeshi la polisi liboreshwe kifikra ili wenyeji na wageni wajisikie huru na salama jijini usiku na mchana. Mtake msitake panyarodi ni matokeo ya police failure, full stop!
KWAHIYO TUSEME: "KAZI IANZE"!