Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 427
- 666
Wananchi wa Segerea, Mtaa wa Twiga tunateseka sana kutokana na ubovu wa barabara, hasa wakati wa vipindi vya mvua. Maeneo mengi yamejaa mashimo na mvua inaponyesha hali huwa mbaya zaidi, kiasi cha kufanya usafiri kuwa wa tabu tupu hata kwa watembea kwa miguu.
Licha ya kuwa katika mtaa huu kuna barabara zinazohudumia maeneo muhimu kama makanisa ya Katoliki na KKKT pamoja na eneo la makaburi, bado hali ya barabara imekuwa changamoto kubwa kupitika, hasa wakati wa mvua.
Kwa sasa, eneo hili lina wakazi wengi na ni mtaa uliopo karibu na barabara kuu. Inashangaza kuona kuwa hakuna jitihada madhubuti za kuweka lami au kuhakikisha barabara hii inapitika bila changamoto.
Baadhi ya wadau ikiwemo makanisa tajwa wamekuwa wakijitolea kuboresha maeneo korofi lakini hali bado sio shwari. Hivyo sasa kunahitajika bajeti yenye fungu litakaloweza kuleta suluhu ya kudumu.
Rai yangu kwa Mbunge wa Jimbo la Segerea atusaidie kufikisha sauti yetu kwa mamlaka husika ili barabara hii iweze kuboreshwa na kuondoa kadhia tunayoipata, hasa katika vipindi vya mvua, lakini naamini mamlaka zitaiona hii taarifa, hivyo ni vyema zifuatilie na kuchukua hatua kutuepusha na hii kero.
Pia soma ~ Mbunge Agnesta Kaiza: Jimboni kwangu Segerea, mvua zikinyesha barabara nyingi hazipitiki