Dar: Ukikutwa gesti mchana unakamatwa. RC Makonda akanusha kuwatuma askari kufanya msako

Status
Not open for further replies.

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,961
Kwa sasa ukikutwa gesti mchana Dar unakmatwa kwa kosa la kulala muda wa kazi, polisi walikuwa wanafanya msako Tegeta kukamata watu hao



Kanusho la Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda

Akihojiwa kwenye kipindi cha Pb Clouds amesema hajawahi kutoa maagizo kama hayo, kinachofanyika ni Umbeya umbeya tu.

"Mimi kama Mwenyekiti wa ulinzi Na usalama siwezi kutoa maagizo kama haya, kuna watu wanafanya kazi viwandani wengine usiku hivyo wanahitaji kupumzika mchana huwezi kuwazuia"

Kinachofanyika ni Umbeya, siwezi kujibu hoja za kimbeya ni ujinga ....alimaliza Mh Makonda.!
 
Ukishakamatwa hivi tunategemea utapandandishwa kizimbani ndani ya masaa 24..na utashtakiwa kwa mujibu wa sheria..

Mie nasubiri hilo tu!
 
Mbona Kama siamin hii, Ina mana wanaotoka mkoani kuja kibiaashara Dar Na hawana ndugu wafikie wap?

Basi wapite Na kila Nyumba wakamate waliolala makwao.

Hii haijakaa poa na itazidi kufanya maisha ya Dar kibiashara kuwa magumu kweli.
 
Kwa hiyo aliyekesha na costa za mbeya dar akilala ili anunue mzigo kesho imekula kwake, madereva, wakisubiri magari yao yakitengenezwa baada ya safari ndefu wakimkuta kalala jela!
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom